Kanusho la habari potofu katika Tanzania Daima - 'JK alinda mawaziri'

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


SUNDAY, APRIL 22, 2012

KANUSHO LA HABARI POTOFU KATIKA TANZANIA DAIMA AMBALO LEO LINA KICHWA CHA HABARI KISOMEKACHO "JK.ALINDA MAWAZIRI"



download.png



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Tanzania Daima la leo Jumapili Aprili 22, 2012 lina habari katika ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari ‘JK alinda Mawaziri', inayodai kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

Habari hiyo imedai kuwa Mhe. Pinda anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini, imeendelea kudai habari hiyo, "Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita".

Tunachukua nafasi hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo hazeti la Tanzania Daima Jumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.

Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma.

Mhe Rais anawasihi wananchi wasiamini habari hizo za upotoshaji zilizomo kwenye gazeti hilo la Tanzania Daima Jumapili.

Pia ametoa rai kwa wanahabari wasitoke nje ya mstari wa weledi katika kutekeleza kazi zao ili kuendelea kulinda heshima zao binafsi, vyombo wanavyofanyia kazi pamoja na taaluma yenyewe.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Aprili, 2012


 
hivi kuongea mpaka wakutane ?, hakuna simu (sisemi kama habari ni ya kweli ila kutokukutana hakumaanishi kwamba hawajaongea)
 
kwa maana hiyo Rais hawalindi hao mawaziri hivyo kwa kuwa wanatakiwa kujiuzulu basi watajiuzulu. Mimi ndivyo nimeelewa kutokana na kanusho hili. Nasubiri kesho tutajua mbivu na mbichi si tumeambiwa kwamba kesho PM atatoa tamko!
 
Nataka kujua,kama hizi habari ni za uongo kama tulivyoambiwa,waliotoa habari hizi watafanywa nini?Hatua zisipochukuliwa,itatulazimu tuamini hii habari!!
 
Aseme basi tuelewe asije akamtosa kama ilivyokuwa nyongeza ya posho za wabunge na suala la Jairo, tumechoka na kigugumizi.
 
kwa maana hiyo Rais hawalindi hao mawaziri hivyo kwa kuwa wanatakiwa kujiuzulu basi watajiuzulu. Mimi ndivyo nimeelewa kutokana na kanusho hili. Nasubiri kesho tutajua mbivu na mbichi si tumeambiwa kwamba kesho PM atatoa tamko!
kwa hiyo mawaziri wannajilinda wenyewe!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
jana niliwambia rais hayuko dodoma watu wakagoma na kusikiliza habari za kizushi cha ile thread iliyowachanganya wwengi humu....repor imewasilishwa ikulu mda mfupi uliopita
 
ni nani anayetakiwa kupeleka hiyo taarifa kutoka bungeni na kwa nini amechelewa?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
At least hiyo habari imemtoa nyoka pangoni. Bila makala hiyo ya Tanzania Daima tusingesikia chochote kutoka Ikulu.
Huu ni uchokonozi mzuri. Tusubiri kesho.
hayo sio mambo ya kesho.labda taarifa itamfikia kesho halafu ataipitia wiki nzima na baadae kuitolea ufafanuzi(sio maamuzi)

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Katibu Mkuu, Balozi Ombeni Sefua alikuwa bungeni na alifanya mazungumzo na wadau mbalimbali i.e Spika wa bunge, Zitto, Deo Filikunjombe, etc, ina maana Sefue hajampa taarifa Rais? Tena kwa jambo nyeti kama hili? Na Rais anasuburi nini kutoka bungeni? Bunge ndilo liliteuwa baraza la mawaziri? Au rais na wasaidizi wake hawajasoma report ya CAG? Na kama amesoma hiyo report ana maoni gani?

Kurugenzi ya mawasiliano wameiingiza Ikulu kwenye mtego mbaya. Walitakiwa kabla ya kuandika hili kanusho wajirishishe kuwa maamuzi ya rais kuhusu hatma ya mawaziri 8. Sasa. ili hii press ya kurugenzi iwe ya UWONGO basi ni lazima mawaziri wote 8 (nasisitiza) wajiuzulu. Kinyume na hapo ni dhahiri habari ya Tanzania Daima ni kweli!
 
Huyu Rweyemamu amekulia senene na rubisi? Naona alinyimwa balanced diety. Kama Jeykey hawalindi mbona Mponda na Nkya bado wanakula na kufisadi wizara ya afya achilia mbali hawa tuliowapata ktk kamati. Kwa hili JeyKey ukinyamaza umeondoka na wasikudanganye
 
Heri mngekaa kimya na kurugenzi yenu na kila mtu aamini anavyoona yeye sahihi kuliko kukanusha bila kutufafanulia ukweli ni upi? Sidhani kama msingi wa habari ile ni mkutano kati ya JK na Pinda, maudhui ni mawaziri kujiuzuru au lah. Mbona ya Jairo tuliambiwa akitua tu kwa Zuma kimenuka ina maana huo mkutano waliufanya kiuchawi? Mi sikuiamini ile habari lakini hili kanusho lenu la kukurupuka limenifanya niiamini habari ya TZ Daima kuwa ya kweli.
 
  • Kuirugenzi yenyewe ndo inayovujisha taarifa kila mara, ni katika kujinasua tu
 
Back
Top Bottom