Kanisani naenda lakini ukweli ni kwamba matatizo mengi nimeyatatua kiasili

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Kuwa mkweli ni jambo la kheri nami nimeamua kuwa muwazi juu ya maisha yangu.

Mimi ni kijana ambae kwa sasa najitegemea, nimeoa na nina watoto wawili, kwa sasa naishi kwa mshahara wa serikalini na biashara yangu ndogo.

Tangu udogoni nilikuwa mdau mkubwa tu wa kwenda kanisani na wazazi walihakikisha na kusisitiza tuwe tunaenda kanisani, nilijifunza mengi ambayo yalisaidia tabia na mwenendo wangu wa maisha uwe mwema maana nilijifunza vitu kama nisiibe, nisiue, nisisingizie, nisiwe na dharau, nisake maarifa / elimu, nisaidie wasiojiweza, n.k.

IIla wakati nikizidi kukuwa nimiliyaona mengi katika matukio mbali mbali kwa watu niliowajua tunaoenda nao kanisani na wengine wanaoenda misikitini niliweza kuwashuhudia wanarudi katika tiba asili (tiba sio uchawi) walipopatwa matatizo hasa ya mda mredu yalienda kutatuliwa kwa mtaalam japo sio yote yalitatulika. Nkumbuka kuna mtoto alizaliwa vizuri tu hadi kafikia miaka minne hana tatizo ghafla akawa haongei wala kusikia, wazazi walizunguka mahospitalini na makanisani ila wapi, ikabidi tu waende kwa mtaalam tatizo likatatulika maana kuna wabaya walimteka mtoto kiroho.

Tatizo lengine ni kaka yangu alikuwa mbabe hivi sasa akazinguana enzi hizo sekondari na mwenzake wa darasani kwa kumuibia demu kwa ubabe, muda si muda kaka yangu akawa hawezi kukaa kwenye mwanga hata kidogo huko nje akawa anakaa ndani tu analalamika jua linamuumiza macho, kwenda kwa madaktari akapewa dawa nyingi za aina tofauti kwa miezi miwili ila hakuna dalili, kwenda kanisani nako hakuna kitu na mbaya zaidi kaka yangu niseme ukweli tu enzi hizo sijui kama aliujua hata mstari moja wa biblia, Basi ikabidi ifungwe safari aende kutibiwa kwa njia asili tulimpeleka akabaki huko wiki hivi akarudi yupo fresh, ikabaki stori.

Binafsi mimi kuna kipindi nilienda kusoma shule moja hivi (jina kapuni) nikiwa form 3 siku moja naenda chooni usiku nikakutana na kibwengo kijamaa kifupi kama kina kingora kichwani nilitoka nduki balaa kurudi bwenini, shule hio wengi walisumbuliwa na hivi viumbe, siku nyingine tena hivyo hivyo ikanitokea nikiwa form 4 tena mara mbili, ikabidi nipelekwe kwa mtaalam wa eneo hilo mwenye uzoefu na hivyo viumbe basi tullienda kama wanne hivi tukafukizwa mitishamba na tangu siku hio sijui habari za hivyo vibwengo.

Tukio lingine nilipanga huko uswazi nikiwa chuo kwasababu ya uhaba wa pesa basi kuna wiki flani ilikuwa ya mateso sana kwangu, siku za mwanzo nlikuwa nahisi kuna mtu anatembea juu ya dari, ikaendelea na siku ya pili, siku ya tatu ni kama mtu anamwaga mchanga juu ya bati nilikemea sana wakaondoka , baada ya siku mbili asubuhi naamka nina chale kwenye mkono wa kushoto, duuuh!!! nikaona nirudi tu kwetu siku hio hio nikaenda kutibiwa huko nakumbuka waliniambia tu kuna madhara ningepata.

