pastor masumbuko
Member
- Apr 23, 2016
- 67
- 195
Watu wa MUNGU, bwana asifiwe, pia naomba niwatakie walio katika mfungo funga njema, MUNGU awatangulie njia nzima hadi mwisho wa Ramadhani.
Wakuu nina jambo limenisibu siku ya jana naomba mawazo yenu kama watu wazima.
Jana muumini wangu mmoja alinipigia simu kuwa ana shida ya kuonana na mimi kwa ajili ya maombi binafsi. Unfortunately, Jumatatu huwa ndio siku yangu ya mapumziko, weekends nakua busy sana na huduma za kanisani, hivyo Jumatatu huwa napumzika sigusi kazi yeyote na sitoi huduma yoyote.
Hivyo nikamjibu yule dada kuwa leo sipo ofisini, ila kwa sasa nipo beach napunga upepo nikitafakari kazi za wiki nzima. Akanibembeleza sana aje beach tuongelee huko huko, nikakubali, akaja, ilikua ni saa tisa mchana, hakukua na watu kabisa zaidi ya wazungu fulani na mimi na yule dada.
Akanieleza ugomvi wake na mumewe ndio shida kubwa iliyomleta kwa maombezi. Anyway, wote na mumewe ni waumini wangu wazuri, tena wana vyeo hapo kanisani kwetu hivyo sikuwahi kujua wana ugomvi mkubwa kiasi hicho, basi nikamfanyia maombi hapo hapo tukiwa tumekaa, na baadae kumpa ushauri.
Nikaagiza chakula na vinywaji tukala huku tukiongea mambo mbali mbali, tulipomaliza kula tukaona tukaogelee, kwa nia njema tu, mimi nilikua nina pensi hivyo nikaingia majini moja kwa moja, yule mtumishi hakua na nguo za kuogelea zaidi ya gauni alilovaa, wahudumu wa ile hotel wakasema wanazo swimming costume za kukodisha @5000 nikawaambia haina shida nitalipia, akapewa.
Basi tukawa tunaogolea pamoja kwa nia njema tu, tulipochoka tukarudi kwenye viti na kuendelea kunywa vinywaji vyetu, ni hapo sasa ndipo mumewe akatokea na iron bar mkononi na kutaka kumpiga nayo mkewe kichwani akampata begani, sikujua nani kamwambia mkewe yuko hapo.
Akamvurumishia ngumi kana kwamba anapigana na mwanaume mwenzie, tukashirikiana na watu wa hotel kumdhibiti na kumpeleka kituo cha polisi, amelala huko hadi leo asubuhi, mkewe alitibiwa Jana na kurudi nyumbani, amefungwa bandage kwenye bega.
Leo asubuhi wote tulienda pale polisi kwa maongezi, maongezi hayo yameshindikana, mke kadai hamtaki tena mume kwa yote yaliyo tokea maana mbele ya mkuu wa dawati la jinsia na watoto yule jamaa amedai kuwa mimi natembea na mkewe, kwamba ametufuatilia siku nyingi, madai ambayo si ya kweli, na ninashangaa yametoka wapi, ni wazi kuna watu kanisani wanamtumia kutaka kuniangusha baada ya kuona ministry yangu imefika mbali, hii ni moja ya mbinu chafu ya watu hao.
Sasa hawataweza, huyu ndugu kesho atafikishwa mahakamani kwa shambulio la kudhuru mwili, ushahidi upo wazi, amemuumiza kwa kiwango kikubwa sana mkewe, amevimba uso na bega pia.
Wakuu, naomba kufahamu katika kulishughulikia hili suala. Je kuna sehemu nimekosea, nilipaswa nifanyeje instead?