trem
JF-Expert Member
- Sep 19, 2014
- 340
- 200
Kwa kawaida watu wanatumia msemo usemao kuwa ''kulea mimba si kazi, kazi ni kulea mtoto". Huu msemo unaweza kuibua hisia zetu, lakini pia ni msemo wa mtu ambaye, ama anaujua ugumu wa kumlea mtoto au ni mtu aliyekata tamaa kwa sababu amekuwa katika mlolongo wa kujaribu kumlea mtoto vizuri na akashindwa,
unaweza pia kuwa ni msemo wenye msingi wa mtu ambaye huenda hakutegemea kabisa kukutana na ugumu huo na changamoto nyingi kiasi hicho katika malezi ya mtoto. Biblia inasema."mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee." (mithali 22:6)
Zifuatazo ni kanuni za kumlea mtoto;
1. Kulea kunahitaji juhudi yenye kuendelea bila kukoma uzuri au wema wa mtoto hauwezi kuja hivi hivi tu bila juhudi ya malezi ya wazazi wote (mithali 22:15).
2. Kulea kunahitaji mafundisho ya umakini mtoto siyo kama mnyama, mnyama hujua mambo kwa sababu ya silika yake lakini mtoto hujua mambo kwa njia ya mafundisho sahihi (kumbukumbu 6:6-7).
3. Kulea kunahitaji kuweka nidhamu na heshima (mithali 13:24) nidhamu ina kazi ya kumrudisha kwenye njia.
4. Ili kuweka nidhamu, hakikisha mambo haya unayafanya;
a. Weka mipaka iliyo wazi na mtoto ajue mipaka hiyo.
b. Epuka kuweka sheria zinazofuatana na adhabu za hapo hapo.
c. Usiweke sheria nyingi kwa mtoto, weka chache tu na ziwe wazi.
d. Usibadilibadili sheria zako kila mara zitamchanganya mtoto.
e. Kila sheria iwe na maana na ieleze faida na hasara zake.
f. Usiweke sheria au utaratibu ambao hata wewe mwenyewe huwezi kuutimiza.
g. Adhabu ziendane na uzito wa kosa la mtoto.
h. Usitoe adhabu na zawadi kwa wakati mmoja na kwa tukio moja.
i. Wazazi msipingane katika kutoa adhabu kwa mtoto.
Nawasilisha.
Karibu kwa majadiliano zaidi