Kapigwa marufuku kusoma Arts ngazi ya Cheti

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
782
1,056
Wakuu,

Kuna dogo wa rafiki yangu hapa mtaani kapata division 4 ya 27, ana "C" tatu na "D" kwa Arts, Sayansi hajaambulia Kitu.

Shemeji yake (mume wa dada yake) anataka ampeleke advance private akasome HKL,
Dogo anang'ang'ania apelekwe DSJ kusomea 1 year certificate in Journalism coz anapenda maswala ya redio na TV sana.

Dada yake kamwambia,
"Sitaki kusikia UPUUZI huo wa Journalism hapa,
Nina rafiki zangu wengi Wana degree za hiyo kozi Wana miaka mitatu mtaani hawajapata ajira yake, Sembuse wewe na kisatifiketi Chako??

Utake usitake unaenda advance. Certificates za Arts Zote ni Njaa Tupu!" Dogo kanuna tangu Jana.

Kaja kazini kuniomba nikawashawishi Dada yake na shemeji yake wampeleke huko DSJ coz ni marafiki zangu sana, Nimemwambia nitaenda kwao KUONGEA nao usiku.

Wakuu, Nikaweke msimamo Gani Kwenye ushauri ili nisipate Lawama upande wowote?
 
Mwambie kijana aache utoto aende advance apate elimu maana anaonekana sharobaro anapenda mambo ya kuiga kikubwa akasome advance achukue degree ya hiko atakacho bt naamini akijua maisha na changamoto za ajira wa media hata degree hawez somea journalism. Pia mwambie ckuiz watu wenye redio na tv hawaajiri mapresenter kwa kuangalia elimu na vyeti bali wanaangalia kipaji kama anakipaji ataenda kwenye interview akipata huku anapiga kaz anasoma hiyo certificate kwa evening class.
 
Mwambie Huyo asinayemkataza Aache Kumkataza kusoma anacho kipenda, Siri ya mafanikio sio kufanya unachoambiwa ila ni hali na Mwamko wa kufanya unacho kipenda, kama anapenda Journalism bila shaka anatambua Changamoto na suluhu zake na Zaidi ana Ndoto Kubwa.. Advance anaenda kukariri kwa Sababu miaka Miwili anaenda kujifunza mambo ambayo walimu wanaomfundisha wanajua ni Kwa ajili ya NECTA ila Chuo anaenda uambiwa wapi atatumia na wakati huo huo anakitumia aneenda Kufanya Field kila mwaka kwa hiyo ni rahisi kufikia malengo.
Wazazi na walezi wasiofahamu maana halisi ya Elimu wanapaswa kujifunza Kuwa "A-levels are not only way to Universities kama ndio ndoto zao kuona watoto wao wanafikia kimasomo."
 
Back
Top Bottom