kanywa sumu kwa kuudhiwa na mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kanywa sumu kwa kuudhiwa na mkewe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 17, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKAZI wa Mbezi Juu Mtoni jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la Shabani Kihundo (30), amekutwa amekufa akiwa chumbani kwa kuhisiwa kunywa sumu kwa kuudhiwa na mkewe katika ujumbe aliouacha chini ya kitanda.
  Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Bw. Charles Kenyela alisema kuwa, Kihundo alikutwa amekufa juzi chumbani kwake majira ya saa 7 mchana akiwa amelala kifudifudi.

  Kamanda Kenyela alidai kuwa, Kihundo aliacha ujumbe uliooneshwa kuwa kulikuwa na ugomvi kati yake na mkewe ujumbe aliokutwa chini ya kitanda chake.

  Kamanda Kenyela alifafanua kuwa ujumbe huo ulisomeka hivi: “Nimejiua kutokana na kutoelewana na mke wangu, nimeona nimuachie dunia name niondoke duniani nikatulize nafsi yangu japokuwa nilimpenda”

  “Nimekuachia hiyo nyumba,japo kuwa ulininyima haki yangu, mimi ni mwanachama wa NSSF na kadi yangu anayo mke wangu,

  “Yeye apewe milioni moja ili ziweze kumsaidia kwa sababu atakuwa na maisha magumu, nimeahca baiskeli apewe mdogo wake mke wangu pamoja, nguo na viatu”

  “Pia Samweli ananidai shilingi 28,000 asante”ulimaliza ujumbe huo

  Maiti imechukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  :smash::smash::smash::smash::smash:
   
 3. Kaka Mpendwa

  Kaka Mpendwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 771
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duh, dunia ina mambo??
  Threads nyingine watu wanataka kutoka nje ya ndoa wanatafuta justification, mwingine anataka kuzaa na ex-girlfriend, naona na huyu ndugu kaamua kujimaliza kabisa, kweli mambo ya mapenzi na ndo ni magumu sana..(naona kasi ya wanaume kujiua inaongezeka)
   
Loading...