Kanusho la Taarifa yenye kichwa kinachosema "Kuna somo muhimu sana hapa:-Ally Hassan Mwinyi Baba wa hekima"

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Familia ya Abdallah Saidi Natepe, inapenda kuutarifu umma kuwa habari zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na mtu anaejifanya kuwa anaelimisha kwa makala yake yasemayo "Kuna somo muhimu sana hapa " hazina ukweli wowote na zinafaa kupuuzwa. Mwandishi wa habari hii kwa makusudi au kwa kutokuwa na weledi juu ya anachokiandika amejifedhehesha hata yeye mwenyewe kwa wale wanaojua ukweli, ila familia itatoa ufafanuzi kwa hoja zake chache alizoielekezea familia ya Natepe.

1. Mzee Natepe aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais mwaka 1977, akitokea Zanzibar na kupewa nyumba maeneo ya Upanga, nyumba ambayo ilikuwa inatumiwa na Marehemu Sokoine.

2 Mzee natepe aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani mwaka 1980 akibadilishana na Mzee Salmin Amour Juma na wala sio mzee Mwinyi kama inavyoelezwa.

3. Kipindi ambacho mzee wetu Mwinyi akiwa Raisi wa Zanzibar na pia Muungano, Mzee Natepe hakuhudumu kwenye nafasi yoyote ya uwaziri, alikuwa mtumishi katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mwisho ifahamike wazi Mzee wetu Mwinyi hajawahi kuishi nyumba ya Upanga ambayo Mzee Natepe aliishi hapo toka mwaka 1977 hadi alipofariki mwaka 2015. Kwa hiyo kama familia inamshauri muandishi ajifunze kutokana na kichwa cha habari yake kisemacho "Kuna somo muhimu hapa" ni kweli somo lipo la mwandishi kufanya utafiti wa kina na kujiridhisha kabla hajainua kalamu na kuitaarifu jamii.

HAPA CHINI NAAMBATISHA TAARIFA AMBAYO NIMEIKANUSHA. HII INAPASWA KUPUUZWA
Kuna somo muhimu sana hapa:-

ALLY HASSAN MWINYI BABA WA HEKIMA!!!


Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa Mzee Natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana waziri alieondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.

Ikampasa Mzee Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100, ya kwake wala sio mali ya serekali.

Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serikali, kweli Mzee Mwinyi akaviacha, akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais zanzibar. Natepe wakati anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia, Mzee Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.

Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea Mzee Mwinyi.

Mzee Mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua Baraza la Mawaziri akamteua tena Natepe kuwa Waziri pale pale Mambo ya Ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe siyo kwamba nakupenda sana; hapana, ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja Mzee Mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie?

Ndipo akaambiwa umetoka kwa natepe mzee mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.

Hapa kuna masomo makubwa matatu vema viongozi wetu wa sasa wakajipambanua kwayo ili tuende kwa weledi na umakini sana. Hata kwetu sisi wanadamu ni somo zuri sana la kujifunza.

Soma:



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Issue ndogo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo ndogo hata kidogo. Familia ya marehemu imefanya vizuri kutoa maelezo kwani sasa hivi nchi yetu imejaa vilaza wanaondika hadithi za vijiweni ambazo hazina ukweli wowote.

Mtu anakwenda kijiweni anasikiliza zile simulizi za ''eti nasikia....'' anaonda mbio mbio na kwenda kuandika bila kujali madhara yake. Huu usajili wa simu nadhani ukifanywa kwa umakini utawezesha wazushi kama hawa kukamatwa.
 
Siyo ndogo hata kidogo. Familia ya marehemu imefanya vizuri kutoa maelezo kwani sasa hivi nchi yetu imejaa vilaza wanaondika hadithi za vijiweni ambazo hazina ukweli wowote. Mtu anakwenda kijiweni anasikiliza zile simulizi za ''eti nasikia....'' anaonda mbio mbio na kwenda kuandika bila kujali madhara yake. Huu usajili wa simu nadhani ukifanywa kwa umakini utawezesha wazushi kama hawa kukamatwa.
Saa zingine JF kuna uzushi mwingi sana hasa kuhusiana na mambo ya historia au ya miaka ya nyuma. Kama usemavyo hii issue sio ndogo maana inahusiana na heshima ya mtu tena mwenye hadhi ya kitaifa na kubwa zaidi mwenyewe ameshatangulia mbele za haki.

Familia wamefanya jambo la maana kusafisha jina la Mzee wao na kiungwana natarajia mleta uzi ule wa awali ajitokeze na kuwaomba radhi wanafamilia wa Mzee Natepe.
 
Back
Top Bottom