Kanuni zilizotungwa na Waziri kuhusu namna ya vyama vya siasa kuunda ushirikiano wa kisiasa zinaruhusu vyama kuunda Serikali ya mseto?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,562
2,000
Sheria ya Vyama vya Siasa(marekebisho ya sheria) ya mwaka 2018 katika kifungu 11(c) kinaruhusu vyama vya siasa kushirikiana kwa malengo ya kisiasa huku kanuni za kuunda ushirikiano huo zikiachwa mikononi mwa waziri husika.

Swali langu ni je,wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu baadae mwaka huu,kanuni ziko tayari?

Kama ziko tayari,zinaruhusu vyama vya siasa kuunda serikali ya mseto au hili ni swala la kikatiba na hivyo n lazima kwanza katiba iruhusu vyama kuunda serikali ya mseto?

Tamanio na pendekezo langu ni kuona jambo hili linafanyika ili Zitto apewe uwaziri wa fedha na uchumi ikitokea upinzani unashika dola ingawa swala la kutokuwa na tume huru linatukatisha sana tamaa.

Ukweli Zitto anaonyesha uwezo mkubwa sana katika swala zima la uchumi na mambo ya kifedha hivyo anastahili hiyo nafasi kwa faida ya Taifa hili.

Ushauri wangu: kama katiba ni kikwazo lakini ikitokea upinzani unafanikiwa,basi Zitto apewa uwaziri wa fedha hata kwa kuwa mbunge wa kuteuliwa na Raisi ikitokea hapati/hagombee ubunge mwaka huu.

Katiba na sheria za nchi hii zinazoshabikiwa na CCM na watu wake ni kikwazo kimoja kikubwa sana kwa nchi yetu kutoka hapo tulipo.

Kifungu 11(c) cha Sheria ya Vyama vya Siasa(Marekebisho) ya mwaka 2018 kinasomeka hivi:

11C.- (1) Vyama vya siasa vinaweza kuunda mtandao kwa kusudi la kufikia malengo ya kisiasa ya pamoja.
(2) Waziri anaweza kutunga kanuni zinazoelezea namna ya kuunda mtandao wa vyama vya siasa.
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,906

Tukishamwaga Pombe 2020 tutatengeneza bonge la katiba la Wananchi
 
Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,897
2,000
Kwani kanuni mpaka sasa bado nawakati sheria ilishaanza kufanya kazi!?

Kanuni waziri anaandaa na wadau au wataalamu wa wizara pekee?
Ushirikiano wa 2015 ulikuwa wa kisheria? Lkn athari za 2015 sinaweza pungua ukiwa wa kisheria? Maana lipumba alilamika pamoja na mbatia juzi kuwa ukawa uliwaathiri!

Ebu tusaidiane majibu tuone wanaendaje
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom