Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanuni hizi za bunge zipitiwe upya kwa manufaa ya taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 12, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Wakati watanzania tuko kwenye mchakato wa katiba mpya naamini ni wakati muafaka na wabunge kupitia upya kanuni na taratibu za kuendesha bunge kwani zina mapungufu makubwa na ni janga la kitaifa kwa kuzingatia umuhimu wa bunge.Nitatoa mifano michche ambayo mimi kwangu hainiridhishi:-

  1. Spika,naibu spika na wenyeviti wawe watu huru
  Hii ni kutokana na viongozi hawa kusimamia na kuendesha bunge kwa kuzingatia itikadi za vyama vyao badala ya kufuata kanuni na matokea yake ni mambo kama upendeleo na uonevu ktk maamuzi.

  2. Kanuni juu ya mwongozo na taarifa
  Hii kanuni kwakweli ina upungufu sana kwani inampa spika mamlaka ya kutoa muongozo wakati wowote anaoona unafaa.Nadhani hapa spika anatakiwa awekewe kipengele cha kumbana kwamba ni lazima atoe muongozo ndani ya kipindi fulani na anaposhindwa kufanya hivyo awasilishe sababu bungeni.Vile vile iwe ni lazima kwa spika kupokea muongozo na taarifa kutoka kwa wabunge kwani hivi sasa anaweza kukataa kuruhusu muongozo au taarifa kutolewa.

  3. Taarifa za kamati kutegemea ruhusa ya spika
  Sina uhakika sana na kanuni hii ila kama kweli taarifa ya kamati ya bunge juu ya uchunguzi wa jambo fulani ni lazima kwanza ipate ruhusa ya spika ndio taarifa hiyo iruhusiwe kusomwa bungeni hili nalo ni tatizo kubwa. Nashauri taarifa yeyote ya kamati ya bunge ni shariti isomwe bungeni na spika apewe taarifa tu juu ya uwasilishaji lakini asiwe muamuzi.

  4. Maamuzi yanayohusu mambo mazito kama upitishaji bajeti yawe kwa kura ya siri na sio kwa mtindo wa kuhoji wabunge kwa pamoja.

  5. Wabunge walipwe posho baada ya kusaini mara mbili asubuhi na jioni ili kudhibiti utoro na anaesaini mara moja kwa siku alipwe nusu posho.

  6. Kanuni zipige marufuku mambo kama pongezi za kifamilia na hata mawaziri wasilazimike kuwataja(kuwatambua)wale wote waliochangia ili kuokoa muda na labda anaweza kuwashukuru kwa ujumla tu.

  7. Na kanuni zingine zote ambazo ni kikwazo cha maendeleo kwa taifa letu.

  8. Hoja kwamba jambo lilkishajadiliwa na kufanyiwa maamuzi basi jambo hilo ndio limefungwa rasmi kwa maana ya kwamba halitarudishwa bungeni tena. Kanuni hii ni ya ovyo na inalenga kulea uozo serikalini. Athari ya kanuni hii ni kuhusu mambo kadhaa kwa mfano kashifa ya richmond ambayo kwa sasa imeshafungwa rasmi kujadiliwa bungeni na hata swala la uuzaji wa nyumba za serikali.

  Hapa cha msingi ni kuzingatia nyakati na kama kuna taarifa au ushahidi mpya unaoweza kusaidia jambo fulani kwa wakati wowote jambo husika lilrudishwe bungeni. Pia inawezekana maamuzi ya nyuma yalifanywa kimakosa kutokana na taarifa zilizokuwepo kwa wakati huo na kuna umuhimu wa kuzingatia taarifa mpya au hata mazingira ya wakati wa sasa.
   
 2. D

  DNA Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  safi i read between the lines nakubaliana na wewe 100%
   
 3. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Nashukuru mkuu.
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kabla kulijadili hili , Mtoa mada ulitakiwa ujue ni nani mwenye mamlaka ya kutunga Kaanun za Bunge. Kumbuka kuwa kaanua hizo za Bunge hazimi kwenye marekebisho au katika katiba mpya mnayokusudia kuiandika hivi karibuni.

  Mwanye mamlaka ya kutunga kaanun za Bunge ni wabunge wenyewe ndani ya bunge . Hivyo ni vizuri wabunge hao kwa utashi au kukwazwa kwao na kaanun hizo watachukua nafasi kuomba mwongozo wa kuzitengua na hata kuzifuta na kuweka kaanun muafaka kutokana na wakati husika.

  Kifupi mwenye mamlaka ya kubadilisha kaanun za Bunge ni wabunge wenyewe.
   
 5. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45  Hapo kwenye red naomba ingeongezwa sentesi hii 'tena saini za waheshimiwa ziwe zinachukuliwa mwishoni na si mwanzo wa sessions ili kuepuka zoezi la kusaini na kuondoka
   
 6. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  mnasumbuliwa udhaifu wa kujenga hoja na ukosefu wa nidhamu2, hakuna ziada
   
 7. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Mkuu soma vizuri maelezo yaliyotolewa.Nilichosema ni wabunge wenyewe wabadilishe kanuni za uendeshaji bunge.Swala la katiba limegusiwa tu ili liende sambamba na wabunge kupitia upya kanuni za bunge.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Akina nani wadhaifu??
   
 9. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Bila shaka wewe ni sehemu ya magamba wanaonufaika na kanuni hizi.
  Hivi hizi kanuni ni msaafa au ni maandiko matakatifu ambayo huwezi kuyabadili?Nipe jibu.
   
 10. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  unakubaliana na ulipanaji wa posho sio?
  Wabunge hawalitumikii bunge, wanawatumikia wapigakura wao, hivyo basi wasilipwe na ofisi za bunge bali walipwe na waajiri wao kupitia halmashauri zao na mishahara yao ipitishwe na madiwani, iandaliwe kwa mapendekezo ya wapigakura na kujadiliwa na wataalam katika mjadala huru, wabunge waruhusiwe kufanya kazi zao za kitaalamu na kupokea mshahara huko.

  Wabunge wawajibike kwa wapiga kura wao moja kwa moja na si kwa chama wala bunge!
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nafikiri nami ukuwa umenielewa.

  Nilichotaka kubainisha mabadiliko ya kaanun za Bunge iwe kwa faida za Bunge lenyewe kwa kurahisisha uendeshaji wake na sio kama wewe ulivyo generalize kusema kwa faida ya taifa. Kwani kuwepo tu kwa kaanun za muhimili huo ni faida kwa Taifa hususan kwa Utawala wa Sharia (Rules of Law).

   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  89.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza
  kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa
  kutekeleza shughuli zake.
  (2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hii
  zaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuli
  za Sekretariati ya Bunge na pia utekelezaji wa Shughuli za Bunge
  ndani ya Bunge na zile za Kamati na Kamati ndogo za Bunge

  Katiba inatambua uwepo wa kanuni ila hazijaorodheshwa moja baada ya nyingine, hivo ilivo kwa sheria nyingi hazipo kwenye katiba ila msingi na chimbuko lake ni katiba!
   
 13. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  kanuni nyingi sana zilitungwa wakati wa bunge la chama kimoja na hazikufanyiwa marekebisho ya makubwa ili kulinda chama tawala na serikali!spika anahimiza maswali na majibu kuulizwa au kujibiwa kwa kifupi lakini wakati huohuo anachukua muda mrefu sana ktambulisha wageni sijui wanafunzi,cjui mke wa waziri, sijui wapiga kura, mawaziri nao wanataja wachangiaji mlolongo hauna maana hata kidogo!
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Nimeshangazwa sana sana na kutojua kanuni za uendeshaji wa mabunge ya nchi za Commonwealth, nenda kazisome then ndipo uje na uzi wenye maana kwetu, kwa hapo umekurupuka sana tu
   
 15. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Kama issue ni commonwealth basi hata ushoga turidhie ili tuende sambamba.
  Inawezekana ulinufaika na hela za richmond zinazolindwa na kanuni hizi mbovu.
  Pia acha kukariri commonwealth kwani hiyo sio sababu.
  Iga kilicho bora na sio kuburuzwa na ujue wenzetu wana nidhamu na wana uzalendo.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hiyo ulioiweka ni sharia inayotambua kuwepo Kanuni za kudumu za Bunge Sheria namba 14 ya mwaka 1984. Ibara ya 14 kifungu cha 89 (1,2)

  Nazidi kukushauri hebu pitia Sharia ya Mamlaka ya Bunge Sharia namba 15 Ibara ya 2 ya mwaka 1984 na Sharia namba 20 ibara 11 ya mwaka 1992.

  Kwa kupitia hapo utabaini wazi Katiba ya Tanzania imelitambua Bunge na kaanun zake. Lakin mwenye Mamlaka ya kutunga Kaanun hizo ni WABUNGE WENYEWE na sio wananchi.

  Na haiyumkiniki kabisa kuwa mnapofanya au kuandika Katiba Mpya basi ni lazima na Kaanun hizo za Bunge ziandikwe upya. Hilo sio sahihi. Mabadiliko ya Kaanun za bunge yanafanywa na wabunge wenyewe pale wanapoona kuna ulazima wa kufanya hivyo kulingana na matakwa na wakti.


   
 17. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Kwa yaliyotokea leo bungeni ni wazi kanuni za bunge hazifa kwani kila kiti ni maamuzi ya spika na ni wazi anaibeba serikali ka manufaa ya chama chake.
  Leo hii kambi rasmi ya upinzani imezuiwa kusoma maoni yake juu ya kipengele cha mauaji yenye sura ya kisiasa kwa kisingizio kesi hizo ziko mahakamani na mojawapo ya mambo yaliyozuiwa ni kuhusu mateso na kipigo cha Dr. Ulimboka.Hii ilikuwa baada ya Lukuvi kuomba muongoza kwamba kipengele hicho kisisomwe bungeni kwani kuna kesi iko mahakamani
  Hotuba ilikuwa ni ya wizara ya mambo ya ndani na upinzani walikuwa wanasoma mapendekezo yao juu ya hotuba ya wizara ya mambo ya ndani.
  Kanuni hizi ni mbovu kwani spika amepewe madaraka makubwa mno.
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0

  Nafikiri ahali yangu kama utapunguza ushabiki na kuangalia Katiba yenu hususan pale inapozungumzia separation of power katika Rules of law. Utaona nchi yenu inaongozwa na mihimili Mitatu nayo ni Mahakama, Bunge na Serikali. Na kila kimoja katika hivyo kimepewa mamlaka yake kamili bila kuingiliwa na muhimili mwingine katika utendahi wa Shughuli na kazi zake. Soma Sheria namba Na.15 ib.6 ya 1984, kifungu cha 4 chote.

  Hivyo Bunge wapo sahihi kabisa kisharia kuwa hawaruhusiwi kabisa kujadili kitu chochote au shauri lolote lile kilichopo mahakamani

   
 19. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,039
  Likes Received: 37,823
  Trophy Points: 280
  Mkuu bunge ni chombo cha uwakilishi kwa umma wote wa watanzania kwani haiwezekani kila mtanzania akaenda pale bungeni na wabunge ni wawakilishi wetu kwahiyo wanayoyafanya si kwa manufaa au faida ya bunge lenyewe kama ulivyodai bali ni kwa faida ya watanzania wote kama taita kwa kupitia bunge hilo. Hivi ni kweli uelewi jambo hili au una ajenda yako binafsi!
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0

  Ahali yangu nimekubainishia wazi kama Utapunguza USHABIKI na KULALAMIKA na kutulia kitako kusoma vizuri Katiba yenu utajifunza mengi sana. Kumbuka kuwa katika dhana ya Rules of Law, utaona kila muhimili una kazi zake.

  Kazi za Bunge ni kutunga sharia
  Kazi za Mahakama ni kutafsiri Sharia zinazotungwa na Bunge.
  Kazi za Serikali ni Kusimamia sharia zinazotungwa na Bunge.

  Na hata ukisoma Katiba hiyo hiyo inasema wazi Serikali inawajibika kwa wananchi kwa sababu Serikali ni ya watu. Soma Katiba yya JMTz katika kuona Serikali na watu sharia namba 15 Ibara ya 6 ya mwaka 1984. Imebainisha hivyo.

  Lakin vile vile angalia Sharia hiyo iliyotungwa na Bunge kuhusu separation of Power.
  Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi Sheria namba Na.15 ib.6 ya 1984, kifungu cha 4

  4
  .-
  (1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri

  ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili

  vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka

  ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye

  mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa

  shughuli za umma.


  (2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya

  Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki

  vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya

  Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya

  Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na

  kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni

  Bunge na Baraza la Wawakilishi.


   
Loading...