Kanuni ya Wageni Watatu Timu za Ligi Kuu: Lengo Lake Linaendana na Uhalisia wa Mambo?

mwangalingimungu

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Messages
1,282
Points
1,500

mwangalingimungu

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2013
1,282 1,500
Kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu, TFF imeweka kanuni ya kila timu shiriki kuwa na ukomo wa wachezaji watatu tu wa kigeni. Lengo ni kuwapa nafasi zaidi wachezaji wazalendo na kuwasaidia kuinua viwango vyao. Ni lengo zuri, lenye nia njema.

Lakini tukitizama hali ilivyo kwenye Ligi yetu kwa kutumia kioo cha ligi za wenzetu, hii kanuni itasaidia kweli kufikia lengo hilo? Kwa miaka kadhaa mfululizo, wachezaji wengi wa kigeni wamekuwa ndio roho za klabu zao hapa nchini. Sizungumzii Okwi wala Ochan wa Simba au akina Mwalala na Ambani wa Yanga. Wako wengi tu, ingawa kuna wakati ilidhaniwa kwamba mchezaji wa kulipwa hapaswi kuwa wa nafasi za akiba. Hili kwa namna fulani lilikuwa ni zengwe la kuwabeza na kuwakebehi wachezaji aina hizo na timu zao, lakini hadi leo, kwenye ligi za mataifa yaliyoendela kuna wachezaji wengi wa akiba kwenye safu za akiba. Mifano ya karibu ni Chicharito, Khedira na wengineo kadhaa. Kukawa na hukumu ya jumla ya wachezaji wa kigeni kwamba hawastahiki kwa sababu tu viwango vyao havitofautiani sana, kama sio duni zaidi ya vile vya wachezaji wazalendo, ingawa kwa maoni yangu tatizo hapo sio kanuni yenyewe bali umakini wa utafutaji wachezaji hao.

Hatimaye ndio imekuja kanuni hii ya wachezaji watatu. Sina hakika kama kumetumika vigezo sahihi. Maana hata ligi zilizoendelea zinatoa nafasi zaidi ya hizo. Mbali na hizo, kuna hadi kanuni za kuwapa uraia/ukaazi wachezaji wa kigeni waliokwishachezea ligi hizo muda mrefu ili wahesabike sawa na wazalendo, makusudi ili kutoa nafasi za ziada kwa wachezaji wengine zaidi wa kigeni. Tumekuwa tukizinanga sana timu zetu mbele ya TP Mazembe kwamba imefanikiwa haraka. Lakini ukitizama mafanikio ya timu hiyo, huenda ukashawishika kubaini kwamba yamechangiwa sana na wachezaji wa kigeni kwenye timu hiyo, ambao ni zaidi ya watatu kila wakati.

Tujiulize pia iwapo uchache wa wachezaji wetu kwenye ligi za nchi jirani na kwengineko unachangiwa na kanuni ya sasa ya wachezaji watano. Tujiulize iwapo kwa kanuni ya idadii ya wachezaji pekee tutawezaje kuwa na wachezaji wa kulipwa nje ya mipaka yetu kwenye ligi zenye ushindani wa kweli bila ya mawakala mahiri na weledi walio wazalendo, bila ya wanahabari wanotumia nguvu ya kalamu na taaluma zao kuwanadi na kuwakuza wachezaji wetu nje ya mipaka yetu badala ya kuwananga na kuwafuja kwa sababu tu hapa nchini hawkujiunga na timu chaguo za wanahabari hao.

Tujiulize pia iwapo wingi wa wchezaji hodari kama akina Kipre Chetche, Amisi Tambwe, Hamis Kiiza, Hauna Niyonzima na wengineo kunawalemaza au kuwakomaza wachezaji wazalendo, sambamba na iwapo makocha wa kigeni waliopo wamesaidia kuwakomaza au kuwalemaza makocha wazalendo. Baadaye tujiuize iwapo kanuni ya ukomo wa wachezaji wa kigeni kwenye Ligi Kuu haipaswi kwenda sambamba na kanuni kama hiyo kwa idadi ya makocha wa kigeni kwenye Ligi hiyo; yaani kuwepo pia na ukomo kwa idadi ya makocha wa kigeni ndani ya Ligi Kuu. Maana nionvyo, makocha wana nafasi zaidi katika kukuza viwango vya uchezaji na wachezaji kuliko hata wachezaji wenyewe.

Swala la msingi ni je, ukomo wa wachezaji watatu kwa timu za ligi kuu utaimarisha kweli viwango vya wachezaji wazalendo, au ni dhana tu?
 
BBA

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2012
Messages
319
Points
0

BBA

JF-Expert Member
Joined May 27, 2012
319 0

Tatizo letu watanzania ni kutofanyia research mambo kabla ya kufanyia maamuzi. Wachezaji wa njeni role models kwa wachezaji wetu kwakuwa wengi wao ( wachezaji wetu) hawajitambui licha ya kuwa na vipaji.
Licha ya ukweli kuwa wachezaji wa nje wakati mwimgine huwa hawana uwezo wa chini Jama Mba na Mbiyavanga lakini hilo huwa sio huwa sio lengo la vilabu.
Asilimia kubwa ya wachezaji wetu wanaridhika wakicheza Yanga au SIMBA hii ni kwa sababu ya uelewa mdogo sana walionao wengi.
Kwa ujumla siiungi mkono
 
Forum statistics

Threads 1,392,167
Members 528,552
Posts 34,100,463
Top