mulwanaka
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 5,262
- 12,835
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini leo limeweka maazimio ya hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya korona kwa waumini wa kanisa hilo na jamii kwa ujumla.
Uamuzi huo umetolewa na Halmashauri kuu ya Dayosisi hiyo na kutiwa saini na Askofu wa Dayosisi hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Kanisa Rev.Dr.Frederick Shoo (PhD), umeelekezwa kwa Sharika zote za Dayosisi hiyo na utaanza kutekelezwa kuanzia leo, April 05 mwaka 2020.
Baadhi ya maazimio hayo ni pamoja na;
1. Ibada ziwe fupi (zisizidi dakika 45).
_
2. Waumini wakiwa ibadani wahakikishe wamekaa umbali wa mita 1 kati ya muumini mmoja na mwingine.
3. Kuwe na ibada mbili au tatu kwa siku za jumapili ili kuzuia mkusanyiko mkubwa wa watu kwenye ibada moja.
4. Kabla na baada ya ibada viti, meza na vipaza sauti visafishwe kwa dawa.
5. Wazee wa zaidi ya miaka 70 na wagonjwa wapate ushauri wa wataalamu wa afya kabla ya kuamua kushiriki ibada.
6. Ibada za jumuiya zifanyike katika jumuiya ndogondogo za nyumba 3 hadi 4 na si kwa mtaa mzima kama ilivyokua awali.
7. Mtu yeyote mwenye dalili za kikohozi, mafua au kichwa kuuma amuone kwanza daktari kabla ya kushiriki ibada.
8. Sharika zote ziwe na ndoo ya maji safi na sabuni ambapo waumini watanawa mikono kabla ya kuingia ibadani.
9. Ibada za jumuiya zifanyike nje ya nyumba, mahali penye hewa ya kutosha (watu wasijifungie ndani).
_
10. Kila nyumba itakayoandaa ibada ya jumuiya ihakikishe washarika wamenawa mikono kwa maji safi na sabuni.
11. Ibada za ndoa na ibada za mazishi zihudhuriwe na watu wachache tu hususani wanafamilia na majirani.
12. Kanisa linashauri pasiwepo na sherehe za harusi wala sendoff. Na kama italazimu basi zihudhuriwe na watu wachache sana (jamaa wa karibu) na mazingira ya ukumbi yaandaliwe kwa kufuata kanuni za afya.
13. Hakutakuwa na kushikana mikono wakati wa ibada au wakati wa kushiriki neema (baada ya ibada).
_
14. Hospitali, Vituo vya afya na Zahanati zinazomilikiwa na KKKT Dayosisi ya kaskazini zifuate maagizo yanayotolewa na serikali juu ya kujikinga na kudhibiti virusi vya Corona.
15. Watumishi wa Dayosisi ambao si wa sekta ya Afya wameshauriwa kuchukua likizo kwa kupokezana.!
C&p