Kanisa, msikiti, mpagani, asiyeamini uwepo wa Mungu, wataalamu wa jadi wako wapi kuombea mvua?

masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,738
2,281
Zama kweli zimebadilika,miaka ya nyuma pale ambapo kulikuwa na majanga ya mvua hasa mvua ya kuzidi sana na maporoko.taasisi zote za kiimani zilikuwa zikihamasisha kuombea mvua ya amani.Hata taifa kupitia kipitia Rais wa nchi alikuwa akihamasisha kila MTU kuomba juu ya mvua ya amani.

lakini pia hata pale mvua zilipokuwa zinachelewa kama hivi, bado taasisi hizo hizo watu waliomba na kufunga kwa ajiri ya mvua.kwa wale wangaga walikuwa wakiuliza mizimu yao na ya sehemu husika na ikibidi kutoa kafara maalumu kwa ajiri ya mvua.

Zama kweli zimebadilika na sijui ni kwa nini,kwa sababu hali iko wazi kabisa kuwa kipindi hiki tuna ukame.kwa Tanzania sio rahisi hadi mwezi wa kwanza bado hata maharage hayajaweka maua,mahindi hayajaanza kubeba,zaidi ya robo tatu ya mashamba ya watu hayajalimwa bado.

Malisho ya wanyama wala majani yalikuwa ni mengi sana.. Majani sehemu kubwa ya Tanzania yalikuwa ni kijani, kwa wale wa kijijini.mchicha pori na mgagani ulikuwa ni wa kuchuma bure tena ni mwingi.lakini pamoja na yote hayo kuwa tofauti lakini sijasikia watu wakihamasisha wamuombe Mungu kwa ajiri ya kuleta mvua kwa wakati. Sijui tatizo ni nini.???

Zama zimebadilika kwani nakumbuka kwenye uchaguzi watu tuliomba sana juu ya kupata Rais lakini kwenye mvua sijasikia
Pia pongezi kwa wote wanao omba binafsi kwa ajiri ya mvua na hali ya taifa letu..kwani hata mtu mmoja akisimama vizuri anaweza kiliokoa taifa na Mungu akubaliki sana bila kujari dini au imani yako..
 
wanaomba maisha bora wanapata ukata, wanaomba mafisadi wafungwe, wanaambiwa kufukua makaburi haiwezekani,
wameomba misaada kwa wahanga Bukoba, wamepewa maneno magumu! waliomba elimu ya bure wamepewa elimubure
 
Zamani kulikuwa na viongozi wa dini sasa hivi viongozi wa dini ni wachache mno wengi ni wafanyakazi wa dini kama walivyowafanyakazi wengine.
 
Laana ya kundi fulani kudai ndo wenye miliki ya nchi wakati walishindwa uchaguzi.
Na matusi,udhalilishaji umezidi.
Kuna miungu na wamejitaja hadharani,mara sijaribiwi wewe!!
Anajaribiwa Mungu sembuse wewe!!
Ndo maana hali ipo hivi
Lema lema lema.
Ben8 Ben8
 
Mkuu nimeanzisha huu Uzi ila sikufikiria kumaweza kuwa na hoja za hivk...kwa hiyo huenda ile faru kuthaminiwa kuliko mtu inaweza kuwa ni sababu za haya yote kutokea?
 
Siamini hadi karne ya 21 bado kuna masalia ya watu wenye mitazamo kama yako kuhusu hali ya hewa kuhusishwa na matambiko.

Hapo ulipo bila shaka kamani nyumbani basi kuna mfuko wa mkaa jikoni si ndio.......kuna mbao zimeezeka paa la nyumba yenu .....na mbao zilitumika kuchongea frame za dirisha zote na pia hata milango........basi kama hivi vitu wewe unavitumia .....hayo matambiko hata kama yatafanywa inchi nzima nakuhakikishia hautaona hata tone la mvua.

Nina hisi walakini kusema hauna elimu maana kuhusiana na elimu usingekuwa na uwezo wa kutype hapa..........

Ila kwa level yako unapaswa kujua miti ndio chanzo kikuu cha kuleta mvua katika ardhi mahala kokote duniani. Leo hii unaambiwa kiwango cha ukuaji wa hali ya majangwa kutokana na uharibifu wa mazingira asili unaotokana na shughuli za kibinadamu juu ya ardhi unakuwa kila uchao kwa kasi ya ajabu.

Tambiko sahihi juu ya hii inshu ya ukosefu wa mvua ni wewe kutosapoti matumizi ya mkaa na madirisha ya mbao kwa gharama yeyote...........au vitu vyote ambavyo hutengenezwa na miti. Hii itasaidia kupunguza mahitaji ya miti ambayo yanakuwa kila uchao......

Hata tembo wanauwawa na kuisha kijinga kwasababu ya uhitaji wa pembe zao ambazo hata wao hawajui ni kwanini zinawafanya kuwindwa kwa chuki hivyo .

