Kapata kazi ya 120,000/= afanyeje?

Dah hiyo hela nlikua nalipwa kwenye internships. Mshauri atafute kazi nyingine tu.
 
Kwani toka 2010 July hadi leo Dec 2013 kala Mavi?

Umeongea la msingi hapo kwenye Channel hapo. :poa: Tena kuna uwezekano wahindi hao wanampima tu. Hapa kuna mawili; 1.Wanajua tu kwa hii bei Tsh 120,000 mtu hawezi kuishi mjini. Akikubali, watajua huyu jamaa mwizi anataka kutuibia tu. 2.Anaweza kukubali wakafika wakabadirisha kiwango, akapata ata 200,000Tsh.

Ushauri: Mwambie Binamu Aende Tu... Ila inauma :angry:
Muhindi achana nae kaka, tena wanaweza wakampunguzia.... mimi hawa wahindi siwaamini kabisa, hawa watu hatuendani nao kabisa...
 
Mwambie atafute kazi, kusota ni part ya utafutaji especially kama huna bahati na unachemsha kwenye interview. Mshahara wa 120,000 ni unyonyaji na atakua anajidhalilisha mwenyewe pamoja na fani yake aliyosomea. He should be able to know his price and stick to it!
 
Wanajamii tuweni makini na kwenye majibu hapa, Kijana aanachotaka kujua ni gharama za maisha ili apime kama hiyo kazi inalipa au la?

Haya mengine sijui fanya kazi au achana nayo, ni maamuzi yake binafsi na si sahihi sana kumuingilia kwenye maamuzi yake.

Toeni gharama za maisha ya Morogoro mengine muachieni mwenyewe.
 
Take it from me kazi yangu ya kwanza laki na 30 net, jina la kampuni likanibeba nikaacha nikapata kwingine 220,000net hizo zote benefit napata pensheni na medical.
Hii ya pili at least 20,000 au 30,000 nlikuwa napata bonus.
Nikawapiga chini nkasota 5 months nkapata pengine 300,000 net same benefits nako nkawapiga chini.
Sa hivi nipo kwingine.Mwanzo mgumu hata mbuyu ulianza kama mchicha
 
Back
Top Bottom