Kanuni mpya za fedha: Dr Mpango

KANUNI mpya za kudhibiti utakatishaji fedha, zinatarajiwa kubana zaidi wanaofanya miamala kwa njia za kielektroniki ikiwamo benki na simu za mkononi.

Kwa mujibu wa kanuni hizo zilizosainiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Mei 7, mwaka huu na kuchapishwa kwa umma Mei 24, zinataka taarifa za mtu anayefanya muamala wa fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 10,000 (zaidi ya Sh mil. 20) au zaidi, kutoa taarifa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU).

Kanuni hizo pia zinabana wanaochezesha michezo ya kubahatisha kwa njia mbalimbali ambao nao wanatakiwa kutoa taarifa zao FIU.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, kiasi hicho kinachotakiwa kutolewa taarifa ni kile kilichofika thamani hiyo ya fedha kwa muamala uliofanyika kwa wakati mmoja.

Katika kanuni hizo, uhamishaji fedha umetafsiriwa kuwa unajumuisha “shughuli yoyote ya fedha inayohusisha amana, utoaji, kubadilisha, malipo au kupokea fedha kwa shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni.”

Kanuni ya tano inasema, “mtu anayepaswa kutoa taarifa, atapaswa kutoa taarifa zifuatazo katika Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) (a) ubadilishaji wa fedha zinazohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni ambayo thamani yake ni sawa na dola 10,000 za Marekani au zaidi kwa mara moja.

“(b) Kuhamisha fedha kwa mtandao, unaohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni sawa na Dola 1,000 za Marekani au zaidi kwa mkupuo.

“(4) Katika kutambua thamani ya fedha za kigeni sawa na Dola za Marekani 10,000 kwa madhumuni ya taarifa ya fedha au dola 1,000 kwa lengo la kutoa taarifa za uhamisho wa fedha za kwa njia ya kielektroniki, muhusika anatakiwa kutumia viwango vilivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania vinavyotumika kwa wakati huo.”

Akizungumzia kanuni hizo, Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, alisema; “kanuni zinasema mtu yeyote anayefanya muhamala wa fedha kwa njia ya mtandao ama anayesafirisha fedha kwa njia ya mtandao, atoe taarifa kwamba ‘nataka kusafirisha kiasi fulani kwa sababu fulani’.

“Kama unatuma fedha Japan kwa ajili ya kununua gari ama umepokea fedha kutoka nje, au unataka kumtumia mtu fedha zinazofika kiasi kilichotajwa kwenye kanuni, lazima utoe taarifa, hii ni kwa benki ama simu kwa sababu zote hizo ni njia za kielektroniki.

“Utaona dhumuni hapa ni kupambana na fedha haramu ama ndiyo maana ukienda kwenye mambo ya ‘cash’ kuna sheria inabana ipo kwenye viwanja vya ndege na mipaka, kwamba mtu anaweza kusafirisha kiasi gani cha fedha na azitolee taarifa.

“Kwa hiyo inahusu watu wote kama ni nje ama ndani ndiyo maana inasema ndani au nje ya nchi,” alisema.

Alisema kanuni hizo zinabana hata wale wanaochezesha michezo ya kubahatisha ambao kama wanataka kutoa fedha kama zawadi ambazo zinafika kiwango kilichotajwa na kanuni wanatakiwa kutoa taarifa hizo.

“Kwa hiyo hizi kanuni zinakubana kama unataka kutumia njia za kielektroniki kutuma fedha ama kuchukua fedha huko,” alisema.

Kanuni ya 11 inasema miamala miwili au zaidi ikifanywa ndani ya saa 24 na kufikia dola 10,000 za Marekani au zaidi, itachukuliwa kuwa ni muamala mmoja na hivyo itatakiwa kutolewa taarifa.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, ripoti za uhamisho wa fedha kielektroniki au ripoti zote za fedha zitapelekwa FIU kabla ya kumalizika kwa siku tano za kazi baada ya siku ya uhamishaji.

