Kanusho la habari potofu katika Tanzania Daima - 'JK alinda mawaziri'

Hivi wanaposema hivi wanafikiria wanaonesha umakini na weledi wa Rais?

Tunachukua nafasi hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo hazeti la Tanzania Daima Jumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.

yaani yote yanayoendelea kutokea nchini Rais hata kuzungumza na Waziri Mkuu wake hawajazungumza? Really?
 
Hivi wanaposema hivi wanafikiria wanaonesha umakini na weledi wa Rais? yaani yote yanayoendelea kutokea nchini Rais hata kuzungumza na Waziri Mkuu wake hawajazungumza? Really?

I wonder..ina maana raisi tangu yupo Brazil hakuwa na notification juu ya yanayoendelea nchini?. this is a morning joke!.
 
Nature abhorrs a vacuum. Kama Ikulu haiko tayari kutoa habari kwa kasi inayotakiwa na enzi hii, wanahabari watatunga vitu hata kwa nia ya kulazimisha communiques kama hizi kutoka kwa Salva.Not that I support fabrications, just pointing out an inescapable truism.

Website - not cobwebsite- ya Ikulu iko wapi?
 
Umeanza lini kumwamini Salva au Premi?

jana kikwete hakuwa dodoma..na jana hiyo usiku nilisema kwenye thread ile iliyosema jk atua dodoma...ile thread ilijaza sumu sana na gazeti la tz daima wakatoa habari pale na kuchapicha gazetini
 
Kuwalinda anawalinda! wala Tanzania daima haijakosea. Hivi kweli Ikulu mnafikiri nchi hii ni ya Mang'ombe! Hivi mwenye macho anaambiwa tazama! Hili si jambo hata la kujadili! Pathetic!

Ilibidi tu mtoe tamko ili Kumlinda! What a shame! Unfortunately hao mnaowaona Man'gombe wameanza kubadilika! Mmesahau hata huyu binadamu wa leo aliwahi kuwa Sokwe! :A S angry:
 
Mkuu Kimbunga,

Hii kitu itamuweka pabaya JK, maana vituo vyote vya Television na Radio viliweka habari hiyo kama BREAKING NEWS, magazeti yote nayo yakaiweka kama Habari Kuu, kwamba mawaziri 8 washinikizwa kuachia ngazi. Sasa iwapo mpaka kufikia Jumatatu hakutatokea kitu, then Ikulu itakuwa imewalinda.

Mkuu ni kweli lakini tumeambiwa PM atatoa taarifa kesho bila shaka kuhusu hilo sakata. Habari ya kujiuzulu hao wanane ilikuwa ya majuzi jabari iliyokanushwa ni ya JK kusemekana anawalinds kwa mujibu wa hilo gazeti la Tanzania Daima. Ni kwa nini Ikulu isingesubiri hadi tupate taarifa ya PM manake kesho si mbali.

Najua wanakanusha kwa kuwa Rais ametajwa lakini wangesubiri japo kesho tuona PM anasemaje.
 
Jamani mbona hii idara ya Mawasiliano ya Ikulu inaudhalilisha Uraisi? Kama ni kweli kwamba Raisi hajaongea na waziri mkuu baada ya yaliojiri bungeni wakati huu wa Skype n.k basi tatizo lililopo ni kubwa sana. Kwa taarifa hii inamaana raisi hajaanza kufanyia kazi suala linaloweza kusababisha kuvunjika kwa baraza la mawaziri. Inamaana Raisi asiyelinda Uongozi na nafasi yake kuongoza sio kiongozi.
 
Kurugenzi ya mawasiliani ni kwa ajili ya kukanusha tu taarifa, hamnaga habari nyingine,, yani kila nikiona ni Raisi hajasaini, raisi hajasema, Raisi hausiki etc, niki kitengo ni kama cha propaganda iviiii
 
Hivi wanaposema hivi wanafikiria wanaonesha umakini na weledi wa Rais?



yaani yote yanayoendelea kutokea nchini Rais hata kuzungumza na Waziri Mkuu wake hawajazungumza? Really?

Hapo ndipo nimeishiwa nguvu! Kama ingekuwa nchi zenye utamaduni wa kuwajibika, rais alitakiwa AKATISHE ziara yake huko Brazil na kurudi nyumbani kutatua matatizo. Serikali yake inasambaratikana halafu tunaambiwa hajui?
 
Msishangae. Ngoma nzito huenda Kikwete ameona kuwa ataendelea kucheza makidamakida wakati Makinda ashajaribu na kukwama anaweza kuondoka na maji hasa ikichukuliwa kuwa Lowassa angependa hili litokee. Hivyo Kikwete anazidi kuramba matapishi yake.
 
Na hiyo taarifa ni KWA HISANI YA WATU WAMAREKANI?hamuoni aibu kumtangaza Vasco Da Gama na safari zake na ni ubadhirifu wa fedha au Kujua hilo NAKO KUNAHITAJI WAWEKEZAJI TOKA NJE?KIKWETE hajui kutoa vipaumbele angalia kati ya yanayoendelea bungeni na kuhudhuria mazishi nje ya nchi wakati ana makamu wake!
 
Jk ukiwalinda hao mawaziri amini nakuambia chama kitafia mikononi mwako mwenyewe,hao mawaziri hawabebeki kabisaaaa! Hakuna cha upepo wala mvuaaaa!
 
Aibu kubwa kumbe Mfutakamba na Nundu hawaelewani. Nundu anamtuhumu Mfutakamba kwa kulipiwa gharama na kampuni ya CCC kwenda Uchina na Mauritania kuangalia miradi yao na aliporudi akaandika taarifa ya kuipendelea CCC!

Duh serikali yetu haiko pamoja.
 
Back
Top Bottom