Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Spika au wabunge kuhujumu haki za raia bungeni kunatokana na kutojitambua kisheria kwa raia watanzania. Ibara ya 21(1-2) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ibara ya 34(1-5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge zimewapa mamlaka kisheria raia wa Tanzania kuamuru maamuzi ya spika na ya ...bunge lote kwa ujumla
Ibara ya 34(1-5) ya Kanuni za kudumu za bunge ndiyo imewapa mamlaka raia kuwasilisha maombi yao bungeni kupitia wabunge bila ya kuwa na vipigamizi vya spika na vya wabunge iwapo maombi hayo yamesainiwa na raia wa kila kata za jimbo na majimbo yote ya Tanzania ambayo wabunge watalazimka kuwasilisha maombi hayo bungeni yaliyopokelewa kwao kwa kufuata taratibu za kisheria ambazo haziwezi kukanwa kamwe mahakamani.
Kwa kufuata kanuni za kudumu za bunge uwasilishaji wa maombi bungeni ni tofauti na uwasilishaji wa hoja, hati ya dharura na mswada ambazo yote kwa pamoja yana vikwazo vya spika na wabunge kama zisemavyo ibara ya 53-54 za kanuni za kudumu za bunge.
Ni maombi ya raia peke yake yasiyo na vikwazo vya spika na vya wabunge kuamua watakavyo na pia maombi hayo yanaruhusiwa kuwasilishwa bungeni bila ya kujali maombi hayo yaliyowasilishwa bungeni yamefanana na maombi mengine yaliyowasilishwa bungeni kutoka kwenye majimbo mengine na hivyo kutokujali idadi ya maombi yaliyowasilishwa ambayo yanafanana kuwezesha kulazimika kujadiliwa na kuamuliwa kwa pamoja na bunge.
Kwa hiyo ni ujinga wa sisi raia wa Tanzania kuwalalamikia wabunge wakati hatujawasilisha bungeni kisheria maombi yetu yaweze kupitishwa bungeni bila vikwazo vya spika wala wabunge kwa mujibu wa sheria za katiba na kanuni za kudumu za bunge.
Sasa ni wakati wa raia kutoka kwenye kata za majimbo yote ya Tanzania kuwasilisha maombi bungeni kama yafuatayo.
1.Maombi ya kuunda Kamati ya kuchunguza utekaji wa raia na urejeshaji wa raia waliotekwa.
2. Maombi ya kurejeshaji bunge la katiba ili liweze kuunda katiba mpya huru ya haki, tume huru ya haki ya uchaguzi, ofisi huru ya haki ya msajili wa vyama vya siasa na taasisi huru ya haki ya mahakama.
Raia wanapaswa kuwashirikisha viongozi wa vyama vya kisiasa namna ya kujipanga kwa pamoja katika uwasilishaji ya maombi yao bungeni kwa kipindi kimoja nchi mzima.
Raia tusitegemee hoja, hati za dharura na miswada inayowasilishwa bungeni na wabunge ambazo zote zina vikwazo vingi vya spika na wabunge na kwa hiyo haviwezi kutuletea haki raia wa Tanzania. Raia tutekeleza wajibu wetu wa kuwasilisha maombi yetu bungeni ambao ni mkataba wetu wa kisheria kikatiba wa kushiriki shughuli za utawala ambao tuliousaini kwa kuwapigia kura wawakilishi wetu ambao ni rais, wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa. Tafakali chukua hatua!!!!!!