Kanuni mpya ya Bunge, hakuna hoja bila kukubaliwa na chama

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
5,457
4,351
Ndugu wana JF, nimesoma habari hii, inayohusu kanuni mpya ya Bunge letu. Kanuni hiyo inamtaka Mbunge awasilishe hoja yake kwenye Chama chake kwanza ikikubaliwa ndipo anaweza kuwasilisha bungeni. Naomba kuuliza
a) Kanuni hii itatoa haki ya Mbunge kutoa maoni yake bungeni kwa uhuru?
b) Wabunge wa CCM wataweza kutoa hoja nzito mfano za ufisadi?
c) Kumekuwa na adhari gani mbaya katika mfumo uliokuwa unatumika?
d) Je kanuni hii ina yapi mema kwa Watanzania?

Habari hiyo ni hii

Posted Date::4/16/2008
Kanuni mpya yawafunga mdomo wabunge
*Yawataka kupitishia hoja zao kwenye vyama

*Makinda alieza kwanini hoja ya Rostam ilizuiwa

Na Ramadhan Semtawa, Dodoma

MOJA kati ya kanuni mpya za Bunge ambazo zimeanza kutumika katika mkutano unaoendelea mjini Dodoma, inawafunga mdomo wabunge kwasababu kuanzia sasa watalazimika kupitisha hoja zao binafsi kwenye kamati za uongozi za vyama vyao.

Kanuni hiyo mpya iliibua mjadala mkubwa bungeni jana baada ya Naibu Spika, Anna Makinda kuitolea ufafanuzi kufuatia baadhi ya wabunge kuozungumzia hoja zao katika vyombo vya habari, kabla ya kuzipitisha kwenye kamati za uongozi za vyama vyao kupata baraka.

Makinda pia alinukuu kanuni ya 110, ambayo imewekwa mahususi kwa ajili ya kuviwezesha

vyama kujiwekea utaratibu bora wa kuratibu masuala ya vyama vyao, pamoja na kushughulikia masuala mbalimbali yanayokusudiwa kuwasilishwa bungeni.

Alisema utaratibu huo upo katika mabunge yote ya Jumuiya Madola, ambayo ndiyo wakati

mwingine huwezesha kambi moja kususa na kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge.

Makinda aliongeza kwamba, azma ya kuweka kanuni hiyo ni kuwezesha uwajibikaji wa

pamoja kichama bungeni(Collective Responsibility).

Kanuni hiyo inataka mkakatika kifungu cha kwanza (1) kwamba: �Kamati za

vyama vya siasa bungeni zitajiwekea utaratibu kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli

zake,� inasema nakuongeza katika sehemu ya pili (2) kwamba:

�Majadiliano yote kwenye mikutano ya kamati na mengineyo yanayohusu Kamati hizo yatakuwa na hadhi, kinga na nafuu zote zinazotolewa kwa mujibu wa sheria kuhusu majadiliano, kumbukumbu na mambo mengineyo ya Bunge na Vikao vyake kwa mujibu wa mashariti ya Ibara ya 100 (1) na (2) ya Katiba na Sheria ya Kinga, Madarakana Haki za Bunge.�

Kutokana na maelezo hayo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alisimama

na kumtaka Naibu Spika kwanza, aeleze maslahi yake kutokana na kwamba yeye ni mjumbe

wa Kamati hiyo ya CCM.

Pia Zitto aliwatetea wabunge hasa wa CCM akisema kuwa mara nyingine kamati za vyama zinanyima wabunge demokrasia katika kuwasilisha hoja na maelezo yao, kwa kutumia njia mbalimbali zinazokubalika bungeni.

Wakati Zitto akieleza hayo huku akiwatetea wabunge wa CCM, wabunge wa chama hicho

tawala waliku wawakiguna:, �Mmh!, huku wakionekana kumkejeli.�

Hata hivyo, Makinda alijibu akisema amezungumzia kanuni na wala si mambo ya chama

kama ilivyoelezwa na Zitto na kufafanua kimaslahi, hakuna asiyejua kama yeye na Spika wanatoka CCM jambo ambalo liko wazi.

Baada ya hapo, Anna Abdallah aliomba mwongozo wa Spika, akihoji maslahi ya wabunge hao

wa upinzani kuwazungumzia wa CCM.

