Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Sheria ya Vyama vya Siasa(marekebisho ya sheria) ya mwaka 2018 katika kifungu 11(c) kinaruhusu vyama vya siasa kushirikiana kwa malengo ya kisiasa huku kanuni za kuunda ushirikiano huo zikiachwa mikononi mwa waziri husika.
Swali langu ni je,wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu baadae mwaka huu,kanuni ziko tayari?
Kama ziko tayari,zinaruhusu vyama vya siasa kuunda serikali ya mseto au hili ni swala la kikatiba na hivyo n lazima kwanza katiba iruhusu vyama kuunda serikali ya mseto?
Tamanio na pendekezo langu ni kuona jambo hili linafanyika ili Zitto apewe uwaziri wa fedha na uchumi ikitokea upinzani unashika dola ingawa swala la kutokuwa na tume huru linatukatisha sana tamaa.
Ukweli Zitto anaonyesha uwezo mkubwa sana katika swala zima la uchumi na mambo ya kifedha hivyo anastahili hiyo nafasi kwa faida ya Taifa hili.
Ushauri wangu: kama katiba ni kikwazo lakini ikitokea upinzani unafanikiwa,basi Zitto apewa uwaziri wa fedha hata kwa kuwa mbunge wa kuteuliwa na Raisi ikitokea hapati/hagombee ubunge mwaka huu.
Katiba na sheria za nchi hii zinazoshabikiwa na CCM na watu wake ni kikwazo kimoja kikubwa sana kwa nchi yetu kutoka hapo tulipo.
Kifungu 11(c) cha Sheria ya Vyama vya Siasa(Marekebisho) ya mwaka 2018 kinasomeka hivi:
11C.- (1) Vyama vya siasa vinaweza kuunda mtandao kwa kusudi la kufikia malengo ya kisiasa ya pamoja.
(2) Waziri anaweza kutunga kanuni zinazoelezea namna ya kuunda mtandao wa vyama vya siasa.