Basi nikafutwa hizo chale na nikachanganiwa miti shamba flani na kinyesi cha nguruwe nikaambiwa nirudi na hico kitu nikiweke darini siku si nyingi ntapata matokeo na kikiyapata nihame, niliuliza matokeo yapi lakini nikaambiwa ntayaona tu, basi nimerudi huko geto nikafanya nlichoambiwa usiku ule nilila bila bugudha nlizozoea ila usiku wa siku ya pili kitu kizito sana kilidondoka kwenye bati usiku wa maanae "PUUUHH!!!

Aisee kila mpangaji alitoka ndani mwake kuangalia ni nini kimedondoka ila cha ajabu hatukuweza kuona, siku 3 mfululizo niligundua kitu tofauti maana mama mwenye nyumba hakuwa akitoka kuotea jua wala kufua nguo, sasa mi nikajua huyo ndio alikuwa jangiri, siku ya nne nilihama na kuchoma dawa nliyopewa, nliaga wapangaji wenzangu tu mama mwenye nyumba hata sikutaka kumuona.

Ni matukio mengi sana tu ambayo kiukweli wengine amam mimi nimeyatatua kwa njia za asili, naweza kuitwa mshirikina lakini kumbe si kweli, nachofanya ni kutatua matatizo kwa njia walizotumia babau zangu enzi toka enzi maana matatizo mengi yalianza hata kabla ya ukoloni na mpaka leo yapo.

Mwisho kabisa napenda tu niwaambie kuna waganga matapeli kibao sana, kwa ushauri nakuomba utafute chifu wa kabila lako au sehemu unayoishi, utaelekezwa kwa mtaalam ambae kizazi chake toka mababu ndio fani yao, usiende kwa wataalam hawa wanaojitangaza mitandaoni, utatapeliwa na wanaweza kukujengea chuki na ndugu zako au familia

Ni hayo tu ndugu zangu.
 
Kuna msemo kwamba 'do everything as if God does not exist for you while you believe he exists'. After all, ni bora kuamini Mungu yupo na kumtegemea yeye maana hupotezi kitu kuliko kutoamini na kuishi kwa wasiwasi kwamba hutaenda kwenye uzima wa milele.
 
Mbaya zaidi huku mtaani wengi wanateswa na hizi mambo lakini hawajui tu. Wengi ni wabishi na wanaamini hizi mambo hazipo,ni wachache sana huzinduka/huzinduliwa na kujinasua ila kundi kubwa sanaa wanaishi kwa mateso kwa kuonewa na wakuu wa shughuli za Giza.

Mungu hakumuumba mja hata mmoja aje ateseke kwa maradhi,uvivu,umasikini,mifarakano,kuchukiwa,kupoteza na mengine mengine mengi bali ni kuvifaidi.

Walinisumbua sanaa kwa miaka zaidi ya 29 wehu hao. Ila Mungu ni mwema,kuna muda huleta msaada.
 
Wewe ni mmoja ya wale wanaoenda kanisani kimwili tu.

Yani mwili upo kanisani ila roho ipo kwa sangoma.

Hazina ya mtu ilipo ndipo ma moyo wake ulipo.

Wewe hasina yako ipo kwa masangoma.
Mkuu tiba salama haijalishi inahitaji tu daktari.

Unaweza ukaumwa kichwa ukaenda kwa daktari hospitali ukapewa panado.

Unaweza ukavwa na funza kwenye kidole ukatibiwa kiasili kwa kupachikwa ndulele

Zote ni tiba tu, unaweza kutumia dini zilizotuk=fikia huku afrika miaka 100 iliyopita au unaweza kutumua tiba asili zilzotumika na mababu zetu zaidi ya maelfu ya miaka,

Binafsi nikiona tatizo kama kuumwa malaria limenipata huwa naenda hospitalini maana malaria ipo sehemu nyingi duniani na dawa ikabuniwa kututibu wengi ila inapokuja swala mfano mtu kapigwa chale basi hali ni tofauti, wazungu hawazijui hizo chale ila huku afrika ni kitu kilichozoeleka na dawa ya kutatua hili tatizo zilishapatikana, kwanini nisizitumie hizi zenye uhakika??,

UCHAGUZI NI WAKO
 
Mbaya zaidi huku mtaani wengi wanateswa na hizi mambo lakini hawajui tu.
Wengi ni wabishi na wanaamini hizi mambo hazipo,ni wachache sana huzinduka/huzinduliwa na kujinasua ila kundi kubwa sanaa wanaishi kwa mateso kwa kuonewa na wakuu wa shughuli za Giza...
HII NI AFRIKA.

