Kanuni mpya: Mchezaji asiyepimwa afya marufuku kucheza soka Tanzania

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
MCHEZAJI yeyote atakayesajiliwa msimu huu hataweza kupatiwa leseni ya kucheza soka ikiwa hatapimwa afya yake na kuidhinishwa kwamba ni mzima.

Hayo ni miongoni mwa masharti matatu yaliyopitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliyoketi Jumapili Julai 30, 2017 ambapo pamoja na kupimwa afya, inatakiwa pia mchezaji husika awe amekatiwa Bima ya Afya na klabu yake.

FikraPevu imeelezwa kwamba, kanuni hizo zitaanza kutumika msimu huu wa 2017/2018 na mbali ya Ligi Kuu, zitahusisha pia Ligi Daraja la Kwanza na Daraja la Pili.




Kwa makala nzima soma Kanuni mpya: Mchezaji asiyepimwa afya marufuku kucheza soka Tanzania
 
Wawe wanahakikiwa na umri maana wachezaji wa kiafrika wanadanganya sana kwenye umri.
 
Apo kwenye Bima ya Afya ndo pataleta ugomvi tena mpaka ligi daraja la kwanza na la pili, kuna team ligi kuu tu zinasafiri na vyombo vya kupikia kwenye gari.....
 
Back
Top Bottom