Kanusho la habari potofu katika Tanzania Daima - 'JK alinda mawaziri'

Ikulu leo hii imetoa taarifa kwamba Rais Jakaya Kikwete hajaongea kitu chochote na waziri mkuu Mizengo Pinda chakushangaza gazeti la tanzania daima limeandika kwamba jk kamwambia Pinda huo ni upepo utapita tuamini lipi?

Sasa ulitegemea Tanzania daima waandike nini kama siyo kumponda JK. Yaani magazeti yote wao tu ndiyo walipata taarifa ya JK kuongea na PM kweli? hata mimi naamini ni uongo tu huo, tusubiri msemakweli kesho.
 
jana niliwambia rais hayuko dodoma watu wakagoma na kusikiliza habari za kizushi cha ile thread iliyowachanganya wwengi humu....repor imewasilishwa ikulu mda mfupi uliopita

Huwa nasikitishwa sana waandishi kutoa habari za kutengeneza na kupotosha. Hiyo haitusaidi sisi wananchi hata kidogo. Tujaribu kuweka uzalendo mbele kwa kuandika habari za kweli bila kupotosha. Kwa mfano; waandishi wa habari walimnukuu vibaya Jenister Mhagama pale alipohojiwa na kusema; " Wabunge wa CCM wamechukua maamuzi magumu" Pale alikuwa anamaanisha wamechukua maamuzi magumu katika michango yao ndani ya bunge. Watu wakaleta hapa mawaziri nane wajizulu. Huu ni ujinga na inakera sana kusoma habari ambayo baadae unagundua kuwa sio ya kweli.
 
Enyi kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu, mnaponukuu tusi, Nanyi mnatukana kwa midomo yenu wenyewe!!! Tazama mmetuambia kuwa JK ALINDA MAWAZIRI, kama hawalindi mbona hawajiuzulu? tuhuma za mawaziri zipo wazi sana.
 
Wameona kachemka ndo wanataka kumuosha

Vice versa is also true. Inawezekana kabisa Wabaya wa JK wameona yeye hajaguswa sasa wanataka kumchafua tu. Tumuache Rais afanye kazi zake kwa kufuata hekima, busara na kufuata misingi ya utawala bora.
 
...hapana bhana toeni kanusho jingine hili halijajitosheleza...inamaana pamoja na madudu yooote hayo waliyofanya mawaziri wake,ni kweli rais amekuja na kukaa kimya!?,wanataka kutwambia kuwa rais ameshidwa ata kum-beep au kumtumia sms Pinda kama kweli ameshidwa kwenda Dododoma kujua mambo yanaendaje!?...
 
Mie ningependa JMK AONGEE mwenyewe asitumie Watu wengine. Isitoshe kanusho hili lineelekea limeandikwa kwa pupa. Kuna makosa ya kisarufi mfano aya ya 3. HAZETI la Tanzania Daima,ndio nini hapa?

Hawa jokers washawahi kufanya makosa matatu, ya kisarufi na spelling katika communique ya sentensi moja kutayarisha tangazo la jina la Katibu Mkuu kiongozi mpya.

Kama Ikulu inashindwa kutoa a proofed one sentence communique unategemea rais ataweza kuwajibisha mawaziri?
 
Hivi wanaposema hivi wanafikiria wanaonesha umakini na weledi wa Rais?



yaani yote yanayoendelea kutokea nchini Rais hata kuzungumza na Waziri Mkuu wake hawajazungumza? Really?

Wakuu ushabiki wa hivi umezidi, tujaribu kupunguza na kuweka mizani. Hivi mtu anapowapotosha watanzania anatenda haki eti kwa sababu tu ikulu imejaa upuuzi? Upotoshaji habari si kitu cha kuchekewa hata kidogo. Kuunga mkono ujinga huu ni ujinga mara dufu.
 
kwa maana hiyo Rais hawalindi hao mawaziri hivyo kwa kuwa wanatakiwa kujiuzulu basi watajiuzulu. Mimi ndivyo nimeelewa kutokana na kanusho hili. Nasubiri kesho tutajua mbivu na mbichi si tumeambiwa kwamba kesho PM atatoa tamko!
hana jipya, kumbuka mgomo wa madaktari
 
Ile yule muhaya aka Ruyemamu ahalalishe cheo chake lazima atoe haya matamko la sivyo wabunge wa CDM watahoji .
 