Matatizo yetu ya huku huku wapi na wapi mzungu atayajua.

Wazungu hawaamini kuna uchawi kwasababu kwao watu wako bize na kazi za kimaendeleo na mtu kule akitaka akutese anakutwanga risasi tu, huku hali ni tofauti mtu unakuta hana shughuli yoyote yeye yupo kibarazani tu anapiga stori ama kuotea jua akitaka kukukomesha yeye anakukomesha kichawi na lazima uisome namba kama upo bila bila katika dini au mambo ya asili.
 
Binafsi siamini kanisa ama imani juu ya dini ina msaada wowote kwenye matatizo..

Nilifika rwanda kikazi. Tukiwa kule tulitembelea makanisa kadhaa... rwanda kila kanisa lilojengwa zamani nyuma ya 1994.. utakuta lina kaburi kubwaaa...

Kipindi cha mauaji ya kimbari.. watutsi wengi walikimbilia makanisani...wakiamini watapata muujiza wowote... ila wahutu walivyofika makanisani. Walifanya mauaji ya kinyama sana bila msaada wowote wa muujiza wa kanisa.. kuna kanisa nakumbuka jina nyamata catholic church ukifika hapo hata uwe kauzu vipi lazima chozi likutoke ukiona mabaki..

Toka nilivyotoka rwanda nimeona kanisa ni usanii tu kudanganyana na kuwapa watu sadaka
 
Kuna msemo kwamba 'do everything as if God does not exist for you while you believe he exists'. After all, ni bora kuamini Mungu yupo na kumtegemea yeye maana hupotezi kitu kuliko kutoamini na kuishi kwa wasiwasi kwamba hutaenda kwenye uzima wa milele.
.



Uko sahihi mkuu
 
HV hawa watu wanaweza mtafutia MTU Kazi kwel
Au kushinda interview pale unavyoitwaa !
vitu vingine unajiongeza tu, iwe unamwamini mungu au wataalam ukweli unabaki palepale wenye sifa za kazi waliohitimu vyuoni ama hata wenye skills bila kwenda shule wapo mamilioni ila kazi zinazotangazwa ni chache mno hasa katika hii awamu. jiongeze tu ukiona kazi hupati sio tatizo lako na wala hauko peke yako maana hata wenye masters wapo wengi tu hawana kazi, hivyo unaweza hata kujiajiri maana hata wanaosajili laini pia wapo waliokosa ajira wakaamua kwenda kusajili laini na hawakosi pesa ya kukidhi mahitaji yao licha ya kwamba hutilia maanani ya kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
 
Mkuu kama umtendei mtu ubaya hakuna dhambi
Ndio maana napenda kwenda kanisani maana hata biblia pia ina maarifa mazuri tu, Tiba asili nayo ni tiba kama tiba nyingine tu, tuache ushamba wa kudhani ni uchawi
Ntakuja Tz nitakutafuta unipeleke huko MZEE
Ukipata wataalam wazuri na wakweli wenye hofu ya Mungu wala hakuna shida kabisa

Jr
Hakuna dawa ya kweli ya matatizo ya kiroho isipokuwa Yesu Kristo. Wengi wanafikiri kuna waganga wa kienyeji wanaotibu mtu kwa maana halisi ya kutibu.

Watu wanadanganyika sana kwa kufikiri mganga wa kienyeji ni adui wa mchawi. Hapana, wote wanatumikia ufalme ule ule na chanzo cha nguvu zao ni kimoja.
 
Back
Top Bottom