Kanyaboya ya kariakoo!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanyaboya ya kariakoo!!!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Aug 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Kisa cha mchezo wa kanyaboya ulioingia mjini miaka ya themanin nakitu mjini Dar na hususani sehemu za Kariakoo.


  [​IMG]


  Kwanza ni lazima niweke wazi maana ya neno hilo lilipotokea na kwanini usanii au wizi wa kiaina fulani uitwe Kanyaboya.

  Ringberia Kanyaboya ni jamaa fulani wa kutoka nchini Burundi,kama mtakumbuka kuwa aliibuka mjini Dar miaka ya themanini na kitu akidai kuwa yeye ni mpiganaji ngumi wa kulipwa na alitafutiwa mapambano makubwa hapa nchini lakini baadaye ikajulikana kuwa si chochote ni muongo na hajawahi kupigana sehemu yeyete ile duniani na tayari aliisha kula pesa za watu na kutokomea gizani pasi ya kujulikana sehemu alipokwenda.

  Mpaka hivi leo ukimfanyia mtu usanii wa kumuibia kwa njia ya udanganyifu watakuita umemfanyia mtu Ukanyaboya.Nimewahi kufanya kazi ndani ya soko la Kariakoo ambako company niliyokuwa naifanyia kazi kufungua ofisi ndogo ndani ya soko hilo,nili bahatika kujifunza mambo mengi mle ndani na nimeshuhudia huo ukanyaboya jinsi unavyoendelea hususani katika mtaa wa Tandamti na nyamwezi ambao umepakana na soko pale mbele ya maduka ya washihiri,

  Targeti ya wezi hao ni watu kutoka miji midogo midogo wanaoingia mjini kutafuta mashati ya ndege,kama mnavyokumbuka fesheni ya mashati ya ndege ilivyoingia miaka ya mwisho sabini na tisa na kuendelea.

  wizi wenyewe ni ka hivi,kwanza unamuona mtu kasimama mbele ya duka na shati la ndege analionyesha kuwa analiuza kwa bei poa,na mara unaona anatokea wakuja kuulizia bei ya hilo shati la ndege na kupewa bei yake na baada ya kupatana kwa muda jamaa anakubaliana na bei ya mnunuzi ,yule jamaa anayeuza shati hayuko peke yake ni timu ya watu wawili mmoja ana simama mbali kidogo na hao wawilina mambo yakiwa tayari humpa sign yule jamaa yake aje na kijifurushi kilichojazwa matambara mabovu ndani yake kinacho fanana na kile kilichokunjwa na shati la ndege


  wakati wakuja anahesabu fedha ili kulilipia shati la ndege wale wawili tayari wameisha peana sign na yule mwenye shati la boya huja nalona kumpatia mwenzie kiujanja pasi na wakuja kuona baada ya hapo hulipia shati feki na kukabidhiwa mzigo wake wenye vitambara vibovu ndani yake ,nimeshuhudia wizi wa aina hii mbele ya macho yangu na kunawakati ilikuwa ni part ya entertainment yangu wakati jamaa zangu wakija nitembelea pale ofisini kwangu kama hatuna la kufanya huwachukuwa kwenda kuwapa burudani ya bure pale nje ya soko,ni kamchezo kabaya sana yaani mtu anapigwa Kanyaboya akiamini kuwa kweli amenunua shati la ndege ,kama mnavyojua mtu akiisha nunua kitu kipya kuna wakati atataka kukifungua na kukiangalia vizuri,yaani ni ka ma uchawi unamuona mtu kama hatua kumi anajaribu kufungua kile kifurushi alichonunua akiamini mle ndani kuna shati lake la ndege akikifungua kile kifurushi anakuta ni matambara na uchafu mweingine ndani yake,

  utamuona mtu anaangalia pale alipotoka kulinunua lile shati na tayari jamaa wameisha yeyuka gizani ,wakuja yule atakuja na kujaribu kumtafuta mtu aliyemuuzia shati pasi na kujua amuulize nani,yaani ni mchezo unaosikitisha sana na ni burudani moja ya kuchekesha sana ninatamani ka ningeweza kuufanyia document kwenye film yaani kurekodi kila hatua jinsi mtu anavyolizwa pesa yake ni kichekesho kikubwa
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mh.........
   
Loading...