Kanuni za sayansi za kusaidia mtu kuishi maisha marefu

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,667
food.jpg

Nyama nyekundu inaelezwa kuwa ni moja ya vyakula vinavyopunguza urefu wa maisha.

Kwa miaka mingi sana binadamu wa karne zote wamekuwa wakitafuta siri za maisha marefu, kuzuia uzee na hata kuzuia kifo.

Lakini pamoja na jitihada nyingi mambo haya yameendelea kuwa changamoto kubwa kwenye maisha ya mwanadamu katika nchi mbalimbali duniani.
Kwa Tanzania, inakadiriwa kuwa umri wa kuishi kwa wanaume ni takriban miaka 58.2 na kwa wanawake ni miaka 60.5.

Muda huu wa kuishi ni mfupi sana ikilinganishwa na wenzetu katika nchi zilizoendelea kama vile Marekani ambako wastani wa kuishi ni unakadiriwa kuwa ni miaka 78.2.

Wanasayansi wamekuwa na nadharia nyingi kuhusu sababu zinazosababisha binadamu azeeke na kufa mapema. Ila wengi hufikiri kuwa tunazeeka mapema kutokana na sababu za maumbile na vinasaba tunavyorithi kwa wazazi wetu.
Wengine husema kuwa tunazeeka haraka kutokana na kuwa na mtindo usiofaa wa maisha.

Mtaalamu wa Afya, Dk Mark Stibich anasema kwamba kuzeeka haraka na kuishi maishi mafupi ni suala mtambuka na linahusisha mambo kama vile vinasaba,kemia, fiziolojiaya mwili pamoja na tabia zetu kwa mujibu wa makala yake ya Mei 10, 2014 liyowekwa kwenye tovuti ya longevity.about.com.

Mtaalamu wa maabara nchini Ujerumani, Dk James Vaupel anadai kuwa vinasaba huchangia kasi ya kuzeeka kwa asilimia tatu pekee na sehemu kubwa ya visababishi vya kuzeeka haraka hutokana na mtindo wa maisha usiofaa pamoja na lishe duni.

Dk Vaupel anaongeza kusema kuwa tafiti nyingi zinaonyesha kuwa hata pacha wanaozaliwa siku moja, hupishana urefu wa maisha kwa karibu miaka 10 kutokana na kuwa na mitindo tofauti ya maisha.

Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wakazi wa maeneo wanaoishi maisha marefu zaidi duniani kama vile Japani, Italia na Marekani, pamoja na mambo mengine, wanajiepusha na matumizi ya vileo, tumbaku na kupunguza ulaji wa nyama nyekundu.
Pia huvuta hewa safi ya kutosha na kupata mapumziko ya kutosha baada ya kazi ngumu kila siku.

Watu hawa pia huwa na mtazamo chanya wa maisha, mazoezi na chakula asilia cha mimea kama vile mbogamboga na matunda kwa wingi.

Vyakula vya asili vineelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa matokeo ya watu kuishi miaka mingi kuliko wale ambao hawazingatii utaratibu huo.

Katika utafiti mmoja uliofanyika huko Japan, iligundulika kuwa chakula chenye asili ya mimea kinaongeza ubora na urefu wa maisha.

Katika utafiti huo, wanawake vikongwe 200 walioshiriki katika utafiti walithibitika kuwa katika kipindi cha juma moja, hutumia zaidi ya aina 100 za vyakula vyenye asili ya mimea.

Jambo lingine likaonekana kwamba wamekuwa wakifanya hivyo kwa kipindi kirefu cha maisha yao. Ripoti hii ni kwa mujibu wa Cook, G.C na Zumla A katika kitabu chao chaManson's Tropical Diseases,toleo la 21.

Katika utafiti wa Dk Pan A na wenzake uliochapishwa katika jarida la kitabibu laArchives of Internal Medicine, la Machi, 2012, inaonekana kuwa kula nyama nyekundu kwa wingi, hupunguza umri wa kuishi.

Nyama yenye shida kubwa ni ile yenye mafuta mengi, nyama choma iliyoungua na ile iliyosindikwa.