Tukiendelea hivi miaka 50 tanzania itakuwa ni jangwa kama vile uarabuni.
 
Suala la mvua ni suala la kisayansi na kamwe si la kishirikina namna hiyo! Hakuna maombi yanayoweza kuleta mvua hata kama anayeomba ni yesu au mtume.
 
Ni kweli zama zimebadilika. Saaa hivi watu sio wajinga kama zamani. Kila mtu anajua mvua hailetwi kwa maombi au matambiko. Tuwaulize watalamu wa hali ya hewa kwanini mvua hakuna.
 
Siamini hadi karne ya 21 bado kuna masalia ya watu wenye mitazamo kama yako kuhusu hali ya hewa kuhusishwa na matambiko.

Hapo ulipo bila shaka kamani nyumbani basi kuna mfuko wa mkaa jikoni si ndio.......kuna mbao zimeezeka paa la nyumba yenu .....na mbao zilitumika kuchongea frame za dirisha zote na pia hata milango........basi kama hivi vitu wewe unavitumia .....hayo matambiko hata kama yatafanywa inchi nzima nakuhakikishia hautaona hata tone la mvua.

Nina hisi walakini kusema hauna elimu maana kuhusiana na elimu usingekuwa na uwezo wa kutype hapa..........

Ila kwa level yako unapaswa kujua miti ndio chanzo kikuu cha kuleta mvua katika ardhi mahala kokote duniani. Leo hii unaambiwa kiwango cha ukuaji wa hali ya majangwa kutokana na uharibifu wa mazingira asili unaotokana na shughuli za kibinadamu juu ya ardhi unakuwa kila uchao kwa kasi ya ajabu.

Tambiko sahihi juu ya hii inshu ya ukosefu wa mvua ni wewe kutosapoti matumizi ya mkaa na madirisha ya mbao kwa gharama yeyote...........au vitu vyote ambavyo hutengenezwa na miti. Hii itasaidia kupunguza mahitaji ya miti ambayo yanakuwa kila uchao......

Hata tembo wanauwawa na kuisha kijinga kwasababu ya uhitaji wa pembe zao ambazo hata wao hawajui ni kwanini zinawafanya kuwindwa kwa chuki hivyo .

Tukiendelea hivi miaka 50 tanzania itakuwa ni jangwa kama vile uarabuni.
Nakubaliana na Wewe lakini lazima ufahamu kuwa hata miaka ya nyuma mvua zilikosa na huku hali ya hewa ni nzuri. Fahamu kwamba kitu nilichokielezea hapa ni kuwa,mbona zamani tulikuwa tunaamini katika maombi,toba na matambiko Ili hali ya hewa itegemae.naamini kama unakumbukumbu nzuri sio zaidi ya mara moja kwa miaka ya nyuma ulisikia viongozi wa kiimani na kiserekali wakihamasisha kuwa kila MTU aombe kwa ajiri ya utengemao wa hali ya hewa..l
Nashukuru kwa mawazo yako lakini mtazamamo wangu ni kuwa mbona miaka hii mahamasisho hayo hayapo kama zamani. ???
 
Siamini hadi karne ya 21 bado kuna masalia ya watu wenye mitazamo kama yako kuhusu hali ya hewa kuhusishwa na matambiko.

Hapo ulipo bila shaka kamani nyumbani basi kuna mfuko wa mkaa jikoni si ndio.......kuna mbao zimeezeka paa la nyumba yenu .....na mbao zilitumika kuchongea frame za dirisha zote na pia hata milango........basi kama hivi vitu wewe unavitumia .....hayo matambiko hata kama yatafanywa inchi nzima nakuhakikishia hautaona hata tone la mvua.

Nina hisi walakini kusema hauna elimu maana kuhusiana na elimu usingekuwa na uwezo wa kutype hapa..........

Ila kwa level yako unapaswa kujua miti ndio chanzo kikuu cha kuleta mvua katika ardhi mahala kokote duniani. Leo hii unaambiwa kiwango cha ukuaji wa hali ya majangwa kutokana na uharibifu wa mazingira asili unaotokana na shughuli za kibinadamu juu ya ardhi unakuwa kila uchao kwa kasi ya ajabu.

Tambiko sahihi juu ya hii inshu ya ukosefu wa mvua ni wewe kutosapoti matumizi ya mkaa na madirisha ya mbao kwa gharama yeyote...........au vitu vyote ambavyo hutengenezwa na miti. Hii itasaidia kupunguza mahitaji ya miti ambayo yanakuwa kila uchao......

Hata tembo wanauwawa na kuisha kijinga kwasababu ya uhitaji wa pembe zao ambazo hata wao hawajui ni kwanini zinawafanya kuwindwa kwa chuki hivyo .

Tukiendelea hivi miaka 50 tanzania itakuwa ni jangwa kama vile uarabuni.
Maelezo yanayokinza na lengo la mada tajwa
 
Back
Top Bottom