“Zitapelekwa kwa njia ya kielektroniki au vinginevyo inavyohitajika na FIU, kila operesheni ya shughuli za michezo ya kubahatisha atahitajika kutoa ripoti ya fedha kwa fedha zilizopatikana kutoka kwa mteja,” inasema sehemu ya kanuni hizo.

Kanuni hizo pia zimeweka adhabu mbalimbali kwa watakaoshindwa kufuata matakwa yake ikiwa ni pamoja na faini na kifungo.

Zinasema FIU au mdhibiti akiridhika kwamba mtoa ripoti ameshindwa kutoa ripoti ya fedha au uhamisho wa fedha zilizohamishwa kielektroniki au kimataifa, kitengo hicho kinaweza kutoa onyo au tahadhari ya kurudia mwenendo uliosababisha kutotii.

Mtu atakayefanya kosa hilo pia anaweza kusimamishwa kufanya shughuli yake ama biashara, kutozwa faini isiyozidi Sh milioni tano na isiyopungua Sh milioni moja kwa siku ambayo kasoro ilijitokeza.

Adhabu nyingine ni kusimamisha leseni ya biashara au kusimamishwa au kuondolewa kutoka ofisi ya mfanyakazi ambaye alisababisha kasoro hiyo.
R.I.P MWALIMU NYERERE
 
Hawakurupuki, wao wanaogopa pesa ya mabeberu isiingie nchini kinyamela. Nchi zinazopata misuko suko huwa kuna donor somewhere anaingiza nguvu ya pesa, wao hapo wamebana. Vyama vya siasa wamepewa mashart magumu kuliko yenu, wao kiasi chochote wanachopewa wanahitaji kuriport serikalini, na balozi zote zimepewa masharti ya jinsi na namna ya kusaidia vyama vya siasa na NGOs, lengo lao ni kuhakikisha hakuna anayepata pesa nje serikali isifahamu, huo ndio udhibiti walioweka. Ubalozi au shirika lolote la nje likitaka kukisaidia chama cha siasa kwanza serikali inapewa taarifa za kiasi na malengo ya msaada, na ndio maana uliona ulifanyika uhakiki wa NGOs zote na kuweka masharti ya kutoa taarifa za mipango kazi yao mara kwa mara serikalini.
Walengwa siyo nyie wananchi wakawaida, nyie mmekumbwa na mtego wa panya. Kulinda madaraka siyo kazi rahisi, lazima yatengenezwe mazingira magumu kwa kila mtu ili ionekane ni kawaida, na siku wakibinywa waseme hii siyo kwao tu bali ni nchi nzima.
Hivyo msimlaumu Dr. Mpango, yeye ni mtekelezaji wa mipango iliyo kwisha ratibiwa serikalini. hata akifahamu hasara ya sera Fulani leo, hawezi kubadirisha kama imeamriwa hivyo. Nyie mnadhani Bashe anaakili sana kuliko Dr.mpango, ni kwasababu mpango hutekeleza mipoango iliyopo hatengenezi sera yeye.
Beberu aingize $1000 kwa MPESA? Acheni ushamba bhana.
 
Kwa hyo watumishi wanaolipwa mishahara kuanzia mil 5 pale mishahara yao inaipoingizwa kwenye a/cc zao.
Je kitengo cha kulipa mishahara kitatakiwa kutoa taarifa FIU
 
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati
JF bwana inakizazi ambacho kinaumaskini mkubwa wa kuchakata taarifa wanazopokea, jilizisheni kwanza taarifa husika na ukimbilie jukwaa kutoa maoni.
jambo jingine jifunzeni kidogo huko ulaya wanafanyaje kuhusu mambo hayo ya transaction? kwa dunia ya leo hupiti na hela zaidi ya dola elfu kumi air port mpaka uitolee taarifa, haya mambo hayajaanza kwetu bongo,yapo kitambo kwa wenzetu sema sie ndo tunaanza labda
 