Nyama ya namna hii huchangia kutokea kwa magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari na saratani ya utumbo.
Hii inasababishwa na uzalishaji wa kemikali kaman-nitrosanapolycyclic aromatic hydrocarbons (PAHs)zinazodhuru afya.

Ingawa jamii ya Wamasai wanakula nyama nyekundu kwa wingi, tafiti zinaonyesha kuwa wanatumia pia mitishamba (acacia goetzeinaalbizia anthelmintica).

Pia hutumia vyakula vya mimea kwa wingi vikiwa katika uasilia wake, jambo ambalo huwapunguzia hatari itokanayo na nyama.

Hilo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Johns T na wenzake walioufanya Ngorongoro mwaka 1999 na kuchapishwa katika jarida la dawa za asili lijulikanalo kamaJ. Ethnopharmacology.

Katika utafiti mwingine uliofanywa na Dk Dean Ornish na madaktari wenzake wa Chuo Kikuu cha Califonia na San Francisco (UCSF), iligundulika kuwa mazoezi na mtindo bora wa maisha huimarisha afya ya vinasaba vya mwili vinavyohusika na kuzeeka vijulikanavyo kamatelomeres.

Mazoezi yanaelezewa kuwa hufanyatelomeresvirefuke, hivyo kuongeza maisha.Telomereszinapoathirika na kuwa fupi husababisha seli za mwili kudhurika na maisha kuwa mafupi.

Utafiti huu ulichapishwa kwenye jarida laThe Lancet Oncologyla Septemba, 2013.
Jambo jingine linalochangia kuwa na maisha marefu, ni uhusiano mzuri katika familia na jamii, kwa mujibu wa utafiti wa Rikke Lund wa Chuo Kikuu cha Copenhagen Denmark na wenzake katika jarida laEpidemiolojiana afya ya jamii mwaka 2014.

Wataalamu wengine wa masuala ya afya ya jamii wanaongeza kusema kuwa, uhusiano bora na mtazamo chanya katika maisha huongeza urefu wa maisha kwa miaka saba na nusu.

Katika utafiti mwingine uliochapishwa katika jarida la tiba la Uingereza laBritish Medical, watafiti pia waligundua kuwa kutoelewana, ugomvi na mabishano ya mara kwa mara ya wanafamilia au wanandoa, huchangia watu kufa mapema zaidi.
Taarifa hii ilichapishwa katika mtandao wa kisayansi waScience Dailyla Mei 8, mwaka huu.

Kutokana na maelezo ya tafiti hizo, unaweza kubaini kuwa kuishi maisha marefu duniani, kunaweza kutegemea mfumo wa maisha wa mtu pamoja na mazingira yake.

Ukizingatia baadhi ya kanuni hizo za kitaalamu unaweza kuishi muda mrefu duniani.

Clifford Majani ni mmoja wa watafiti, Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Mbeya (NIMR-MMRC)

MCL
 
asante ndugu angu kunipa seminar kuhusu chakula na kunipa muongozo katika maisha yangu juuu ya chakula cha asili na faida yake katika maisha
 
Kwa maisha ya kiswahili, nyama mara 2 kwa mwezi tena finyango 2 kwa mtu utasema huyo mtu anakula red meat kuliko mla burger mmarekani?

Watu wanakufa kwa malaria, kuharisha na mapnemonia au tb.

Ulaji hafifu wa nyama ulionwa na kanisa katoliki mapema ndio maana amri ya kutokula nyama kila ijumaa kwa nchi za dunia ya tatu haikutolewa ikabaki ijumaa kuu tu.

Au unawazungumzia wa masaki na oysterbay?
 
Kwa maisha ya kiswahili, nyama mara 2 kwa mwezi tena finyango 2 kwa mtu utasema huyo mtu anakula red meat kuliko mla burger mmarekani?

Watu wanakufa kwa malaria, kuharisha na mapnemonia au tb.

Ulaji hafifu wa nyama ulionwa na kanisa katoliki mapema ndio maana amri ya kutokula nyama kila ijumaa kwa nchi za dunia ya tatu haikutolewa ikabaki ijumaa kuu tu.

Au unawazungumzia wa masaki na oysterbay?


