Kanisa: Tumechoka kuzika wanaouawa na majambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa: Tumechoka kuzika wanaouawa na majambazi

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jun 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Na Mashaka Mgeta  14th June 2010


  Latupa lawama kwa Jeshi la Polisi

  Kanisa Katoliki limesema kwamba limechoshwa kuzika waumini wake wanaouawa na majambazi ambao wamekuwa wakilitetemesha eneo la Kimara jijini Dar es Salaam, na kutaka Jeshi la Polisi kukabili hali hiyo vinginevyo wenye dhamana na Jeshi hilo wawajibike.
  Akihuburi katika misa ya Jumapili jana ambayo iliambatana na utoajio wa komunio ya kwanza kwa wanafunzi 100, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Maburunza, Padri Athanas Zengo, alisema kuendelea kuongezaka kwa ujambazi katika eneo hilo ni ishara kwamba polisi wameshindwa kutimiza wajibu wao.
  Padri Zengo aliwataka waumini kupaza sauti zao kwa kuwa kukaa kimpya wakati wenzao wakiendelea kuuawa kila wakati huku wengine wakiendelea kuishi maisha ya hofu kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ujambazi, usalama wa maisha na mali zao utazidi kuwa shakani.
  Kutokana na hali hiyo, kanisa hilo limetoa rai kwa viongozi wenye mamlaka husika, kujiuzulu nyadhifa zao, vinginevyo wananchi hawapaswi kuwachagua tena katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
  Jeshi la polisi lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambayo waziri wake ni Lawrence Masha na Naibu Waziri wake ni Balozi Khamis Kagasheki.
  Kwa mara kadhaa, makundi mbalimbali ya kijamii yamekuwa yakitoa wito kwa mawaziri hao kujiuzulu kutokana na kushamiri kwa ujambazi.
  Kama ilivyozoeleka kwa viongozi wengi, Masha alikaririwa akisema hawezi kujizulu wadhifa huo.
  Lakini katika mahubiri yake ya jana, Padri Zengo alisema, dawa ya viongozi walioshindwa kutumiza wajibu wa kuwalinda raia na mali zao, kutokana na kuendelea kushamiri kwa ujambazi, hawapaswi kuchaguliwa ikiwa watashindwa kujiuzulu wenyewe.
  “Jeshi la polisi liko wapi, polisi mpo wapi mpaka tunapoteza kondoo wetu kwa ujambazi, inaonekana Kova kazi imekuwa ngumu kwake,” alisema.
  Suleiman Kova ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam aliyechukua nafasi hiyo baada ya kustaafu kwa mtangulizi wake, Alfred Tibaigana.
  Padri Zengo alisema binafsi ameshiriki kuwazika waumini watatu wa kanisa hilo waliokufa kutokana na kuuawa na majambazi, hivyo akaiasa jamii kupaza sauti zao ili waliopo madarakani wasikie kilio cha kuchoshwa na uhalifu huo.
  “Tupaze sauti zetu, wasituone tupo kama vile hatujui kinachoendelea, maana tukinyamaza ipo siku mtakuta na sisi mapadri wenu tumeingiliwa na majambazi,” alisema.
  Alitoa mfano wa tukio la kuvamiwa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtoni, ambapo majambazi walipora tabernakul ambayo ni mfano wa nyumba ya kuhifadhi sakramenti takatifu.
  Padri huyo akionekana kukerwa na ujambazi, alisema raia wasiokuwa na hatia wanavamiwa majumbani, huku wenye magari wakishushwa na kutakiwa kuwaelekeza majambazi mahali watakapopata wanachokihitaji.
  “Majambazi wamefikia hatua sasa wanacheza wanavyotaka…tuwaambie kazi imewashinda hivyo mjipange upya ama vinginevyo mjiuzulu,” alisema.
  Padri Zengo alisema inashangaza kuona wakati jamii ikikabiliwa na matatizo mbalimbali, yakiwemo yanayotokana na ujangili, bado kuna watu wanaokubali kuhongwa chakula kama pilau ama khanga na pombe za kienyeji, ili kuwachagua viongozi wasiofaa.
  “Wakati huu si wa kusubiri pilau na kuvishwa kofia na khanga, tujiandae kuchagua viongozi wanaotufaa,” alisema.
  Hivi karibuni majambazi waliua watu wawili, wote wafanyabiashara katika eneo la Kimara, Temboni baada ya kuwavamia wakirejea nyumbani kwao usiku katika tukio lililotokea usiku mmoja. Kadhalika vitendo kadhaa vya ujambazi vimeripotiwa eneo hilo, huku wananchi wakiishi kwa hofu kubwa.
  Kamanda Kova akizungumzia hali hiyo hivi karibuni alisema wananchi wanapaswa kushirikiana na polisi katika kampuni ya polisi jamii kwa kuanzisha vikundi vya ulinzi katika mitaa yao na polisi watashirikiana nao na kuwapatia masaada unaostahili.
  Kamanda Kova alisema kwa sasa ujambazi umekimbia katikati ya Jiji na unaendelea maeneo ya pembezoni, hata hivyo alisema wamejipanga kukabiliana na changamoto hiyo.
  Wakati huo huo, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarpo Kardinali Pengo, atakutana na mapadri wote wa jimbo hilo, katika misa na mkutano utakaofanyika parokiani Mavurunza.
  Kwa mujibu wa matangazo yaliyotolewa kanisani hapo jana, Kardinali Pengo atakutana na mapadri hao Alhamisi ijayo na siku inayofuata, kutafanyika mkutano wa mapadri kutoka Dekania ya Kibaha.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Sasa unashangaa watu bado wanachagua ccm
   
 3. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kimara na Mbezi hatari tupu! Unanyanyasika na uko kwako, mapanga mashoka kwa kwenda mbele, wanachanja kama wanachanja kuni.
   
Loading...