Hii kubana bana hii itazidi kutupoteza hongera muheshimiwa Peter Serukamba ndiyo haya uliogusia... kuna video nimeiona Ayo tv umeongea mambo ya msingi sana.. Big Up
 
JF bwana inakizazi ambacho kinaumaskini mkubwa wa kuchakata taarifa wanazopokea, jilizisheni kwanza taarifa husika na ukimbilie jukwaa kutoa maoni.
jambo jingine jifunzeni kidogo huko ulaya wanafanyaje kuhusu mambo hayo ya transaction? kwa dunia ya leo hupiti na hela zaidi ya dola elfu kumi air port mpaka uitolee taarifa, haya mambo hayajaanza kwetu bongo,yapo kitambo kwa wenzetu sema sie ndo tunaanza labda
Uongo mfano ulaya na Marekani wao ni wakali mno kama unatoka na pesa kwenye nchi zao lakini kama unaingiza wala hawakuhoji wala kukusumbua.Ndio maana mapesa kibao huingizwa mabenki ya uswisi na offshore banks.Wao wanataka ziingie ndio maana hata ukisafiri nchi zao kuomba Visa unatakiwa kupeleka benki statement wajue utawaingizia pesa.Hicho ulichonacho kwenye benki statement hawahangaiki kuhoji.Beba dola zako au pound zozote nenda nazo ulaya au Marekani uone kule kama kuna atakayekuuliza.Lakini Beba hizo pesa uje nazo nchi zetu za Dunia ya tatu utakoma.Hii vita ni kitu cha vi nchi maskini ndio vinavalia njuga.Nigeria hiyo Sheria ya money laundering walikataa wakasema ni uonezi kwanza dola elfu kumi ni hela ndogo pili mbona kwao viongozi wa Nigeria wanaingiza mabilioni nchini kwao mbona hawafuatilii wala kupiga makelele.Kwenye hii vita tutaumizana bure.Mtu kama anaingiza pesa nchini kwako au benki yako usiwe mkali mno Kila kitu Ku suspect vibaya!!!! Deposit tu za benki unashtuka shituka.Kenya kiwango cha kushitukia deposit au transfer ni dola laki tano or equivalent.Sisi hapa tu milioni sijui 25 mtu ajieleze Looooo.Kampesa sijui ka tu shilingi milioni sijui mbili toa maelezo mtaua sekta ya fedha.Watu wanapoingiza fedha toka nje mara ingine fumba macho kama kufuatilia fuatilia kimya kimya kama una suspect kitu sio tu kupiga miyowe .Wenzetu wasiri viongozi wa Afrika wakiiba na kupeleka kwao kuweko mabenki yao au kununua majumba nk wameufyata kimya kama hawajaona sababu zinaenda kuchangamsha uchumi wao.Kuamasha uchumi sio lelemama kuna maeneo mengine unatakiwa kuwa msiri na unapotezea kimya kimya.Pesa za kuhangaika nazo sana ni za serikali hizo ndizo uchunge sana hizo zingine za nje ya serikali chukulia poa tu achana nazo unless una suspect kitu fulani kibaya . Private money sio za kuvalia njuga ohhh unadeposit milioni 300 umetoa wapi.Kwani kwako serikalini kumeibiwa? Labda kama ni mfanyakazi wa serikali hapo sawa kuhojiwa sababu kuna maadili ya viongozi wa serikali nk.Lakini kwa private sector na watu binafsi ambao hawako public sector serikali iwe makini huko isipende kuchungulia chungulia na kuweka vitu vya kuchokonoa chokonoa huko ooh yule mbona anaingiza nchini dola milioni Moja.Kausha.Anakuingizia pesa kwenye nchi yako kama kufuatilia iwe kimya kimya Bila yowe asije shindwa kukuletea siku ingine sababu pesa hizo aweza kuwa kacheza kamari au kapata za Biko nk huko atokako kaamua kuja kuzilia nyumbani.Viongozi wetu kuweni wasiri jamani.Hata hayo madeposit sijui na miamala sijui iwe kiasi gani mngenong'onezana vikao vya ndani na mabenki na makampuni ya simu na maafisavAirports zetu na mipakani kuwa waripoti tu kama Wana suspect kitu kibaya Basi.No suspicion wakaushe mtu aingize pesa nchini au ku deposit au ku transfer kimya kimya.Na mkimdaka mtu suspect msipige yowe kuwa tumekamata mtu anaingiza pound milioni Moja .Mumalizane kimya kimya
Hakuna haja ya kupiga tarumbeta kwenye public.Watu watasusa kuleta hela iwe kwa transfer za bank au cash.Maswala ya haya mambo ya money laundering yanataka usiri na umakini mkubwa.Ukienda papara unaua sekta ya fedha na biashara ndani ya nchi
 