Mleta mada hajazungumzia tabaka lipi ni kwa faida yetu sote, kwani mkuu hata hao wa Masaki na Obey washapata elimu hii ya bure.
 
Utafiti haujasema kabisa kuhusu michepuko,wakati tunapoteza nguvu kazi kila kukicha kwa vijana kufa kwa Ukimwi!
 
Kwa maisha ya kiswahili, nyama mara 2 kwa mwezi tena finyango 2 kwa mtu utasema huyo mtu anakula red meat kuliko mla burger mmarekani?

Watu wanakufa kwa malaria, kuharisha na mapnemonia au tb.

Ulaji hafifu wa nyama ulionwa na kanisa katoliki mapema ndio maana amri ya kutokula nyama kila ijumaa kwa nchi za dunia ya tatu haikutolewa ikabaki ijumaa kuu tu.

Au unawazungumzia wa masaki na oysterbay?
Observation nzuri maana hata huo umri wa miaka 58 kwa wanaume na miaka 60 kinachotuangusha vifo vinavyotokana na magonjwa mbalimbali kama ulivyoanisha plus vo vya under 5. By the way elimu nzuri kwa kuzingatia maana na sie wabongo kipato kikiongezeka kukaangaza na nyama choma ndio unakuwa mtindo mpya wa maisha na mchicha na majani ya maboga tunasahau
 
Asante sana mleta wazo na hoja zuri kama hili linalohusu maisha yetu wenyewe. Mwenye kusikia asikie mkaidi yeye twamngojea cku ya iddi
 
Mnamo 2006, visiwa vya Okinawa, Japani,
ambavyo vina wakaaji milioni 1.3 vilikadiriwa
kuwa na watu 740 hivi walio na zaidi miaka
100, na asilimia 90 kati yao walikuwa
wanawake. Hilo linaonyesha kwamba kwa kila
watu 100,000, watu 50 hivi wana umri wa
zaidi ya miaka 100, kulingana na Uchunguzi
wa Okinawa wa Watu Walio na Umri wa Zaidi
ya Miaka 100 ulioongozwa na Dakt. Makoto
Suzuki. Katika nchi nyingi zilizoendelea, kwa
kila watu 100,000, watu kati ya 10 na 20
wana umri wa zaidi ya miaka 100.
Uchunguzi huo unaoendelea unaosemekana
kuwa “uchunguzi wa muda mrefu zaidi wa
watu walio na umri wa zaidi ya miaka 100
ulimwenguni,” ulionyesha kwamba “idadi
kubwa sana ya watu walio na umri wa zaidi
ya miaka 100 walikuwa na afya nzuri sana.”
Ili wajue kwa nini watu hao huishi muda mrefu
hivyo, Suzuki na kikundi chake walichunguza
maisha na chembe za urithi za watu zaidi ya
900 walio na zaidi ya umri wa miaka 100
pamoja na wakaaji wengine wa Okinawa walio
na umri wa miaka 70 au zaidi. Wachunguzi
hao waligundua kwamba watu hao wazee
walikuwa wembamba lakini wenye nguvu na
afya, mishipa yao haikuwa na mafuta mengi,
na hawakupatwa sana na kansa na magonjwa
ya moyo. Na wale waliokaribia umri wa miaka
100, ni wachache tu waliokuwa na matatizo ya
kusahau mambo wakilinganishwa na wengine
katika nchi nyingine zilizoendelea. Siri ni nini?
Jambo moja linalochangia ni chembe za
urithi. Lakini kulikuwa na sababu nyingine,
kama vile kutumia kileo kwa kiasi, kupata
lishe bora, na kuepuka kuvuta sigara. Chakula
cha Okinawa hakina kalori nyingi, kina
nyuzinyuzi za asili na mafuta mazuri (ya
samaki), nao wenyeji hula mboga na matunda
mengi. Na watu hao wanakula hadi
wanapohisi wako karibu kushiba. “Unapaswa
kuacha kula unapohisi tu umeshiba,” anasema
Dakt. Bradley Willcox, mchunguzi katika
uchunguzi huo. “Dakika 20 hivi hupita kabla
ya tumbo kuambia ubongo kwamba limejaa.”
Wakaaji wa Okinawa hufanya mazoezi kwa
kulima, kutembea kila siku, kucheza dansi za
kitamaduni, au shughuli nyingine. Mtazamo
wao ulipochunguzwa walionekana kwamba
wana mtazamo mzuri na wako tayari
kubadilika kulingana na hali. Walikabiliana
vizuri na mfadhaiko na hasa wanawake
“walikuwa na uhusiano mzuri na watu
wengine.”
“Hakuna dawa ya kimuujiza” ya kuwasaidia
watu kuishi muda mrefu, anasema Willcox.
Kama uchunguzi huo ulivyoonyesha siri ni
chembe za urithi, kula vizuri, kufanya mazoezi,
kuwa na mazoea mazuri, “na kukabiliana
vizuri na mfadhaiko.”
 
