Kanisa: Tumechoka kuzika wanaouawa na majambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa: Tumechoka kuzika wanaouawa na majambazi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngambo Ngali, Jun 14, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Latupa lawama kwa Jeshi la Polisi
  Kanisa Katoliki limesema kwamba limechoshwa kuzika waumini wake wanaouawa na majambazi ambao wamekuwa wakilitetemesha eneo la Kimara jijini Dar es Salaam, na kutaka Jeshi la Polisi kukabili hali hiyo vinginevyo wenye dhamana na Jeshi hilo wawajibike.


  Akihuburi katika misa ya Jumapili jana ambayo iliambatana na utoajio wa komunio ya kwanza kwa wanafunzi 100, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Maburunza, Padri Athanas Zengo, alisema kuendelea kuongezaka kwa ujambazi katika eneo hilo ni ishara kwamba polisi wameshindwa kutimiza wajibu wao.


  Padri Zengo aliwataka waumini kupaza sauti zao kwa kuwa kukaa kimpya wakati wenzao wakiendelea kuuawa kila wakati huku wengine wakiendelea kuishi maisha ya hofu kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ujambazi, usalama wa maisha na mali zao utazidi kuwa shakani.

  Kutokana na hali hiyo, kanisa hilo limetoa rai kwa viongozi wenye mamlaka husika, kujiuzulu nyadhifa zao, vinginevyo wananchi hawapaswi kuwachagua tena katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.


  Jeshi la polisi lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambayo waziri wake ni Lawrence Masha na Naibu Waziri wake ni Balozi Khamis Kagasheki.
  Kwa mara kadhaa, makundi mbalimbali ya kijamii yamekuwa yakitoa wito kwa mawaziri hao kujiuzulu kutokana na kushamiri kwa ujambazi.


  Kama ilivyozoeleka kwa viongozi wengi, Masha alikaririwa akisema hawezi kujizulu wadhifa huo.
  Lakini katika mahubiri yake ya jana, Padri Zengo alisema, dawa ya viongozi walioshindwa kutumiza wajibu wa kuwalinda raia na mali zao, kutokana na kuendelea kushamiri kwa ujambazi, hawapaswi kuchaguliwa ikiwa watashindwa kujiuzulu wenyewe.

  “Jeshi la polisi liko wapi, polisi mpo wapi mpaka tunapoteza kondoo wetu kwa ujambazi, inaonekana Kova kazi imekuwa ngumu kwake,” alisema.
  Suleiman Kova ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam aliyechukua nafasi hiyo baada ya kustaafu kwa mtangulizi wake, Alfred Tibaigana.
  Padri Zengo alisema binafsi ameshiriki kuwazika waumini watatu wa kanisa hilo waliokufa kutokana na kuuawa na majambazi, hivyo akaiasa jamii kupaza sauti zao ili waliopo madarakani wasikie kilio cha kuchoshwa na uhalifu huo.
  “Tupaze sauti zetu, wasituone tupo kama vile hatujui kinachoendelea, maana tukinyamaza ipo siku mtakuta na sisi mapadri wenu tumeingiliwa na majambazi,” alisema.
  Alitoa mfano wa tukio la kuvamiwa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtoni, ambapo majambazi walipora tabernakul ambayo ni mfano wa nyumba ya kuhifadhi sakramenti takatifu.
  Padri huyo akionekana kukerwa na ujambazi, alisema raia wasiokuwa na hatia wanavamiwa majumbani, huku wenye magari wakishushwa na kutakiwa kuwaelekeza majambazi mahali watakapopata wanachokihitaji.
  “Majambazi wamefikia hatua sasa wanacheza wanavyotaka…tuwaambie kazi imewashinda hivyo mjipange upya ama vinginevyo mjiuzulu,” alisema.
  Padri Zengo alisema inashangaza kuona wakati jamii ikikabiliwa na matatizo mbalimbali, yakiwemo yanayotokana na ujangili, bado kuna watu wanaokubali kuhongwa chakula kama pilau ama khanga na pombe za kienyeji, ili kuwachagua viongozi wasiofaa.
  “Wakati huu si wa kusubiri pilau na kuvishwa kofia na khanga, tujiandae kuchagua viongozi wanaotufaa,” alisema.


  Hivi karibuni majambazi waliua watu wawili, wote wafanyabiashara katika eneo la Kimara, Temboni baada ya kuwavamia wakirejea nyumbani kwao usiku katika tukio lililotokea usiku mmoja. Kadhalika vitendo kadhaa vya ujambazi vimeripotiwa eneo hilo, huku wananchi wakiishi kwa hofu kubwa.


  Kamanda Kova akizungumzia hali hiyo hivi karibuni alisema wananchi wanapaswa kushirikiana na polisi katika kampuni ya polisi jamii kwa kuanzisha vikundi vya ulinzi katika mitaa yao na polisi watashirikiana nao na kuwapatia masaada unaostahili.


  Kamanda Kova alisema kwa sasa ujambazi umekimbia katikati ya Jiji na unaendelea maeneo ya pembezoni, hata hivyo alisema wamejipanga kukabiliana na changamoto hiyo.


  Wakati huo huo, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarpo Kardinali Pengo, atakutana na mapadri wote wa jimbo hilo, katika misa na mkutano utakaofanyika parokiani Mavurunza.


  Kwa mujibu wa matangazo yaliyotolewa kanisani hapo jana, Kardinali Pengo atakutana na mapadri hao Alhamisi ijayo na siku inayofuata, kutafanyika mkutano wa mapadri kutoka Dekania ya Kibaha.  CHANZO: NIPASHE

  Though the church is partly to blame by saying that the president ni chaguo la mungu, but now at least you are showing us that you were wrong.

  The writting is on the wall, Kova kachaguliwa na raisi, IGP kachaguliwa na raisi Waziri kateuliwa na rais na wote wamekataa katakata kujiuzulu, na watu bado wanakufa. Njia pekee iliyobaki ni kutumia njia aliyoisema paroko kuwa ikifika oktoba 31 tuwanyimena kuwafuta kazi. Ona red and bold hapo juu.

  Njia pekee ya kuwanyima kazi ni kutochagua CCM ni rahisi kama kusukuma mlevi.

  Paroko naomba urudie tena na tena kanisani na kuyaambia makanisa mengine yaseme.
   
 2. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hawa ndio viongozi tunaowataka. Viongozi walio na uwezo wa kukemea uoza hadharani. Kwakweli hali ya kimara na maeneo mengine inatisha. Almost kila ijumaa saa mbili usiku kunatukio linatokea na wakuu wetu wa usalama wanadai wanawafahamu hawa watu na kuawataka wajitokeze. Haya yote yanaendelea wakati bado tunaendelea kupoteza wapendwa wetu na nguvu kazi ya taifa na kuendelea kuishi kwa hofu.

  Tutavumilia mpaka lini hali hii? tutawavumilia mpaka lini watawala hawa wasio na nia ya kuwasaidia wananchi? Wakati umefika na wakati ni huu..Tusimame kwa pamoja na tupaze sauti tupaze sauti kwa sanduku la kura tuwawajibishe maana wao wameshindwa kuwajibika.

  Oct 31 Jumepili 2010 sote tujitokeze kupiga kura, na kura yetu kwa namna yeyote ni NO KA CCM
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mwambie kila aliye jirani yako kuwa mauaji hayo ni matokeo ya ugawaji mbaya wa rasilimali za taifa, kama tugewana vizuri kusingekuwa na watu wasio na ajira hivyo ujambazi usingekuwepo.

  Kinyume cha hiyo ujambazi umeshamiri na watu wanakufa ovyo polisi ambao ni tegemeola wananchi kama ambavyo crown zao zimeandikwa usalama wa raia hawafanyi hivyo badala yake wamekuwa usalama wa viongozi ambao sisi tumewachagua, viongozi hao wanaona na hawachukui hatua yoyote kukabili haya mambo.

  Hivyo viongozi wetu wanakubaliana na yanayotutokea, hivyo dawa ni kuwakataa tu hakuna jingine. Tuseme, tuimbe tukariri.
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwa niliyoyaona jana kwenye luninga basi tusahau ili la kuleta mabadiliko kwa njia ya kura. Wasomi tunaowategemea kuwa ndio cheche za mabadiliko haya tunayo yasema kila siku ndi wanakuwa wa kwanza kujipendekeza kiasi hiki, eti wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma wameandamana na kuchangishana pesa hadi zikafika 1.2 million na wamempa JK ili aweze kuchukua tena fomu za kugombea urahisi oooooh sorry Urais,, nae kuthibitisha kuwa tarehe 21-June (not sure) atakwenda kuchukua fomu, maana yake JK atarudi tena magogoni! tutashuhudia sana tu ndigu zetu wakiuwawa sio tu na majambazi, ajali na polisi wenyewe, tena hawa siku hizi wanashindana na majambazi kuuwa wananchi!
   
 5. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #5
  Jun 14, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakiambiwa ukweli wanaruka na bado sana.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hii ndio inaitwa dhiki kuu. Mwananchi wa kawaida anapokea mapigo kutoka kila angle. Hamna mtetezi.
   
Loading...