Kanyaboya: Malipo ya dola milioni 300 na mtazamo wa Barrick vs tulichotangaziwa kuwa ni malipo ya "good faith"!

[QUOTEmylary Slip, post: 24154686, member: 84376"]"In the region of approximately total settlement for tax dispute."

Jiulize tulikuwa tunawadai kodi kiasi gani alafu haya malipo ya dola milioni 300 ndio yakaribie kumiliza mgogoro wote wa hilo deni.[/QUOTE]
Mbona nyie mlisema hiyo 425tilioni ni uwongo,Leo unarefer tena hapo hapo!!
Halafu hiyo habari mbona huendelei mbele inaposema hiyo siyo final position na bado mazungumzo yanaendelea?
 
Uoneshwe mkataba wewe kama nani?
Serikali haiendeshwi hivyo,kwamba kila kinachokubaliwa kiwekwe hadharani.
Walipa kodi wana haki ya kuona jinsi pesa zao zinavyotumika! Kwani serikali inapata wapi pesa? Serikali iliyowekwa madarakani na wananchi inapaswa kuwa submissive kwa wananchi.
 
Halafu hiyo habari mbona huendelei mbele inaposema hiyo siyo final position na bado mazungumzo yanaendelea?

Kwa hiyo miezi 3 ya mazungumzo nini kilichopatikana sasa hadi wajumbe kustahili kupewa vyeti?!? Mazungumzo yanaendelea kwa kuwepo na wajumbe wapya ama walewale? Kama walewale vipi kuhusu wao kufahamika na kuhongwa?!?
 
Kutoka kwenye kusema hatulipwi na tutashitakiwa mpaka kuwa mtafsiri wa maneno yasio rasmi.
Utahangaika sana.Tafuta hoja nyingine umeshindwa kwenye ndege,umeshindwa kwenye Makinikia,sasa tafuta hoja nyingine ya kupinga
Kwani ndege imeachiwa? Na ulivyo mweupe kichwani hujui kama wenye mbwa walitii tahadhari ya Lisu kiasi cha kuwaita Barrick kuwa ni "wanaume"! Tatizo vichwa vyenu vimejazwa ujinga na kila kitu mnashangilia. Leo fedha ambazo zingeenda kununulia madawa zinagharimia marudio ya uchaguzi uliosababishwa na kununua madiwani na mnunuzi anakuwa promoted! Hovyo kabisa nyie watu!
 


Fungua hiyo link hapo ujisomee.

Kuna sehemu inasomeka:

"Barrick sees $300 mln Acacia payment in the region of total settlement for tax dispute"

Kama huelewi hiyo lugha; hiyo phrase: "in the region of", maana yake ni sawa na neno "approximately"

Sasa soma sentensi nzima alafu utapata jibu.

Mange anasemaje kwani?
 
Kwa hiyo pande zote mbili zinategemea malipo yote baada ya mazungumzo yanayoendelea haayatakuwa mbali na hizo $300m wanazotaka kutanguliza kuonyesha Goodfaith (hawajatupa za bure).
 
Yaani wakuu nyie mnachokitafuta Ni negative issues tu za kuihusu serikali!

Wasi wasi wangu Ni kwamba wa Tanzania wakiaminishwa kwamba upinzani kazi Yao iliyobaki Ni hiyo basi mmejimaliza wenyewe!!

Hebu tafuteni matatizo halisi yanayowagusa wananchi wa chini moja kwa moja muyasemee, hapo ndipo kwenye pona yenu!

Vinginevyo Mzee wa kule kanyigo ukamuambia mzungu wa accasia ametoa dola Mln 300 badala ya dola nyingi alizokuwa anaiba, tena hizo dola mln 300 anatoa baada ya kubanwa Na Rais Magufuli, hapo itaonekana mshindi Ni Raisi Magufuli tu!! Mtaonekana waropokaji tu!!

Hakuna cha kutafuta negative issues mkuu!Wapinzani kwa uchungu mkubwa ndio waliopiga kelele za kuibiwa na hawa wazungu ndio serikali ikaona aibu na kuanza kulishughulikia kivyao vyao bila kuwahusisha hata wapinzani kana kwamba hawajui kinachoendelea!

Mbaya zaidi hata mawazo waliotoa namna ya kushughulikia hii issue yakapuuzwa na kuoenekana ndio maadui wa taifa hata kuliko hao wazungu wanao iba!

Hii Tanzania ni ya wate,watawala na wapinzani pia!Haiwezekani msamaria mwema akakueleza kuwa kuna samba anawamaliza mifugo wako,sasa badala ya kushikamana nae ili akuonyesha mahali huyo samba alipo na hata kushirikiana mbinu za kumuua,lkn badala yake ukamtenga na kukimbilia kumtafuta samba mwenyewe na kumwona na kumtangaza msamaria kuwa ni adui mkubwa!

Kuna siku tu wapinzani wataeleweka ila nina wasi wasi itakuwa too late!
 
Daa mmezidi sasa kila linalofanywa na serikali kwenu ni baya.Pambaneni na hali za vyama vyenu tuu.JPM kawapoteza.Sisi WATZ bwana.
 
Kutoka kwenye kusema hatulipwi na tutashitakiwa mpaka kuwa mtafsiri wa maneno yasio rasmi.
Utahangaika sana.Tafuta hoja nyingine umeshindwa kwenye ndege,umeshindwa kwenye Makinikia,sasa tafuta hoja nyingine ya kupinga
Good faith utakuwa umelipwa nini? Kutoka trillion 400 mpaka 600bn? 0.001% vilaza sana
 
Wamesema tena kuwa watalipa hizo bil 700 baada ya kuachiwa ule mchanga ambao kamati yetu tukufu ilipiga hesabu nzuri sana katika makontena yale 277 Taarifa ilisema kuwa
Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi. Viwango hivyo ni katiya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t. Wastani huu ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwaBandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani watani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni676 (USD307,292,720). Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,146,860,330,000 (USD 521,300,150).Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni1,147.
Sisi ni wajinga kweli
 
Back
Top Bottom