Kapita Bila Kupingwa - Mgombea Pekee

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kazimwaga zake sera, ilani kanipatia,
Kaniomba zangu kura, moyo kuuchagulia,
Imekuwa werawera, nia kanitangazia,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!


Bila ya kuchakachua, mgombea kajinadi
Ahadi nimechambua, nimeshindwa ukaidi,
Mwishoni nimeamua, ni mgombea stadi,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!

Kura nimempatia, asubiri kuapishwa,
Wengine wamekimbia, yeye pekee kapishwa,
Hongera nampatia, wote mtafurahishwa,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!!

By. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Mgombea Pekee!
 
huyo unayemsema, kagombea chama gani
ni CUF au CHADEMA, tujulisheni jamani
ni baba au ni mama, jamani niambeni
Kama kapita hakupingwa, sio mshindi wa kweli

sio mshindi wa kweli, naomba kusisitiza
hakushinda kwa adili, kitu hiki chatatiza
nani kachukua ya pili, kama yeye ni wa kwanza
ushindi wa bure bure, mimi siufagilii
 
Kazimwaga zake sera, ilani kanipatia,
Kaniomba zangu kura, moyo kuuchagulia,
Imekuwa werawera, nia kanitangazia,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!

Wastahili pongezi, wa kijiji nakwambia
Ni wazi umemuenzi, sera zake kutambia
Aliupanga utenzi, kura zako kuomnea
Umechagua sawia, Mgombea anofaa


Bila ya kuchakachua, mgombea kajinadi
Ahadi nimechambua, nimeshindwa ukaidi,
Mwishoni nimeamua, ni mgombea stadi,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee![/QOUTE]

Hahitaji chakachua, kuuwini wako moyo
Tayari alijifua, kuukabili wako moyo
Alijua tachukua, jimbo la wako moyo
Wastahili pongezi, kupapa mtu shujaa


Kura nimempatia, asubiri kuapishwa,
Wengine wamekimbia, yeye pekee kapishwa,
Hongera nampatia, wote mtafurahishwa,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee!!

By. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Mgombea Pekee!

Kura siingeweza mnyima, ni stadi mashuhuri
Ameuweza mtima, akapanga ushauri
akajitoa mazima, kunasa wako uturi
Hongera zake hongera, mgombea wa pekee

Kila la heri kaka..........
 
Huyo ni laurence masha. Dhana ya mzee mwanakijiji hapa nilivyomuelewa mimi ni kwamba, hakuna mgombea hata mmoja aliyepita bila kupingwa, maana wananchi hawakuulizwa kama wanawahitaji au hapana, ilitakuwa kuwe na visanduku vya ndio au hapana, msingeamini masikio yenu, labda nusu yao wangekatariwa na wananchi. Mfano mdogo jimbo la prof anna tibaijuka yeye amepita dezo dezo, lakini chadema imepata madiwani 8 na ccm imeambulia madiwani 3. Je wananchi hao wangepewa nafasi ya kupiga ndio au hapana ingekuwaje? Tafakali.
 
Fumbo hilo ni zito lahitaji muda kulitafakari.....vinginevyo utachakachua majawabu yake.................
 
Wastahili pongezi, wa kijiji nakwambia
Ni wazi umemuenzi, sera zake kutambia
Aliupanga utenzi, kura zako kuomnea
Umechagua sawia, Mgombea anofaa


Bila ya kuchakachua, mgombea kajinadi
Ahadi nimechambua, nimeshindwa ukaidi,
Mwishoni nimeamua, ni mgombea stadi,
Kapita bila kupingwa, ni mgombea pekee![/QOUTE]

Hahitaji chakachua, kuuwini wako moyo
Tayari alijifua, kuukabili wako moyo
Alijua tachukua, jimbo la wako moyo
Wastahili pongezi, kupapa mtu shujaa

Kila la heri kaka..........

Kumbe MJ1 na wewe wamo lakini HAWAVUMI ............. :happy:
 
Back
Top Bottom