Kanuni za Bunge tukufu: kanyaga twende hata kama watu wanaendelea kufa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanuni za Bunge tukufu: kanyaga twende hata kama watu wanaendelea kufa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Feb 3, 2012.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jana nimeshudia jambo ambalo sikuliona kama liko sawa hata kama ni sawa sawa kulingana na kanuni tukufu za bunge tukufu.

  Wabunge Mh Ndululile na Mh Mnyika walitoa hoja ya kusitisha shughuli zote za bunge ili kujadili suala la mgomo wa madaktari.

  Mh naibu spika Ndugai akasema ni kweli hoja zimetolewa vizuri lakini kwa vile hazikuungwa mkono – Kanyaga twende….

  Hii ni bila hata kujali kuwa watanzania wanaendelea kupoteza uhai wakati bunge likiendelea kujadili mijdala ya kawaida ambayo hakuna tutakachopoteza tukiyaahirisha na kuokoa maisha ya Mtanzania.

  Nawasilisha
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kimsingi nashangaa sana utaratibu huu,na kweli unapohisi utaratibu unaweza kuwa ni hatari kwa Taifa huko mbeleni ni sharti zifanyiwe marekebisho haraka sana...kwa hili hii kuna siku nchi inaweza kuwa imevamiwa na mbunge anatoa hoja tupeleke jeshi,kwasababu hoja haikuungwa mkono kwa kusimama kwa wabunge tukaamua kukaa kusubiri utaratibu...Hii ni hatari kwa muono wangu.
   
 3. h

  hayaka JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hatuna wabunge wanaowakilisha wananchi bali tuna wabunge wawakilishi wa tumbo zao!
   
 4. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mfano uliotoa hauna uhalisia. Binafsi naliona Bunge linaendeshwa kisiasa. Kwa kweli, kanuni zinasema haugombei ubunge mpaka uwe mwanachama wa chama cha siasa kilichosajiliwa. Kwavyovyote lazima mbunge ataangalia maslahi ya chama chake kwanza kwa kuwa ndicho kilichomnadi, kisha ndio Wananchi. Nadhani utaratibu huu hautufai. Turuhusu taasisi zingine na watu binafsi kugombea ubunge.
   
 5. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapo penye red tuko pamoja
   
 6. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Wagonjwa mahospitalini si hoja ya mingi kwa wabunge wa Tanzania. La muhimu: posho,...posho...daima posho.
   
 7. Bi. Kiroboto

  Bi. Kiroboto Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nahisi nina mtazamo tofauti ndugu zangu.
  Kwanza, siungi mkono kwa jinsi serikali ilivyochelewa kutoa tamko lake bungeni.
  Pili siungi mkono jinsi waziri wa afya alivyolidanganya bunge na umma kwa ujumla, hapa nina maana kwamba waziri ameridhika kuondoa baadhi ya madai ya msingi ya madaktari. Kwa mfano, katika taarifa yake, waziri ama kwa makusudi au kwa sababu anazozijua yeye, hakusema kama madaktari wanahitaki uboreshwaji wa huduma ya afya kwa ujumla. Lakini pia hajatuambia kuwa hata yeye analalamikiwa.

  Ila kwa upande mwingine, kulikuwa na kila sababu kwa wabunge kupata kwanza taarifa rasmi ya serikali juu ya jambo hili kabla ya kulijadili. Sio rahisi kujadili jambo ambalo hujapata taarifa rasmi, hasa jambo lenyewe linapokuwa nyeti kama hili. Wabunge walitakiwa wawe na facts(ingawa sina hakika kama kwa taarifa ya leo wamepata facts) kwa ajili ya kujiweka ktk nafasi nzuri ya kujadili.

  Lakini pia mimi namuunga mkono Ndugai kwa uamuzi wake siku ya leo. Nadhani, tukubaliane kwamba ili mjadala uende vema ni lazima kuwe na balance ktk information. Sio rahisi kufanyia kazi ushahidi wa upande upande mmoja. Tutakubaliana kwamba kwa yeyote aliyeona/sikia taarifa ya serikali ameweza kuona kwamba taarifa ile iliegemea zaidi upande mmoja-serikali; kwamba serikali imetumia oppotunities zoke zilizokuwepo kutatua tatizo hili, na ikashindikana. Lakini, je, ni kweli kwamba serikali haina namna nyingine ya kusolve tatizo hili?

  Wabunge wanahitajika kupata taarifa kutoka upande wa pili, na ikiwezekana hata upande watatu ambao unajumuisha wadau mbalimbali, ikiwemo wagonjwa na hata wabunge wenyewe individually. So, ili tuweze kuwahukumu wabunge, tunasubiri kusikia jinsi watakavyojadili jambo hili hapo watakapokuwa wamepata kusikia kauli za upande wapili.

  Pamoja na hili, tunategemea Ndugai awe amefanya uamuzi huu kwa utashi wake. Maana kuna uwezekano wa kuwa ameelekezwa kuahirisha mjadala, kwa kuwa leo madaktari wanakutana tena na serikali kujadili jambo hili. Na kama hili liko hivyo, wabunge na umma wote tutakuwa tumepigwa changa la macho.

  Lakini pia sitarajii kuona kamati iliyopewa jukumu hili ikirudisha majibu ktk mkutano wa 7, hiyo haitakuwa dharura tena.
   
Loading...