Kanusho la habari potofu katika Tanzania Daima - 'JK alinda mawaziri'

Dah, sasa ofisi ya rais nayo mbona inatuzingua.. Mbona watu tunafahamu JK alikuwa Dodoma na alifanya kikao hadi kufikia maamuzi ya kuwambia mawaziri wasijiuzuru iweje anakataa kutofanya mazungumzo?. Haya na tusubiri hiyo Jumatatu sijui J'nne kama kutakuwa na taarifa yoyote tofauti na uzushi huu wa gazeti Daima maana tunajua fika kwamba walitakiwa kujiuzuru na ngoma hiyo ilimsubiri yeye tu. Wakati mwingine ni busara kutojibu kila gazeti linapoandika..
 
''nimembeep mh. Rais, akitua tu johanesburg atanipigia''
hayo yalikuwa maneno ya Pinda wakati wa sakata la Jairo. Kama hayo yalikuwa mawasiliano, hakuna budi kwamba waliwasiliana.

Ni dhahiri kwamba Jk alikuwa ametingisha kiberiti kujua kama imejaa. Baada ya kugundua kumbe ni noma kaamua kutuma kurugenze yake kukanusha.
Mkulu ameshikwa nyeti hakuna pa kufurukuta
 
hiki kitengo cha mawasiliano kimejaa wakurupukaji na wababaishaji sana.

hivi taarifa gani hii imechanganya lugha mbili: Kiingereza (upande wa anwani) na Kiswahili (upande wa ujumbe). sisi tusiojuwa kiingereza hata cha kuombea maji hamuoni kama mnatuchanganya?


habari ni ya kweli. hata hao mawaziri wezi waking'oka, habari itabaki kuwa ya kweli.

nani asiyejua sarakasi za magamba?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
ile thread jana jion humu imejaza uongo mkubwa na na tulipojaribu kukanusha kuwa jk hayuko dodoma watu wakabisha na hawa tanzania daima walitolea humu habari na kuandika gazetini
 
Mkistaajabu ya Mussa mtaona ya Firauni ! Kwani huyu Baba yake Mwanaasha ndio mnamjua leo ? Mbona Jairo katulia tu na mambo yamekwisha huo ni upepo tu kama anavyosemegaa
 
Kwanini ikulu imejibu hili upesi saana?

By the way, maoni yeyote au hatua yoyote itakayochukuliwa watanzania watajua ni ya kweli au la!!! wasipotemwa ujue tanzania daima walikuwa wa kweli.

Halafu ikiwa vinginevyo ofcoarse ndivyo tunavyotegemea mawaziri hawatawajibishwa kwa lolote basi pinda pinda usichafuke aisee mara ngapi umeshauri nchi, rais ikawa inagoma jiuzuli tu. hayo ndo maamuzi magumu teh teh teh.

Kikwete wajibika aisee too much vasco does not help this country, ivi huwa unaenda huko kwa ajili ya semina au misaada? Maana kama ni misaada nchi wahisani wamegoma na ikiwa ni semina mbona unazo nyingi kuliko za watendaji? Sasa hizo semina una-apply wapi?
 
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.
Duh!

Kama ni kweli JK hajaonana na Pinda atakuwa rais wa ajabu sana, nilidhani kwa mtafaruku huu ingekuwa ni kama dharura au kwa haraka sana kukutana na pm wake ili kuweka mambo sawa kumbe yeye kaja kauchuna tu, hii ni dharau sana hasa kwa wabunge wa CCM zidhani kama ataweza kuwasikiliza pengine iwapo hajawasikiliza hata pale wanapotaka kuivunja serikali yake.

Hii kali kwenye msiba wa Kanumba alijihimu upesi upesi, kwenye kero za wabongo karudi na kuuchapa usingizi ikulu
 
Jamani habari za uzushi kama hizi zinaweza kuleta machafuko katika taifa letu,nawaomba wanaohusika serikalini wachukue atue kali za kisheria dhidi ya gazeti la Tanzania Daima ili isijetokea tena!
 
ile thread jana jion humu imejaza uongo mkubwa na na tulipojaribu kukanusha kuwa jk hayuko dodoma watu wakabisha na hawa tanzania daima walitolea humu habari na kuandika gazetini
nani kakwambia hayuko dodoma? acha upuuuzi? sasa unazani aliporudi alieenda bagamoyo?
 
Wanajikosha tu, kwani hawawezi kuongea kwa simu na kumpa kila kinacho endelea, Mbona mawaziri wemegoma kujiuzuru?
 
jana niliwambia rais hayuko dodoma watu wakagoma na kusikiliza habari za kizushi cha ile thread iliyowachanganya wwengi humu....repor imewasilishwa ikulu mda mfupi uliopita
Umeanza lini kumwamini Salva au Premi?
 
Mimi naamini hii habari ni ya kweli lkn Mukulu hakutegemea itoke ilivyo na anaona upepo unaendelea kuvuma kwa kasi zaidi ya alivyotegemea ndo maana akaja na hoja ya kukanusha. Ngoja tuone hiyo kesho
 
Hili linasababishwa na usiri mkubwa wa msanii na Serikali yote katika kutaka kuficha mambo yanayojiri ndani ya Seikali hii fisadi.

Kama wangekuwa wawazi katika kulifahamisha Taifa kila kinachojiri bila kutaka kuweka pazia kubwa basi kungekuwa hakuna sababu ya kuandika habari ambazo ni nusu nusu. Hivyo wa kulaumiwa hapa si vyombo vya habari bali ni hii "Siri Kali" fisadi ya msanii.
 
kwa maana hiyo Rais hawalindi hao mawaziri hivyo kwa kuwa wanatakiwa kujiuzulu basi watajiuzulu. Mimi ndivyo nimeelewa kutokana na kanusho hili. Nasubiri kesho tutajua mbivu na mbichi si tumeambiwa kwamba kesho PM atatoa tamko!

Mkuu Kimbunga,

Hii kitu itamuweka pabaya JK, maana vituo vyote vya Television na Radio viliweka habari hiyo kama BREAKING NEWS, magazeti yote nayo yakaiweka kama Habari Kuu, kwamba mawaziri 8 washinikizwa kuachia ngazi. Sasa iwapo mpaka kufikia Jumatatu hakutatokea kitu, then Ikulu itakuwa imewalinda.
 
Last edited by a moderator:
Jamani habari za uzushi kama hizi zinaweza kuleta machafuko katika taifa letu,nawaomba wanaohusika serikalini wachukue atue kali za kisheria dhidi ya gazeti la Tanzania Daima ili isijetokea tena!
Tanzani daima waweke ushahidi wa kilichoandikwa,hakuna hadaa zama hizi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
ile thread jana jion humu imejaza uongo mkubwa na na tulipojaribu kukanusha kuwa jk hayuko dodoma watu wakabisha na hawa tanzania daima walitolea humu habari na kuandika gazetini
Unataka wapate habari wapi? Nyumbani kwako? Hiyo habari ni ya ukweli
 
At least hiyo habari imemtoa nyoka pangoni. Bila makala hiyo ya Tanzania Daima tusingesikia chochote kutoka Ikulu.
Huu ni uchokonozi mzuri. Tusubiri kesho.

Mkuu Jasusi itakuwa poa sana kama hicho kinachotakiwa kutangaziwa Taifa kesho kitavuja na kuwekwa hapa jamvini kabla Jumapili hii haijaisha ili tu kuikomoa hii Serikali fisadi na usiri wake mkubwa wa kuficha habari muhimu kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom