Kanisa lawatosa waumini wengine 17.....

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,549
2,000
Kanisa lawatosa waumini wengine 17


Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga;
Tarehe: 7th December 2010


KANISA Katoliki la Kristu Mfalme mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, limeendelea kuwaadhibu waumini wake inaodai kuwa waliisaliti imani yao katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, baada ya juzi kutangaza kuwasimamisha na kuwafukuza waumini wengine 17 wa Kanisa hilo.

Kufukuzwa kwa waumini hao kuhudhuria Ibada za Misa Takatifu na kufungiwa Sakramenti zote, kunatokana na wenzao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 400 waliopewa adhabu kama hiyo hivi karibuni na kanisa hilo kwa kinachodaiwa kuwa wameisaliti imani ya Kanisa hilo.


Majina hayo yalitangazwa wakati wa ibada ya misa ya kwanza juzi ambapo majina ya waumini hao yalikuwa yamegawanywa kwenye makundi mawili.


Kundi la kwanza ni la waumini ambao hawawezi kusamehewa na Padri yeyote isipokuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Sumbawanga pekee, wakati kundi la pili ni la waumini sita ambao wamevuliwa Ukristo wao ambao hata wakitubu, hawawezi kusamehewa.


Padri aliyekuwa akiendesha misa hiyo ambaye ni Paroko Msaidizi na hakutaka kutaja jina lake huku hata waumini wakiogopa kulitaja, aliyasoma majina hayo rasmi muda mfupi kabla ya kumaliza misa.


Paroko huyo alidai shughuli hiyo ni ya kudumu kwa kuwa Kanisa liko vitani kuhakikisha linakuwa safi na si vinginevyo.


“Nasema hivi kwa kuwa siku hizi hata simu zinarekodi basi kwa wale wanaorekodi haya warekodi ni ruksa, tumepata habari kuwa hata magazeti yameanza kuandika habari hizi, nasema yaendelee tu kwani kanisa linafuata sheria na liko sahihi," alisema Padri huyo.


Hata hivyo, Paroko Msaidizi huyo hakutaja majina ya wahusika wa adhabu hizo mbili, katika uamuzi ambao tayari umezua gumzo kwa watu mbalimbali mjini hapa na katika mikoa mingine nchini.


Wakati huo huo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Charles Kabanga anakusudia kukata rufaa kwa Baba Mtakatifu mjini Rome kupinga kufutwa Ukristo wake hivi karibuni.


Akizungumza na gazeti hili, Kabanga alisema anajiandaa kuuza mali yake asafiri hadi Rome kwenda kuonana na Baba Mtakatifu kupinga kuondolewa Ukristo wake na Paroko wa Kanisa Katoliki, Padri Leonard Teza ambaye ni Paroko wa Kanisa la Familia Takatifu lililopo eneo la Kizwite mjini hapa.


"Kwanza nitaonana na Kadinali Pengo (Muadhama Polycap Kadinali Pengo) na asiponirudishia Ukristo wangu, basi nipo tayari kuuza mali zangu na kufunga safari hadi Rome kukata rufaa kwa Baba Mtakatifu ambaye ndiye kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki Duniani," alisisitiza mwanasiasa huyo.


Alisema, hatua yake hiyo inatokana na adhabu hiyo kali aliyopewa na Paroko wa Kanisa likimtuhumu kutenda makosa makuu matatu ambayo ni sawa na kuisaliti imani ya Kanisa hilo.


Akifafanua, alisema Oktoba 29, mwaka huu, alikabidhiwa barua na Padri Teza ikimtaarifu kuwa amevuliwa Ukristo wake rasmi kuanzia tarehe hiyo.


Alisema anashutumiwa kwanza kumshabikia mgombea ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM, Aeish Hilaly wakati akifahamu wazi kwamba ni Muislamu na alimnadi kwa kutumia dhana ya mafiga matatu ambayo mgombea huyo aliyafananisha Utatu Mtakatifu katika imani ya Kikristo.


Kosa la pili analoshutumiwa Kabanga, ni kukufuru msalaba, kwamba baada ya uchaguzi kumalizika na matokeo kutangazwa ambapo mgombea wa Chadema, Norbert Yamsebo alishindwa, wana CCM walifanya maandamano huku wakiwa wamebeba msalaba kama ishara ya kumzika mgombea huyo wa Chadema.


Tatu, alisema anashutumiwa na Kanisa hilo kwa kutukana mapadri kwamba nao wana mapungufu yao, yakiwemo kuwa na vimada ambao wamewajengea nyumba na pia kuzaa nao.


Anadaiwa pia kuwa alitukana kwamba baadhi ya watoto wa mtaani wanaorandaranda mijini hapa wamezaliwa na baadhi ya mapadri wa Kanisa hilo.


Alisema amekanusha makosa yote hayo mbele ya Padri Teza ambaye alimtaka atubu, lakini alikataa kutubu kwa kuwa hajatenda makosa hayo.


Alisema alimwambia Paroko huyo hata yeye kama angekuwa kwenye nafasi aliyonayo kama Mwenyekiti wa CCM, basi lazima wakati wa uchaguzi, angehubiri kuhusu mafiga matatu kwa kuwa CCM ilikuwa inaamini kuhusu mafiga matatu kuwa lazima achaguliwe rais, mbunge na diwani kutoka CCM na si vinginevyo.
 

