Kapata kazi ya 120,000/= afanyeje?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habarini ndugu zangu..nimeombwa ushauri na mimi pia nawaombeni ninyi ushauri...kuna binamu yangu aliyehitimu IFM 2010 fani ya accountancy...baada ya kula msoto wa muda mrefu amepata ajira atakayokuwa analipwa 120,000/- kwa mwezi kwenye kampuni moja ya kihindi..itambidi atoke dar aende morogoro kama eneo lake la kazi...anaomba ushauri wenu wazoefu wa maisha kama hiyo kazi itakuwa na maslahi kwake! asanteni...!
 
Something is better than nothing. Hasa ukizingatia umesema jamaa kashasota kishenzi. Aende akaitumie elimu yake awaibie hao wahindi.
 
Kama hakuwa na kijiwe kinacholipa zaidi ya iyo aende, maana mwanzo wa ajira ndo huo. Ila kama cvyo aachane nayo na aendeleze gurudumu lake na pia yaweza ikawa ndo mtoko wenyewe pia
 
Duh japokuwa ajira ngumu but 120 jamani, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu, nyumba atalipa kodi bei gani, nauli bei gani, chakula bei gani na mavazi bei gani.
 
aende akafanye kazi morogoro kidogo maisha simple sio kama dar anaweza akafanya kazi vizuri akapandishwa hata cheo.... mimi mwenyewe nilifanya kazi morogoro kwa msharara wa 160,000 miaka mitatu lakini nilijipanga kiukweli na nilifurahia maisha kama mfanya kazi tu kikubwa ni malengo safari huanzisha na nyingine haman jinsi aende tu.
 
Roughly:

Chumba kwa mwezi: Tsh 10,000 (No umeme wala Maji)

Chakula per day minimu Tsh 3000 x 30 days= Tsh 90,000

Mafuta ya kupaka+ Sabuni+ Dawa ya Meno+ Vocha+ Vizagazaga vidogo vidogo vyoote= Tsh 10,000 per month.

Emergence yoyote kama Kuumwa, Kupoteza hela ata buku tu, aombee tu isimpate.

Kununua vitu kama nguo, Soda, Kuonga, Out asahau.

Jamani. Ebu muulize vema anapewa social.service gani hapo? Angalau chai na lunch vipo oficin? Kuna.nyumba ya mfanyakazi?
 
aende akafanye kazi morogoro kidogo maisha simple sio kama dar anaweza akafanya kazi vizuri akapandishwa hata cheo.... mimi mwenyewe nilifanya kazi morogoro kwa msharara wa 160,000 miaka mitatu lakini nilijipanga kiukweli na nilifurahia maisha kama mfanya kazi tu kikubwa ni malengo safari huanzisha na nyingine haman jinsi aende tu.

Umeongea ukweli mtupu.

ILA

Tuambie ilikua mwaka gani? Na Morogoro Manispaa au kule kijijini?
 
Asipo fanya kazi si atakula mavi? Fanya kazi mwanzo mgumu, lakini itasaidia kupata chanel nyingine.

Kwani toka 2010 July hadi leo Dec 2013 kala Mavi?

Umeongea la msingi hapo kwenye Channel hapo. :poa: Tena kuna uwezekano wahindi hao wanampima tu. Hapa kuna mawili; 1.Wanajua tu kwa hii bei Tsh 120,000 mtu hawezi kuishi mjini. Akikubali, watajua huyu jamaa mwizi anataka kutuibia tu. 2.Anaweza kukubali wakafika wakabadirisha kiwango, akapata ata 200,000Tsh.

Ushauri: Mwambie Binamu Aende Tu... Ila inauma :angry:
 
Hapa sio kijiwe cha Saisa,hata kije chama gani kama kichwa buyu ni buyu tu.Msingi ni kujituma

Jamaa we nenda kafanye kazi.
Mshahara huo lazima nyumba atakuwa amepewa kama Staff house.

We nani kakuambia ukiwa msomi usifanye kazi ya kipato kidogo,kama wewe unajiona msomi basi hizo degree siku hizi kama darasa la saba tu zilivyo mjini.

Na ndio mana hawa wenye kujiona wana Elimu ya Chuo wanazurura mjini wakidharau kazi za wenzo,wakati muuza maji wa mjini anaingiza hesabu kuliko yeye.
We muuza maji tu aningiza si chini ya Tsh:5,000 kwa siku wewe ukipishananae tu na vyeti vyako.

-Kwanza Itakusaidi kupata uzoefu na kujuana na watu
-Uaminifu ndio kitu muhim,na pia ndio sehem ya kuonyesha taalum yako.
-Kaa na wafanyakazi wenzako wote vizur bila kubagua,huwezi kujua nani mwema na nani atakuwa kuwa msaada na chanzo cha channel nyingine,ukiiishi vizuri unaweza kukuta mwenzako alietoka hapo na kwenda kwingine akakutafuta ili upate kazi yenye maslahi mazuri.Mwanzo uwe na pakushika kwanza.Wewe mwanaume na muhim ni kujituma na kufanyakazi yoyote halali,hao unaowaona waliofanikiwa wamepitia safari ndefu ila leo tunaona kama wamepata pesa juzi ila siri yao ipo moyoni.

-Pia usijifanye wewe ni msomi au mjuaji,be cool and friendly one to all staffs,hapo utaona njia ya mafanikio.Usifanye tu tamaa ya kutaka utajiri wa mapema wa kupanga wizi,hapo ni kwamba mungu hatokuwa pamoja na wewe.

-Mwisho ni kwamba Mshirikishe mungu katika kila nyendo yako ya maisha ili akupe ustahamilivu,subra na njia.
acha anasa,na kama ni mlevi acha kabisa kitu hicho.
Ni Bora upate kidogo lakini ni chako na chenye Kheir na baraka za Mungu ili mwisho wa maisha pia uwe mwema kwako.
 
Back
Top Bottom