Uongo wao ni wakali mno kama unatoka na pesa kwenye nchi zao lakini kama unaingiza wala hawakuhoji wala kukusumbua.Ndio maana mapesa kibao huingizwa mabenki ya uswisi na offshore banks.Wao wanataka ziingie ndio maana hata ukisafiri nchi zao unatakiwa kupeleka benki statement wajue utawaingizia pesa.Hicho ulichonacho kwenye benki statement hawahangaiki kuhoji.Beba dola zako au pound zozote nenda nazo ulaya au Marekani uone kule kama kuna atakayekuuliza.Lakini Beba hizo pesa uje nazo nchi zetu za Dunia ya tatu utakoma.Hii vita ni kitu cha vi nchi maskini ndio vinavalia njuga.Nigeria hiyo Sheria ya money laundering walikataa wakasema ni uonezi kwanza dola elfu kumi ni hela ndogo pili mbona kwao viongozi wa Nigeria wanaingiza mabilioni nchini kwao mbona hawafuatilii wala kupiga makelele.Kwenye hii vita tutaumizana bure.Mtu kama unaingiza pesa usiwe mkali mno Kila kitu Ku suspect vibaya!!!! Deposit tu za benki unashtuka shika.Kenya kiwango cha kushitukia deposit au transfer ni dola laki tano or equivalent.Sisi hapa tu milioni sijui 25 mtu akieleze Looooo.Kampesa sijui ka tu shilingi milioni sijui mbili toa maelezo mtaua sekta ya fedha.Watu wanapoingiza fedha toka nje mara ingine fummba macho kama kufuatilia fuatilia kimya kimya kama una suspect kitu sio tu kupiga miyowe .Wenzetu wasiri viongozi wa Afrika wakiiba na kupeleka kwao kuweko mabenki yao au kununua majumba nk wameufyata kimya kama hawajaona sababu zinaenda kuchangamsha uchumi wao.Kuamasha uchumi sio lelemama kuna maeneo mengine unatakiwa kuwa msiri na unapitezea kimya kimya.Pesa za kuhangaika nazo sana ni za serikali hizo ndizo uchunge sana hizo zingine za nje ya serikali chukulia poa tu achana nazo unless una suspect kitu fulani kibaya . Private money sio za kuvalia njuga ohhh unadeposit milioni 300 umetoa wapi.Kwani kwako serikali ni kumeibiwa Labda kama ni mfanyakazi wa serikali hapo sawa kuhojiwa sababu kuna maadili ya viongozi wa serikali nk.Lakini kwa private sector na watu binafsi ambao hawako public sector serikali iwe makini huko isipende kuchungulia chungulia na kuweka vitu vya kuchokonoa chokonoa huko ooh yule mbona anaingiza nchini dola milioni Moja.Kausha.Anakuingizia pesa kwenye nchi yako kama kufuatilia iwe kimya kimya Bila yowe asije shindwa kukuletea siku ingine sababu pesa hizo aweza kuwa kacheza kamari au kapata za Biko nk huko atokako kaamua kuja kuzilia nyumbani.Viongozi wetu kuweni wasiri jamani.Hata hayo madeposit sijui na miamala sijui iwe kiasi gani mngenongonezana vikao vya ndani na mabenki na makampuni ya simu , Airport's zetu na mipakani kuwa waripoti kama Wana suspect kitu Basi.No suspicion wakaushe mtu aingize pesa nchini au ku deposit au ku transfer kimya kimya.Na mkimdaka mtu suspect msipige yowe kuwa tumekamata mtu anaingiza paid milioni Moja .Mumalizane kimya kimya
Hakuna haja ya kupiga tarumbeta kwenye public.Watu watasusa kuleta hela iwe kwa transfer za bank au cash.Maswala ya haya mambo ya money laundering yanataka usiri na umakini mkubwa.

Well said Yehodaya.
Hivi vinchi masikini kama cha kwetu tunabanabana watu kwa pesa mbuzi kama dola 10000.
Hakuna Taifa la Money laundering kama Marekani, Wao Dola huwa wanachapisha tu wakijisikia kwa sababu wanajua kuwa Dola yao ina demand kwa hiyo itahitajika tu na Pia yupo Saudia pale atauza wese kwa dola tu na kuipa value hata kama wataprint. Lakini sisi akina hohehahe tunajiingiza katika vita siyo ya kwetu tunaanza kumaindi hata vidola 1000 hadi 10000!. Dola 10000 ni hela ambayo Messi anaitengeneza kwa dakika halafu SISI huku akina DR MPANGO wanataka kutusumbuasumbua kujaza maripoti sijui kitu gani.
THESE PEOPLE ARE NOT SERIOUS!
 
Kitu usichokijua ni kwamba wakati unasema uongo kuhusu Ulaya na Marekani kwenye mitandao, kuna watu humu wanaishi huko. Usifikiri kuwa wote humu tuko huko Buguruni. Ulaya gani hiyo ukimtumia shangazi yako $1000 kwenye nchi hiyo hiyo inatolewa taarifa?
JF bwana inakizazi ambacho kinaumaskini mkubwa wa kuchakata taarifa wanazopokea, jilizisheni kwanza taarifa husika na ukimbilie jukwaa kutoa maoni.
jambo jingine jifunzeni kidogo huko ulaya wanafanyaje kuhusu mambo hayo ya transaction? kwa dunia ya leo hupiti na hela zaidi ya dola elfu kumi air port mpaka uitolee taarifa, haya mambo hayajaanza kwetu bongo,yapo kitambo kwa wenzetu sema sie ndo tunaanza labda
 
Kwa waliowahi kufika Ethiopia watakubaliana nami kuwa tunaelekea Ethiopia sasa. Kama walivyo Waethiopia, tutaanza kuikimbia nchi yetu katika hii miaka 10 ya hawa watu.
Mkuu, nishaanza kufikiria kuhamia kati ya Uganda, zambia, na malawi. Hapa bongo kutoboa ngumu sana
 
Safi sana Serikali kwa kuliona ilo, natumaini pia ni njia sahihi ya Watu wanao takatisha Pesa kukomeshwa.

Kuna wengine wananunua Magari ya Fahari wanayajaza Showroom yote hiyo kutakatisha Fedha.

Hii njia ni Bonge la Mwarobaini kwa Serikali yenye juhudi za kuweka Usawa. Pongezi Waziri Dr Mpango heshima kwako.
Kwahiyo wewe inakuuma nini kuona mtu kanunua magari ya kifahari? Au ni kwasababu huna uwezo? Akili za kimaskini sana hizi mkuu. Badala uwaze namna ya kutafuta pesa Unashangilia kuona tajiri anabanwa?

Tajiri mmoja anauwezo wa kuajiri watanzania wengi. Sasa ukimbana huyo tajiri unamuumiza nani? Hivi unafikiri tajiri wako akiminywa utaendelea kupokea hako kamshahara kako ka mawazo?

Uchumi wetu ndo unaenda jehanamu hivyo, hakuna mwekezaji (FDI) atawekeza Tanzania kwa sheria za namna hii.
 
Back
Top Bottom