Kanuni za Mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa zilenge kusahihisha tulikopita

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Nimesikia Rais ameagiza Waziri kuandaa kanuni za mikutano ya vyama vya siasa na hapa ndipo tunatakiwa kurejea katika historia yetu na kujiuliza tumekuwa na changamoto gani mpaka hapa tulipo na kanuni hizi zilenge kutoa majibu.

Tukirudi katika historia tunaambiwa miaka ya 60 na 70 tulikuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa na ilipofika mwaka 1977 tulifuta mfumo huo na kubaki na chama kimoja cha siasa. Je sababu zilikuwa ni zipi?

Miaka ya 90 tukarejea katika mfumo wa vyama vingi na hapa tulipo leo tunatakiwa kujiuliza, je yale tuliyoyakimbia miaka ya 70 yanajirudia leo au ndiyo tulijifunza?

Kwa kifupi ni kwamba mwalimu Nyerere alifuta vyama vingi kutokana na siasa zilizokuwa zikifanyika katika mfumo wa vyama vingi huo kutokuchochea maendeleo ya watu na badala yake siasa zilijikita katika kuchongeana, kupakana matope, kutengenezeana fitina miongoni mwa wanasiasa ilimradi wananchi wamchukie huyu na kumpenda yule.

Ingawaje miaka hiyo sikuwepo kuyashuhdia wanasiasa waliyokuwa wakiyafanya kwenye majukwaa na vyombo vya habari lakini nimeshuhudia mengi katika mfumo wa vyama vingi vya siasa wa miaka ya 90 ambayo yanashadadia yale niliyoyasikia.

Sisemi mfumo wa chama kimoja unatufaa bali hoja yangu ni tutunge kanuni zitakazoondoa fitina, uongo, chuki na mengine ya jinsia hii miongoni mwa wanasiasa.

Pengine tuombe serikali iunde chombo huru cha kudhibiti nidhamu za wanasiasa kinachosimamiwa na vyama vyote vya siasa kwa pamoja na mtu akikiuka anapewa adhabu kulingana na kanuni zinavyosema.

Tusitake kuwaaminisha watu kuwa siasa ni uongo, kwamba huwezi kumzuia mwanasiasa kutengeneza fitina bali tuweke mikakati ya kuwaelekeza wanasiasa katika kujenga hoja za ukweli

Labda nitoe mfano, kuna siku nilikuwa nasikiliza Mchungaji Msigwa na Humphrey Polepole wakihojiwa katika kipindi cha TV kikiwa live. Baada ya mjadala kushika kasi nilimsikia mmoja wao akimuambia mwingine kuwa "wewe katika ofisi uliyokuwa ukifanya kazi ulimbaka mfanyakazi"

Sijui ilikuwa ni kweli? sijui huyu alitunga hoja baada ya kuona mwenzake kambana kwenye hoja kaamua kuleta jambo la kumfedhehesha mwenzake. Hizi siyo siasa. Yawezekana ni kweli na kwa mwanasiasa kutenda haya ilitakiwa aadhibiwe kwa maadili ya wanasiasa na yawezekana alisingiziwa na hivyo mtu kumsingizia mwingine hivyo naye alitakiwa kuadhibiwa na kanuni za maadili ya wanasiasa.

Kanuni zilenge kuboresha siasa na siyo kumruhusu mtu yeyote kufanya chochote kupitia mgongo wa siasa
 
Back
Top Bottom