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
6,996
2,000
Makosa yake ni:

1.. kumshabikia mgombea ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM, Aeish Hilaly wakati akifahamu wazi kwamba ni Muislamu na alimnadi kwa kutumia dhana ya mafiga matatu ambayo mgombea huyo aliyafananisha Utatu Mtakatifu katika imani ya Kikristo.

2.. Kosa la pili analoshutumiwa Kabanga, ni kukufuru msalaba, kwamba baada ya uchaguzi kumalizika na matokeo kutangazwa ambapo mgombea wa Chadema, Norbert Yamsebo alishindwa, wana CCM walifanya maandamano huku wakiwa wamebeba msalaba kama ishara ya kumzika mgombea huyo wa Chadema.


3.. alisema anashutumiwa na Kanisa hilo kwa kutukana mapadri kwamba nao wana mapungufu yao, yakiwemo kuwa na vimada ambao wamewajengea nyumba na pia kuzaa nao.


4.. alitukana kwamba baadhi ya watoto wa mtaani wanaorandaranda mijini hapa wamezaliwa na baadhi ya mapadri wa Kanisa hilo.


 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
214,549
2,000
Kanisa Katoliki lafafanua waliotengwa


Na Edmund Mihale

KANISA Katoliki Jimbo la Sumbawanga limezungumzia sakata la kusimamishwa kwa baadhi ya waumini wa jimbo hilo na kudai kuwa adhabu hiyo ni kawaida kuchukuliwa kwa waumini wanaokwenda kinyume na imani ya kanisa hilo.Hatua hiyo ya kanisa hilo
imekuja baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa limesimamisha waumini 400 ambao ni wanachama wa Chama Cha Mpinduzi (CCM).

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Paroko wa Kanisa Kuu la Sumbawanga, Padri Deogratius Simemba alisema wanachama waliosimamishwa si 400 kama ilivyoripotiwa bali hawazidi na hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu ya kwenda kinyume na maelekezo ya kanisa

Alisema kitendo cha kusimamishwa kwa waumini hao ni cha kawaida katika kanisa hilo katika kusimamia nidhamu kwa waumini wake na si mambo ya kisiasa wala kukichukia chama fulani.

"Kanisa siku zote limekuwa likisisitiza waumini wake kushiriki katika siasa, lakini kwa uadilifu na iwapo litaona muumini anakwenda kinyume na maelekezo ya kanisa humchukulia hatua kwa mujibu wa sheria za kanisa," alisema Padre Simemba.

Alisema wanachama hao wamesimamishwa kutoka na kuvunja sheria za kanisa kwa kuukufuru utatu mtakatifu yaani Mungu Mwana wa Mungu Baba na Roho Mtakatifu .

Gazeti moja la kila siku liliripoti jana akuwa utatu huo mtakatifu ulifananishwa na 'mafiga matatu ya CCM, ambapo mgombea urais, Rais Kikwete alifananishwa na Mungu, Mgombea ubunge alifananishwa na Yesu Kristo na wagombea udiwani wakalinganishwa na Roho Mtakatifu.

Padri alisema kosa lingine la waumini ni kushangilia ushindi wa mbunge wa jimbo kwa kutumia msalaba jambo ambalo ni kosa kutoka na sheria na kanuni za kanisa hilo.

Alisema kuwa kanisa limekuwa likitoa adhabu kwa waumini wake wanaofanya makosa mbalimbali, yakiwemo kushiriki katika imani za kishirikina na wote wanaokwenda kinyume na sheria za kainisa.

Naye msemaji wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Modestus Katonto alisema watu wanataka kulichukulia suala hilo kisiasa, wakati ni la kiimani.Alisema anavyofahamu yeye watu waliotengwa na kanisa hilo hawazidi 10, miongoni mwao wakiwamo wanane waliokufuru msalaba ambao walikuwa wakikimbia na msalaba kushangilia ushindi wa mgombea wa CCM huku wakisema kanisa limezikwa na msalaba.

"Wengine hawajatengwa na kanisa, lakini wamepewa barua kwenda kuomba msamaha katika ngazi ya Jumuiya, wakisamehewa na jumuiya wataendelea kushiriki kama kawaida," alisema.

 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,212
2,000
This is too much now...Ni karibia post ya 5, talking of the same content...boring!!:redfaces:
Tuweke vitu vya tofauti jamani!
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,817
0
Makosa yake ni:

1.. kumshabikia mgombea ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM, Aeish Hilaly wakati akifahamu wazi kwamba ni Muislamu na alimnadi kwa kutumia dhana ya mafiga matatu ambayo mgombea huyo aliyafananisha Utatu Mtakatifu katika imani ya Kikristo.Baba Enock

Hapo kwenye Red kaa umemsingizia Padri hivi, hawezi kusema kuwa hilo ni kosa.
 

Chupaku

JF-Expert Member
Oct 15, 2008
1,091
1,500
Baba Enock

Hapo kwenye Red kaa umemsingizia Padri hivi, hawezi kusema kuwa hilo ni kosa.Baba Enock anaripoti vya magazetini, hajakosea. KUna watu wanataka jambo hili lionekane ni la kisiasa na kidini. Hapo hakuna cha kufukuzwa kwa sababu ya kumkampenia muislamu bali kuenda kinyume na imani. Jamani tuache haya mambo ya udini kuyakuza bila sababu hayapo ila watu ndio wanayavalia njuga, wanaboa sana aisee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom