Kanivunjia simu zangu kwa sababu nisizozijua

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,791
8,739
Nipo nae yapata 2yrs na miez kadhaa, huyu binadamu ameoa na anawatoto wa 2, tumefanya vitu vingi vya maendeleo ikiwa ni pamoja na kufungua kampuni na baadhi ya miradi mingine midogo midogo, aliamua kushirikiana nami baada ya kuona mkewe kila akimfungulia biashara inakufa na akitafutiwa kazi miezi 2 tu anashindwa na kurudi nyumbani.

Kuna baadhi ya miradi tumeshare na mingine kila mtu kasajili kwa jina lake hakuna siku tumegombana ila kuna kupishana kauli tu mara moja moja. Jana kuna document nilimpelekea ofisi kwake nilipofika nikaongea na secretary km anaweza kuniruhusu niingea ndani akanambia anawatu, baadae secretary alioona wageni wake wametoka akaniruhusu nikaingia.

Nilipoingia kule ndani ghafla simu yangu ikaita, nilipokea na kuaza kusema na aliyenipigia ghafla mwenzangu akanipokonya ile simu na kupigiza chini na kuivunja vunja, akaninyang'anya mkoba wangu akachukua na simu nyingine akaibonda bonda, kibaya zaidi na laini akaziharibu kabisa, kulitokea ugomvi bahati yangu kulikuwa na watu wengine, me ikabidi nitoke na kuondoka, sikulala nyumbani kwangu kuogopa angeweza kuja usiku.

Nimeumia sana kwa hili tukio kwani angehoji kwanza hata angetaka nimpe namba ya niliyekuwa naongea nae ningempa kuliko hiv alivyofanya, sjaelewa hadi sasa nini hiki!!

Mawazo yenu tafadhali
 
hapa dhambi ya kumchukulia mume wa mtu inakujongea,tena shukuru hamiliki bastola ange ku ufosarolisation
 
kama mna miaka yote hiyo hajawahi lazima kuna ukweli hujatuambia hapa! hawezi kukurupuka! jipange uje tena!
 
Vunjeni ngalawa! Mugawane mbao!
Utafute mtu akuoe!
Zinaa ni dhambi,but na mme or mke wa mtu ni dhambi zaidi!
...
Wake up! Nyanyua macho uangalie mbele!
Usiwe na mtazamo kama wa jongoo! Eti hadi ujigonge ndio utambue hapa hakuna njia!
Angalia kama ngedere vile! (ngedere hupanda juu kileleni and then anasimama na miguu ya nyuma anakuwa kama mtu vile! Hapo huweza kuangalia hata meter 3000!)
...
Peleka muda!
Uskubali muda ukupeleke!
 
, sikulala nyumbani kwangu kuogopa angeweza kuja usiku.

Nimeumia sana kwa hili tukio kwani angehoji kwanza hata angetaka nimpe namba ya niliyekuwa naongea nae ningempa kuliko hiv alivyofanya, sjaelewa hadi sasa nini hiki!!

Mawazo yenu tafadhali
kama huna kosa kabla ya kuja jf...ungeanzia hapa...
kituo+cha+polisi+msigiri.JPG
 
Umeona hili nililokufanyia halikutoshi sasa umeamua kuja kuniaka mbele ya kadamnasi niache nitulie na my wife wangu
 
Chezeya wivu usiokuwa na limit weye!!! Shukuru Mungu hakukuwa na bistola au tindikali karibu, pole sana.
 
Kuna kitu nyuma ya pazia, subiri hasira zimuishe myamalize ila kumbuka si wako huyo anamwenyewe.
 
Kumbe we small hauz!! Ungekuwa mke ningekushauri!! Ngoja zahrawhite aje atakupa ujanja!
 
Back
Top Bottom