TAFITI mbalimbali zimebaini kuwa, watu
wanaotembea mara kwa mara huishi muda
mrefu, wana uzito unaofaa, hawana shinikizo
la damu na wanaishi maisha ya raha kuliko
wanaotumia magari kwa muda mrefu.
Tafiti 26 zilizofanywa na wanasayansi
mbalimbali zimebaini kuwa unapotembea
huku ukiwa na viatu vifupi hatua 2100 kwa
siku husaidia mwili kuimarika na
kushambualia magonjwa.
FAIDA ZA KUTEMBEA
Huongeza umri wa kuishi. Utafiti uliofanywa
mwaka 2011 umebaini kuwa kutembea zaidi
ya saa moja kwa siku huongeza umri wa
kuishi kwa kiasi kikubwa. Utafiti uliangalia
washiriki 27,738 wa umri kati ya miaka 40 na
79 kwa miaka 13 na kubaini kuwa gharama za
matibabu hazikuongezeka licha ya umri
walioishi.
"Ongezeko la gharama za matibabu
wanaotembea kwa muda fulani wafikiapo uzee
kwani huitaji mahitaji malumu kwa fedha
nyingi za dawa, kutembea humaliza ugonjwa
wa kisukari," utafiti umebaini.
Unapotembea kwa nusu saa katika siku moja
unajikinga na kisukari, utafiti wa mwaka 2002
uliangalia watu wenye uzito mkubwa na
kubaini kuwa wapo katika hatari ya kupata
magonjwa ya shinikizo la damu na kisukari.
Utafiti uliofanywa mwaka 2007, umebaini
kuwa, kama una ugonjwa wa sukari kutembea
ni njia ya kukusaidia kumaliza tatizo hilo.
Unapotembea mara nyingi inakupunguzia
hatari ya kupoteza maisha.
Kutembea maili sita hadi nane kwa wiki
husaidia kuongeza uwezo wa kuweka
kumbukumbu na kupunguza mateso ya uzeeni
ya kupoteza kumbukumbu, hii imebainika na
utafiti uliofanyika kwa watu 299 katika kipindi
cha miaka 9.
Aidha, kutembea maili tano kwa wiki inaweza
kutoa ulinzi katika ubongo usishambuliwe na
ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, wale
ambao tayari wanaosumbuliwa na ugonjwa
huo wanapotembea husaidia kupungua na
kurudi katika hali ya kawaida.
KUTEMBEA HUTIBU SHINIKIZO LA DAMU
Shinikizo la damu linaweza kuisha
unapotembea kwa dakika 30 kwa siku, mara
tano kwa wiki hata usipozimaliza ukatembea
asubuhi mchana na jioni hadi kufikia dakika
hizo unajitibu.
Shinikizo la damu ndicho chanzo kikubwa cha
ulemavu
na vifo vya mapema nchini Uingereza, kupitia
kiharusi,
mshtuko wa moyo na maradhi ya moyo.
Mmoja kati ya watu wazima watatu nchini
Uingereza ana shinikizo la damu, na kila siku,
watu 350 hukumbwa na kiharusi kinachoweza
kuzuiwa unasababishwa na hali hii.
Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema watu
wengi zaidi katika maeneo yote duniani wako
katika hatari ya kupata ugonjwa wa kupooza,
maradhi ya moyo na saratani.
Takwimu zake za mwaka 2012 kutoka nchi
zote wanachama 194, WHO imesema hali
kama za shinikizo la damu na unene wa
kupita kiasi vinaongezeka kutokana na watu
kula vyakula vingi vya mafuta, sukari na
chumvi na kushindwa kufanya mazoezi.
Kila mtu mzima mmoja kati ya watatu duniani
ana ongezeko la shinikizo la damu, hali
ambayo inasababisha karibu nusu ya vifo
vyote vitokanavyo na kiharusi, na maradhi ya
moyo.
Takwimu hizi ni kutokana na ripoti mpya ya
shirika la afya dniani (WHO) ambayo pia
inasema mtu mzima mmoja kati ya kumi
duniani ana ugonjwa wa kisukari.
Hata hivyo nchi za Afrika zilizo kusini mwa