Makinda alisimama na kufunga mjadala akisema: � Waheshimiwa wabunge, hiyo kwa kiingereza tunaita 'light moment'. Hapa bungeni hatupo kwa ajili ya maslahi ya chama bali kwa sote tupo hapa kwa maslahi ya wananchi.�

Katika hatua nyingine, uamuzi wa Spika wa Bunge Samwel Sitta, kumzuia Rostam Azizi, kuwasilisha maelezo yake binafsi kuhusu sakata la Richmond, umeibua mjadala bungeni.

Mjadala huo ambao siku zoteulikuwa ukienda chini kwa chini, jana uliwekwa hadharani

baada ya Naibu Spika kuzungumzia suala la Rostam.

Dalili za kuibuka mjadala huozilianza kujitokeza baada ya Naibu Spika Makinda, kusoma taarifa ambayo kwa wachambuzi, waliweza kubaini ilionekana kuwa na siri nyuma

yake.

Katika taarifa hiyo, Makinda aliongeza kwamba baadhi ya wabunge hao wamekuwa wakifanya hivyo hata kabla yakupata baraka za vyama vyao vya siasa kuhusu hoja au miswada hiyo.

Baada ya maelezo hayo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed

alihoji mwongozo akisema:, �Hivi kama mbunge ameshaleta hoja binafsi bungeni, je bado chama kina nafasi?�

Mara baada ya Rashid kumalizakuomba mwongozo, Makinda alimtaka atoe mfano wa mbunge,

ndipo akasimama na kumtaja Rostam, kwamba litaka kutoa maelezo binafsi kama

alivyotakiwa na Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond, lakini

akazuiliwa.

�Waheshimiwa wabunge, nimefurahi sana hili la Rostam kuulizwa, suala hili limekuwa likizungumzwa,� alisema Makinda, akithibitisha kwamba tangu awali kuna kitu alikuwa

akikilenga ambacho kilijificha nyuma ya taarifa yake.

Bada ya hapo Makinda alifafanua sakata hilo, akisema kanuni ya 54(4) pia ilitumika

kumzui Rostam kuwasilisha hoja hiyo ambayo tayari ilikuwa katika kumbukumbu za Bunge

(Hansard), huku maelezo yake yakiwa hayana tofauti yoyote na aliyowasilisha katika

Mkutano wa 10 wa Bunge.

Alisema Spika aliona hakuna haja ya kuibuliwa mjadala ambao ulishafungwa huku pia mbunge huyo, akitaka kurudia maneno ambayo tayari ameshatoa na yapo katika kumbukumbu hizo.

Hata hivyo, haikuthibitika n ivipi maelezo ya Rostam katika mkutanohuu wa 11 yalikuwa ni sawa na ya awali, kutoka na mambo hayo kuwa siri kati ya Ofisi ya Spika na Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kamati ya Uongozi ya CCM inaundwa na wabunge wote wa chama hicho ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu (CC), wakiwemo Naibu Spika na Spika wake.

Katika siku za karibu, uamuziwa Spika kumzuia Rostam kutoa maelezo binafsi umeonekana kuibua hisia tofautindani ya bunge.

Baadhi ya wabunge wanahisi uamuzi huo wa kumzuia Rostam haukuwa sahihi, kwani

unaonekana kuwa na shinikizo la Kamati hiyo ya CCM, huku wengine wakiona hakukuwa na

haja ya kurudisha mjadala wa Richmond.

Katika maelezo ya Rostamkatika mkutano wa 10 wa bunge, ambayo yapo katika kumbukumbu za bunge pamoja namambo mengine alikana kuwa na hisa au umiliki wa aina yoyote ndani Kampuni ya Richmond.

Pia Rostam alisema, Spika Sitta alishindwa kudhihirisha kauli mbiu yake ya Kasi na Viwango katikautekelezaji wa majukumu ya Kamati Teule, hasa baada ya kuongeza muda baada ya kamati hiyo kuwa haijatoa mapendekezo.

Source. Mwananchi
 
Mie nafikiri ungejaribu ku-edit title yako ili ilete maana kidogo. Labda ungebadilisha kidogo iwe Kanuni Mpya ya Bunge badala ya Mbunge. Sorry, ni mtazamo wangu. Ombi linaweza kukubaliwa au kukataliwa.
 
Wakati wanajaribu kuficha zaidi sisi tunafumua zaidi wakija kushutuka hakuna cha kuficha tena. hii ni mbinu ya kuta kuwaziba midomo wabunge kwasababu kitu ambacho chama kitaadhilika hakitakubaliwa na chama kisemwe bungeni.
Mapambano ya fikra ni kitu kigumu sana wanaogopa kiasi kwamba wanatamani tusingekuwapo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom