Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Naomba nipewe muongozo kuhusu kama mtu ameathiriwa kwa Kansa ya Kichwa anaweza kupata tiba hapa hapa Tanzania. Jamaa alikuwa ana uvimbe uliotokeza kwa nje ya tumbo lake upande wa kushoto. Akaenda Hospitalini akafanyiwa Opereshni ya kuuondoa uvimbe huo na baada ya Operesheni hiyo akafanikiwa kuishi hivyo kwa kipindi cha miaka 4. Uvimbe ukajirudia tena akafafnyiwa tena operesheni na Daktari aliyemfanyia akamhakikishia kwamba "amekwangua" kabisa chanzo cha uvimbe.
Miezi mitano baadaye uvimbe ukajirudia na kufanyiwa Operesheni Muhimbili. mwisho wa siku madaktari wa muhimbili wakamwambia ni Kansa na tayari imeweka uvimbe kwenye ubongo wake na kusababisha apooze upande mmoja. Sasa amepelekwa Ocean Road Hosp anakopata tiba ya mionzi.
Kama inawezekana kuondoa uvimbe ulioko kwenye ubongo kwa mionzi au kuna tiba mbadala naomba nielimishwe. Au ndiyo mpaka aende India?