Jangwa la Sahara zaidi ya asilimia 40 hadi 50
ya watu wazima wanakadiriwa kuwa na
shinikizo la damu.
Unapotembea husaidia moyo wako kuisafirisha
damu mwilini kirahisi na kuupa mwili nguvu
na hewa aina ya oxygen ambayo mwili
unahitaji. Damu inaposogea, huwa
inajisukuma kwenye kingo za mishipa ya
damu. Nguvu ya msukumo huu ndio msukumo
wa damu.
Pia kutembea ni tiba ya mifupa,
unapopishanisha miguu katika maili moja
unaimarisha mifupa yako na kukuepusha
kupata matatizo ya miguu na kupooza pia.
Ikiwa msukumo wa damu yako uko juu, basi
unaufanyisha moyo na mishipa yako kazi
nyingi. Kwa muda, hii kazi nyingi huenda
ikafanya viungo vya mwili kuharibika, na
kukuweka katika hatari ya matatizo ya kiafya.
Shinikizo la damu mwilini linaweza pia
kusababisha maradhi ya
moyo na figo pia, na linahusiana na aina
fulani za kichaa.
Unapoendelea kuzeeka, athari za mitindo ya
maisha isiyokuwa ya kuendeleza afya bora
zinaweza kurundikana na kuongeza viwango
vya msukumo wa damu yako.
Unapotembea kwa dakika 30 mara tano kwa
wiki, unaweza kuufanya moyo wako kuwa na
afya nzuri, na kupunguza msukumo wa damu
yako.
Utafiti umebaini kuwa huchukua zaidi ya
miaka saba kwa mtu aliyepooza katika umri
mkubwa kurudi katika hali yake.
Ukitembea kwa takribani maili 12.5 kwa wiki
ama zaidi unapunguza hatari ya kupata
ugonjwa wa kupooza. Utafiti uliofanywa kwa
watu 11,000 waliokuwa na tabia ya kutembea
katika umri wa miaka 58 ulibaini kutokuwa na
magonjwa ya aina hii.
Ikiwa una msongo wa mawazo kutembea ni
njia rahisi ya kumaliza tatizo hilo na
kuondosha hatari ya kupata ugonjwa wa
shinikizo la damu ambalo husababishwa na
msongo wa mawazo.
Tafiti zimebaini kuwa kutembea kwa dakika 20
kwa siku unaongeza miaka 7 ya kuishi kuliko
hata kutumia lishe bora.
Kutembea pia husaidia kumaliza tatizo la
kukosa usingizi, unapotembea kwa dakika 45
kula asubuhi kwa muda wa siku tano tatizo
hilo litamalizika.
"Tatizo la kukosa usingizi huwapata
wanawake wenye umri wa miaka 50-74,
wanashauriwa kutembea ili kuondokana na
tatizo hilo,".
Utafiti uliofanywa kwa zaidi ya wanawake
72,000 wenye umri wa miaka 40-65,
waliokuwa na matatizo ya shinikizo la damu
walishauriwa kutembea na kupunguza vifo
kwa asilimia 30 hadi 40.
Nchini Marekani zaidi ya wanawake wenye
umri wa miaka kati ya 40-65 kutokana na
shinikizo la damu huku wanaume wenye umri
wa miaka 73-93 wakishambuliwa na
magonjwa hayo.
Watu hupoteza maisha katika umri mdogo
siku hizi kutokana na shinikizo la damu na
kiharusi kutokana na kukosa mazoezi ya
mwili.
Nfano unatoka ofisini unaingia katika gari
hadi nyumbani ukifika unakula na kulala ni
wazi unajitakia magonjwa kwani mwili
haujatoka jasho ili kupunguza sumu
uliyoingiza kupitia chakula na hewa uliyovuta
kwa siku.
Kutembea husaidia kupunguza uzito, kuondoa
nyama zembe mwilini, kupunguza mafuta (fat)
, na kukufanya uwe mwepesi wa kufikiri.
Kutembea hakuna ugumu wala gharama,
unaweza kupanga muda wako na ukaweza.
Tuache tamaduni za kwenda na wakati ili
tuishi kama walivyoishi zamani kwakuwa
hakukuwa magari walitembea umali mrefu
kufuata huduma muhimu za jamii.
 