Huwa nasikitishwa sana waandishi kutoa habari za kutengeneza na kupotosha. Hiyo haitusaidi sisi wananchi hata kidogo. Tujaribu kuweka uzalendo mbele kwa kuandika habari za kweli bila kupotosha. Kwa mfano; waandishi wa habari walimnukuu vibaya Jenister Mhagama pale alipohojiwa na kusema; " Wabunge wa CCM wamechukua maamuzi magumu" Pale alikuwa anamaanisha wamechukua maamuzi magumu katika michango yao ndani ya bunge. Watu wakaleta hapa mawaziri nane wajizulu. Huu ni ujinga na inakera sana kusoma habari ambayo baadae unagundua kuwa sio ya kweli.

Mkuu.. Jenister alihojiwa na kuonekana kwenye luninga akisema hayo maneno na wala hakunukuliwa vibaya.. Na ndo maana baada ya hapo Waandishi walimfuata Waziri Mkuu na kumuuliza utekelezaji wa maazimio hayo ya Wabunge wa CCM na PM akaahidi Jumatatu itatoka taarifa rasmi..
 
Dah, sasa ofisi ya rais nayo mbona inatuzingua.. Mbona watu tunafahamu JK alikuwa Dodoma na alifanya kikao hadi kufikia maamuzi ya kuwambia mawaziri wasijiuzuru iweje anakataa kutofanya mazungumzo?. Haya na tusubiri hiyo Jumatatu sijui J'nne kama kutakuwa na taarifa yoyote tofauti na uzushi huu wa gazeti Daima maana tunajua fika kwamba walitakiwa kujiuzuru na ngoma hiyo ilimsubiri yeye tu. Wakati mwingine ni busara kutojibu kila gazeti linapoandika..
Umejuaje?
 
Mimi nauliza swali moja: Kikwete alikuwepo Dodoma au ulikuwa ni uzushi? Maana kama alikuwepo Dodoma basi habari ya Tanzania Daima ni kweli. Lakini kama kweli Kikwete hakukanyaga Dodoma basi habari ya Tanzania Daima ni ya uongo kwani msingi wake habari yenyewe ni kwamba Kikwete alikutana na Pinda uso kwa uso!!
 
kazi zake kwa kufuata hekima, busara na kufuata misingi ya utawala bora.

Mkuu, hv JK unayesema kwamba aachwe afanye kazi zake kwa kufuata hekima, busara na kufuata misingi ya utawala bora ni yupi huyo?! ni huyu JK nayemfahamu au ni JK mwingine?! Kama unamzungumzia huyu JK ambaye hata mimi namfahamu basi naomba uniwie radhi kabisa kwa kutofautiana na wewe ktk hili manake JK nayemfahamu mimi angelikuwa anafanya hayo uyasemayo basi leo hii tusingeliongea haya!
 
ikulumawasiliano@yahoo.com...???????? Ikulu wanatumia yahoo kama email address..? Sehemu nyeti.. Duh.. Mie na kikampuni changu cha mkononi ninatumia domain ya my company..







download.png





 
Jk ukiwalinda hao mawaziri amini nakuambia chama kitafia mikononi mwako mwenyewe,hao mawaziri hawabebeki kabisaaaa! Hakuna cha upepo wala mvuaaaa!

hivi takukuru wapo mbona ilikuwa kazi yao kesho wanajiuzuru wakitoka nje ya viwanja vya bunge wana wakamata na kesho kutwa mahakamani hatuwezi kufunga majambazi ili hali waizi wa bata tuna wauwa kwanini tusifanye hivyo kahawa majambazi mavaa suti
 
kazi zake kwa kufuata hekima, busara na kufuata misingi ya utawala bora.

Mkuu, hv JK unayesema kwamba aachwe afanye kazi zake kwa kufuata hekima, busara na kufuata misingi ya utawala bora ni yupi huyo?! ni huyu JK nayemfahamu au ni JK mwingine?! Kama unamzungumzia huyu JK ambaye hata mimi namfahamu basi naomba uniwie radhi kabisa kwa kutofautiana na wewe ktk hili manake JK nayemfahamu mimi angelikuwa anafanya hayo uyasemayo basi leo hii tusingeliongea haya!
 
Hofu ni kitu kibaya sana lakini na uongo ni sumu mbaya sana.Hii nchi imejaa watu wenye hofu na waliobobea kwenye uongo. Nakumbuka kusimama mchana wa jua kali mbele ya Kituo cha Polisi Buguruni mwaka 1986 (?) kungojea mtu "aliyegeuka" nyoka aonyeshwe!! Kesho yake magazeti yalikanusha kwamba hakuna mtu aliyegeuka nyoka, lakini mpaka leo hii kuna watu wanaamini kwamba kuna mtu Buguruni aligeuka nyoka!!

No research No right to speak!!
 
Back
Top Bottom