Inaweza ikawa ni mada ngumu kuikubali
kutokana na sababu kadha wa kadha,
lakini ukweli unabaki kuwa wanawake
wamebainika kuwa na uwezo wa kuishi
miaka mingi zaidi ya wanaume, hii ni kwa
mujibu wa tafiti nyingi zilizofanywa hivi
karibuni ulimwengu, ukiwemo ule
ulioendeshwa na wanasayansi wa Chuo
cha Liverpool John Moores (LJMU) nchini
Uingereza.
Profesa David Goldspink wa LJMU
anayejihusisha zaidi na seli za binadamu
alieleza matokeo ya utafiti wa jopo lake
kuwa “tumebaini kwamba nguvu za moyo
wa mwanaume hupungua kwa asilimia 20
– 25 kutoka miaka 18 hadi 70, lakini
nguvu ya mioyo ya wanawake wenye umri
wa miaka 70 haitofautiani na ya vijana
wenye umri wa miaka 20.”
Kwa maana hiyo mwanaume kadili
anavyozidi kupata umri mkubwa, nguvu
za moyo wake hushuka na hivyo
kupunguza kiwango cha msukumo wa
damu mwilini na kusababisha madhara ya
kiafya na hatimaye kifo. Lakini kwa
mujibu wa utafiti huo huo ambao
ulihusisha zaidi ya wanawake na
wanaume wenye afya 250, ulibaini kuwa
mioyo ya wazee wa kike huwa
haipunguwi nguvu kutokana na umri wao.
Ifahamike kuwa ukimchukua mwanamke
mwenye umri wa miaka 20 ukampima
msukumo wa moyo wake ukalinganisha na
mzee wa miaka 80 utapata nguvu sawa.
Kibaiolojia ni kwamba wanawake
wameumbwa tofauti na wanaume, ndiyo
maana wanatajwa kuishi miaka 5-13 zaidi
ya wanaume na kwamba kiwango hiki
kimekuwa kikiongezaeka kutoka karne
moja hadi nyingine.
Mazingira ambayo yanashibisha hoja hii
ni pamoja na mfumo mzima wa masuala
ya kujamiina ambayo huwahusisha watu
wa jinsia mbili tofauti. Hata ukiangalia
utofauti ulioanishwa mara nyingi na
watafiti umewashirikisha zaidi wanawake
wenye umri kati ya miaka 18 na
kuendeleza, umri ambao kwa kawaida
wasichana wengi huwa tayari wamevunja
ungo na wengine kuanza kushiriki tendo
la ndoa.
Randolph Nesse, mwanasaikolojia wa
Marekani aliwahi kueleza faida anazopata
mwanamke wakati wa tendo la ndoa na
kipindi cha siku zake ambazo zinatajwa
pia kumsaidia katika kusafisha kemikali
za mwili wake na kwamba upo ushihidi
kuwa mwanamke asipoingia kwenye siku
zake afya yake huyumba.
Maelezo haya na mengine yahusuyo
mwanamume kutoa mbegu wakati wa
tendo la ndoa yanaweza kuwa sababu ya
kuweza kutofautisha umri wa kuishi kati
ya mwanaume na mwanamke na kuzidi
kuweka hatari kubwa ya umri wa
wanaume kuendelea kupungua kama
elimu ya kujihami na tatizo hili
haitatolewa kwa wahusika.
Kumekuwa na hoja nyingi kuhusu tatizo la
wanaume kupungukiwa na umri wa
kuishi, wapo wanaosema kuwa wingi wa
majukumu ya kifamilia huwapunguzia
umri wanaume, hata hivyo njia pekee
zinazotajwa kuwasidia mwanaume kuweza
kuimarisha mapigo ya moyo wake ni hizi
zifuatazo:
KWANZA- Ili mwanaume aweze kuusaidia
moyo wake kuwa na nguvu katika kipindi
chake cha maisha ni lazima afanye
mazoezi ya mwili. Wanaume wengi
wamekuwa wakipuuza ufanyaji wa
mazoezi, jambo ambalo ni hatari kwa afya
zao. Ufanyaji wa mazoezi unaweza
kuusadia mwili wa mwanaume kuongeza
msukumo wa damu na kumuwezesha
kutoa kemikali hatari mwilini kwa njia ya
jasho ambalo haliwezi kutoka kama mtu
atakuwa amekaa na kuendekeza starehe.
PILI- Mwanaume anashauri kupunguza
kiwango cha kufanyaji mapenzi.
Upunguzaji huu utasaidia kuufanya mwili
wake uwe na seli za kutosha kulingana na
lishe anayopata, hata hivyo kama
mwanaume anataka kufanya mapenzi kwa
kiwango cha mara tatu au nne kwa siku
lazima azingatie mlo wenye nguvu. Lakini
kwa wanaume ambao ni dhaifu,
wakiwemo wenye virusi vya UKIMWI
hawashauriwi kufanya ngono mara kwa
mara.
TATU- Kucha kutunza hasira kifuani.
Wanawake wengi hufanikiwa kupumzisha
miili yao kwa sababu ni wepesi wa
kukasika na kumaliza mambo tofauti na
wanaume ambao hutajwa kutumia muda
mwingi kufuga chuki moyoni. Inashauriwa
kuwa kama kuna jambo ambalo limetokea
ni vema kulimaliza na kuachana nalo, ili
kuufanya mwili uwe huru. Kitendo cha
kuweka hasira mwilini huchangia moyo
kupungukiwa na nguvu za kufanya kazi
sawa sawa.
NNE – Kuzingatia lishe bora, kupata muda
wa kupumzisha mwili, kuepuka matumizi
ya kemikali kama pombe kali na vinywaji
vyenye nikotini pamoja na kupata vipimo
vya kitabibu hasa vya moyo kila baada ya
miezi mitatu ili kufahamu mapema
matatizo ya moyo wake na kuweza
kuyatibu mapema.
Pamoja na ukweli kwamba wanawake
wanaishi umri mkubwa zaidi ya wanaume,
Daktari Carol . J . Hogue wa Marekani
anawashauri wanawake wote kuzingatia
afya ya uzazi salama, anaseme miongoni
mwa mambo ambayo yanawapunguzia
umri wa kuishi wanawake ni pamoja na
suala la uzazi. Anasema ili mwanamke
aweze kuishi zaidi ya mwanaume ni vema
akapanga uzazi. Inaelezwa kuwa kipindi
cha mwanamke kujifungua ndicho
kinachotajwa kuhatarisha maisha ya
wanawake wengi.
Makala haya yanazingatia ukweli wa vifo
vitokanavyo na hitilafu za udhaifu wa
mwili si ajali na majanga mengine
kwamba wenye hatari ya kufariki dunia
ni wanaume peke yao.
 
Kama una wazazi, babu na bibi, wajomba,
mashangazi, na ndugu wengine wa karibu
ambao waliishi hadi miaka 100 au zaidi basi
kuna uwezekano mkubwa kwamba familia au
ukoo wenu umeshinda bahati nasibu ya
kimaumbile ya kuishi maisha marefu.
Pamoja na hayo, wanasayansi wanaonya
kwamba hata kwa watu ambao wamejaliwa
kurithi chembechembe hizi nzuri za urithi,
bado wanahitajiwa kuishi maisha yenye
kuzingatia afya njema mf. kufanya mazoezi
mara kwa mara, kutokunywa pombe
kupindukia, kutovuta sigara na kutonenepa
kupindukia
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom