Kanisa la Askofu Charles Gadi, lamuandikia Rais Samia ujumbe mzito

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,496
51,090
GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY
BISHOP DR. CHARLES GADI
PRESS RELEASE (May 12, 2021)

Ndugu Waandishi, salamu – naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa kuja kunisikiliza, na pia niwapongeze kwa jitihada zenu za kuelimisha jamii na taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutuhabarisha matukio mbali mbali yanayotukia katika Taifa na jamii yetu
Awali ya yote napenda kumpongeza tena Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha uongozi bora, kuleta furaha kwa wananchi na kuendelea kurekebisha mambo yaliyokuwa Kero kwa wananchi kwa ujumla.

Tunaendelea kumwombea Mungu ili aweze kufanikiwa kila alifanyalo kwani hadi sasa ametuonyesha mwanga mzuri wa mwelekeo wa Taifa letu katika Awamu hii ya Sita. Aidha nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa safari aliyoifanya Kenya na kwa kulihutubia Bunge la Kenya pamoja na maongezi aliyofanya na mwenyeji wake, mheshimiwa Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya watu wa Kenya.

Ziara yake imerudisha uhusiano mzuri wa kibiashara na kijamii kati ya nchi hizi mbili na tayari tumeanza kuona matokeo yake, ikiwa ni pamoja na kuruhusu mahindi yaliyokuwa yamekwama mipakani kuanza kuvuka kuingia nchini Kenya.

Vile vile tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa maagizo ya kupunguza urasimu kwenye maswala ya ardhi hususan kwa wawekezaji, na hili tumelishuhudia katika hotuba ya waziri wa Ardhi Mheshimiwa Lukuvi alipokuwa anagawa viwanja vya uwekezaji wa viwanda hivi karibuni. Na hii inadhihirisha wazi kwamba urasimu na ucheleweshwaji wa kupewa maeneo ya ardhi utakoma katika awamu ya hii ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan na hivyo kuharakisha maendeleo yatokanayo na uwekezaji.

Na pia nimshukuru na kumpongeza Zaidi kwa hatua ya kuteua majaji wa mahakama ya rufaa 7 na majaji wa mahakama kuu 21 ndani ya mwezi huu wa Mei 2021. Jambo hili ni jema mno kwani litaharakisha utolewaji wa haki katika kesi mbali mbali zilizolundikana mahakamani kwa siku nyingi, na ni jambo la kumpendeza Mungu kama mashauri yataamuliwa haraka na haki kupatikana kwa mujibu wa sheria. Kwa hili mheshimiwa Rais anastahili pongezi kubwa na amejibu kilio cha wananchi wengi.

Vile vile tunapenda kumpongeza na kumshukuru mheshimiwa Rais kwa kauli aliyotoa alipokuwa akiongea na wazee wa Dar es Salaam, kwa kukubali kuteua watu wote wenye uwezo kwenye nafasi mbali mbali bila kujali vyama au itikadi zao. Hii ni kauli njema yenye nia ya kujenga umoja wa kitaifa na yenye uzalendo wa hali ya juu. Mheshimiwa Rais anastahili pongezi kubwa kwa hili.

Ndugu waandishi
Pamoja na pongezi hizo kwa kazi njema anazozifanya Mhe. Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Naomba nianze kwa kumshauri na kumwomba Rais kuendelea kutupia macho mambo kadhaa kama ifuatavyo.

Nikianza na swala la Wanadiaspora, tunamwomba aendelee kulitupia macho kwani linahitaji msaada wake haswa. Tunashukuru sana kwa kuwa ameanza kuligusia, na tunamwomba aendelee kulishughulikia hadi lifikie muafaka mzuri. Napenda kukumbusha wanajamii na Taifa kwa ujumla kwamba Mungu amekataza kumwaga damu ya mtu, direct au indirect katika Neno lake.

Kwa kusema hivi ninataka kulihusisha na swala la Wanadiaspora, nikimaanisha kwamba mtu anapofanya kazi kwa mwezi mzima akalipwa mshahara, hiyo ni damu yake aliyoipoteza kwa siku thelathini alizopitia akifanya kazi ngumu na kwa bidii.
Sasa mtu kama huyo anapokuja kununua ardhi nchini halafu akanyang’anywa hiyo ardhi au nyumba ambayo amenunua kwa hela zilizotokana na mishahara yake kwa kisingizio cha kutokuwa na uraia, ingawa ni mzawa wa nchi hii, hiyo ni sawa na umwagaji damu (usio rasmi) dhidi ya mtu kama huyo.

Ndugu waandishi:
Nitoe historia fupi ya nchi yetu katika jitihada zake za kujiletea maendeleo na kuepukana na ubepari na unyonyaji tangu tulipopata uhuru toka kwa mkoloni:
- Mwaka 1967 wakati wa Azimio la Arusha, kulikuwa na utaifishaji wa mali za watu haswa majumba, mashamba na viwanda ili ziwe mali za uma na viweze kuendeshwa na Serikali kupitia siasa ya Ujamaa na kujitegemea.

- Wakati huo huo, ili kuweze kuanzisha vijiji vya ujamaa, ilibidi serikali ihamishe baadhi ya watu kwa nguvu, waliokuwa wakiishi maporini au kwenye vijiji visivyo rasmi, jambo ambalo lilihusisha upotevu wa baadhi ya mali ya wananchi na hata wengine walikufa.

- Mwaka 1977 wakati wa Anguko la Jumuiya ya Afrika Mashariki, serikali yetu kutokana na hali ngumu ya uchumi iliyokuwa inapitia wakati huo, haikuweza kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wa Jumuiya hiyo kama zilivyofanya serikali zingine, kwa hiyo wastaafu wengi walikufa bila kulipwa, ingawa baadaye Serikali ya Awamu ya tatu chini ya Mheshimiwa Mkapa ilijitahidi kuwalipa wastaafu hao na kuwafuta machozi.

- Vivyo hivyo wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili, mheshimiwa Mwinyi alijitahidi kurudisha baadhi ya nyumba na mali zilizotaifishwa (wakati wa utekelezaji wa Azimio la Arusha) kwa baadhi ya watu, na tunampongeza sana kwa hatua hiyo. Wote tunajua kwamba nia ya serikali ya Awamu ya Kwanza ilikuwa njema, yenye nia ya kuondoa ubepari na unyonyaji na kujenga jamii ya kijamaa ambapo mali zote humilikiwa na umma na kuendeshwa na serikali.

Lakini kwa kufanya hivyo katika zoezi hilo kuna watu wengi waliodhulumika, jambo ambalo halina tofauti na umwagaji wa damu usio rasmi, kwani wengi walichanganyikiwa, walikufa kwa presha na msongo wa mawazo, huku tukijua baadhi walikuwa ni wawekezaji waliotoka kwenye nchi zao ili kuwekeza kwenye nchi hii chini ya iliyokuwa serikali ya kikoloni. Kwa hiyo walijikuta wakiwa maskini kwa ghafla huku wakiwa hawana pa kukimbilia.

Ndugu waandishi
Wakati wa serikali ya awamu ya Nne, Aliyekuwa rais wakati huo, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alizunguka mataifa mbali mbali huku akikutana na watanzania wanaoishi humo wanaojulikana kama Wanadiaspora, akawashauri na kuwashawishi warudi kuwekeza kwenye nchi yao.

Wengi waliitika wito huo baada ya kuona umetoka kwa Rais wa nchi na hivyo kutumia mishahara na mikopo mbali mbali kuja nchini kuwekeza, kwa njia ya mahoteli, biashara majumba na mashamba, huku wakiamini kuwa mali zao zitakuwa salama.
Lakini ghafla baada ya kuja kuwekeza wakaambiwa kuwa mali zao zinarudi serikalini kwa sababu wao si raia wa nchi hii, kwa sababu walishachukua uraia wa nchi nyingine ili waweze kufanya kazi huko kwa uhuru.

Kumbuka hawa watu walikuwa wamemwamini Rais wa nchi kwa hiyo hawakujibakizia akiba bali walikuja kujenga nyumba za kustaafia na miradi ya kumalizia muda wao baada ya kustaafu. Sasa wengine walipopata tangazo hilo la kutaifishwa kwa mali zao, walijitahidi kuzimilikisha mali hizo kwa ndugu jamaa na marafiki ili kusudi zisalimike – jambo hili ndilo tulilosema hapo juu ni sawa na umwagaji damu usio rasmi.
Ndugu waandishi,

Pia nyumba nyingi za watu waliopisha upanuzi wa barabara ya Ubungo hadi Kibaha zilivunjwa, ilhali wengi walikuwa na hati rasmi, zikiwemo nyumba za ibada mfano makanisa na misikiti, nyumba za watumishi wa Mungu, maaskofu na mashehe, wanajeshi wastaafu na raia wengine pasipo malipo yoyote hata kifuta machozi tu.

Hatukatai kuwepo kwa maendeleo lakini maendeleo hayo yanapoambatana na kukandamiza haki za wamiliki wa ardhi, nyumba na viwanja, ni sawa na umwagaji damu usio rasmi, kwani baadhi walikuwa wameshastaafu, hawana pa kwenda, na hivyo kupelekea kufa na presha, msongo wa mawazo na wengine kuchanganyikiwa. Kulingana na Neno la Mungu – Biblia, hapakuwa na haki kwa wengi wao.

Ni kweli maendeleo tunayaona lakini taifa haliwezi kutoboza kiuchumi na kijamii kwa sababu ya kutowatendea haki raia wake, ambapo ni sawa na umwagaji damu huo usio rasmi.

Neno la Mungu katika kitabu cha Yeremia 9:24 linasema, “bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana,” Vile vile Mungu anaendelea kusema katika kitabu cha Nabii Yeremia, 17:11 “Kama kware akusanyaye makinda asiyoyazaa, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya siku zake zitaachana naye, . . . .”

Maneno hayo hapo juu yanamaanisha kwamba mali zinazopatikana isivyo haki na dhuluma huwa zinayeyuka wakati wa kufanikiwa kwake.

Ndugu waandishi
Tunajua matatizo haya Mheshimiwa Rais ameyakuta na ameyarithi, hivyo tunamuomba na ikimpendeza Mheshimiwa Rais wa awamu ya Tano, Samia Suluhu Hassan ahakikishe kwamba katika kipindi chake cha utawala anatengeneza mfumo au utaratibu mzuri wa kushughulika na maswala ya umilikaji wa Ardhi, nyumba, mashamba na viwanja kwa wanadiaspora na watanzania kwa ujumla.

Kwa mfano, katika swala la Diaspora, watanzania wawili wanaotoka UK, mmoja mzanzibari na mmoja ni Mtanzania bara, na ambao wana passport za UK, wanaposafiri kurudi nchini, huyu wa Zanzibar akifika Zanzibar Airport anapokelewa kwa heshima zote kama mtu anayeleta baraka na neema kwenye nchi yake kwa kile alichochuma huko nje, huku akiwa Mzaliwa wa Zanzibar. Tena anapata huduma ya first class tofauti na raia wengine.

Lakini huyu wa Tanzania Bara anapokelewa kama mgeni, msaliti wa uraia na uzalendo, na asiyekuwa na haki ya kumiliki chochote ndani ya nchi hii ambayo alizaliwa.


Nichukue nafasi hii kulipongeza sana Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa kutunga kanuni zinazowalinda na kuwasaidia Wazanzibari wanaoishi nje na ambao wamebadili uraia kuweza kurudi na kuendelea kufaidi matunda ya kazi zao ndani ya nchi yao.

Pia baraza hili hili limetunga kanuni inayomwezesha raia yeyote wa nchi yoyote anayetaka kuja kula pensheni yake Zanzibar, aweze kufanya hivyo alimradi ananunua nyumba au kuwekeza miradi itakayomsaidia kuishi akiwa anamalizia maisha yake. Hili ni jambo la kustahili pongezi kubwa kwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, na ni mfano wa kuigwa na wabunge wa bara.

Nimewahi kwenda Dubai , Serikali ya Dubai inampokea mwekezaji yeyote na kumpa second-class citizenship ili aweze kufanya shughuli zake kwa uhuru. Hili ni jambo linalopaswa kuigwa kwani wote ni mashuhuda wa utajiri, maendeleo na mafanikio ya kiuchumi ya Serikali ya Dubai kutokana na sera hiyo njema.

Ndugu waandishi, katika hili tunamwomba tena sana Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan awasaidie watu (wanadiaspora) walioahidiwa na Mheshimiwa Kikwete kurejeshewa majumba yao na ardhi zao, maana waliwekeza ili waje kumalizia kula pensheni zao ndani ya nchi waliyozaliwa. Badala yake wengi wamejikuta wanaanza moja kwani akiba yao yote waliyojiwekea wameiwekeza halafu wanakosa uhalali wa kumiliki na kutumia uwekezaji wao. Wengi waliotaifishwa nyumba na ardhi zao wanalia kwa sababu ya kutokuwa raia wa Tanzania, ingawa ni wazawa pamoja na yote tunamwomba Mhe. Rais awaonee huruma Diaspora wote na kurejeshwa kundini kwani hakuna asiyefanya kosa.

SWALA LA BIASHARA
Ndugu waandishi,
Katika swala la biashara na majirani zetu haswa kutoka Congo kuna haja ya Mheshimiwa Rais kulitupia macho ili kuwezesha bandari yetu kutumika kwa ukamilifu na kuliingizia Taifa mapato makubwa. Kwa sasa Zaidi ya malori elfu tatu (3000) yanatoka na kuingia Lubumbashi – Kongo kwa siku moja kupeleka na kuchukua mizigo bandari ya Durban Afrika Kusini, ambapo ni Zaidi ya kilometa 5000 kutoka Lubumbashi, ilhali umbali kutoka Lubumbashi hadi Dar ni kama 2500 tu!!.

Sababu ni kwamba sheria na taratibu za nchi yetu zinazuia malori yenye uzito na vipimo/viwango (caliber) kama za malori yanayoenda Durban ambapo yakipita kwetu yatazuiliwa ama kwa ajili ya uzito au upana na hivyo kuwekwa kwenye kundi la wide load transit. Nimewahi kusafiri kwenda Lumbumbashi, nikakutana na Gavana wa Lubumbashi, na pia Meya wa Lumbumbashi, na Senetor wa Lumbumbashi, nikafanya nao mazungumzo kadhaa. Pia nilikutana chama cha wafanyabiashara wa usafirishaji wa Lumbumbashi, na katika mambo waliyolalamikia ni kwamba wangependa sana kufanya biashara au kupitisha mizigo yao Tanzania, ambapo ni karibu na gharama za usafirishaji ni nafuu, lakini tatizo la Tanzania kila mtu ni bwana mkubwa. Hakuna mtu wanaweza kujadiliana naye na akatatua (solve) matatizo yao moja kwa moja.

Kwa mantiki hiyo tunamshauri Rais wetu afanye ziara Kinshasa na Lubumbashi au atume ujumbe mzito kwenda kufanya mazungumzo na wasafirishaji hao wa bidhaa ili kuweza kutatua changamoto hizo na hivyo kuleta biashara katika nchi yetu na matumizi ya bandari yetu yaongezeke.
Kwa mfano, Bwana mkubwa mmoja mtanzania (sitamtaja) anamiliki Zaidi ya malori 3000 yanayofanya safari kati ya Lubumbashi na Durban.

Kwa kufanya hivyo ananeemesha nchi za Zambia, Botswana,Zimbabwe na Africa Kusini yanakopitia malori hayo kwa kulipa ushuru huko wa barabara zao, wakati hizo fedha zingeweza kuinufaisha nchi yetu. Mtu kama huyo utalinganishaje uzalendo wake na ule wa wanadiaspora wanaotamani kuja kuwekeza hapa nchini kwa fedha zao walizochuma nchi za kigeni? Maana fedha watakazowekeza hapa zitaongeza mzunguko wa fedha na biashara na kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla kutokana na kodi wanazolipa.
Vile vile nashauri benki zetu kubwa mfano CRDB iende kufungua tawi kule Lubumbashi ili kurahisisha money transfer kwa wafanyabiashara na wasafirishaji kutoka Congo.

Hii itaongeza fursa za Biashara na maendeleo kwa nchi yetu.
Pia Mheshimiwa Rais wetu anaweza kulishauri bunge letu kuwaiga Baraza la Mapinduzi Zanzibar ili kuwezesha wanadiaspora na wawekezaji wengine kuingia na kufanya biashara kwa urahisi hapa nchini. Watu wanasema watanzania hatupendani kwa kuangalia jinsi swala la Wanadiaspora linavyoshughulikiwa. Kwa mfano kwa nini kama tuna watanzania wanaoishi nje ya nchi na wana uwezo na uzoefu wa kuwekeza, wasipewe kipaumbele kabla ya wageni kutoka nchi za nje?

Ni kwa mantiki hiyo tunamwomba mama Samia Suluhu Hassan alitupie tena macho swala la uraia pacha kwani ndiyo hasa mzizi wa matatizo ya wanadiaspora.
Mwisho kwa unyenyekevu tunamwomba tena mheshimiwa Rais alitupie macho swala hili la Ardhi mfano ni mradi wa majumba ya Kawe pale Tanganyika Packers. Kuna wananchi waliokuwa wanaishi hapo ambao walikuwa wafanyakazi walioachwa na kampuni hiyo, lakini mradi huo wa maghorofa ulipoanza waliondolewa kwa nguvu, na sasa mradi huo umekuwa kama white elephant, yaani tembo mweupe, hauendelei tena.

Ni kwa sababu kuna kilio cha wananchi hao walioondolewa bila malipo au mafao huo nao Biblia inautafsili ni umwagaji wa damu usio rasmi.

Tukumbuke kuwa moja wapo ya matatizo ya Waisraeli na Mungu wao, ni kwa sababu walivunja sheria zake zihusuzo ardhi. Mfano aliwaambia kuwa kila mwaka wa saba wasiilime ardhi bali waiache ipumzike lakini wakakaidi na hivyo kukosa baraka za Mungu wao, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa na kuhamishiwa Babeli na mataifa mengine walikoteseka kama wageni na watumwa. Nchi ikikosea kwenye swala la ardhi wananchi wake wanageuka kuwa watumwa.

Tunaamini kwamba Rais wetu ni mama mwenye huruma, na atatupia macho maswala haya yote tuliyomwomba ili nchi yetu isiingie kwenye laana ya maswala ya ardhi au umwagaji damu usio rasmi, hatimaye iweze kutoboza kwenye anga za kiuchumi kitafa na kimataifa, kwa sababu Neno la Mungu linasema, Taifa linalotenda haki litasimama imara na ya kwamba Haki huinua Taifa

Neno la Mungu katika Mithali 14:34 linasema, “Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.”

Naomba nichukue tena nafasi hii kuwashukuru sana kwa kunisikiliza.

ASKOFU DR. CHARLES GADI
GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY
IMG-20210513-WA0048.jpg
IMG-20210513-WA0047.jpg

 
Ana hoja za msingi kubwa mbili nilizoziona

1.Diaspora wenye uraia wa nje kuporwa nyumba na ardhi ingekuwa vizuri akatoa mifano halisi kurahisisha ufuatiliaji awataje kwa majina

2.Kuhusu kufungua malori ya kongo kuja Tanzania badala ya Durban ni hoja nzito serikali iliangalie hilo
 
Hajajitambulisha ni askofu wa kanisa gani, namwona tu amevaa kofia ya Papa sijui ana kibali!!
 
HONGERA KANISA KWA KUTIMIZA WAJIBU WAKO KWA UMA
Namini Mama atathamini ushauri huu na kuufnyia kazi bila kinyongo ama kwa awamu au kwa ahadi
Mungu ni mkuu sana.
 
HONGERA KANISA KWA KUTIMIZA WAJIBU WAKO KWA UMA
Namini Mama atathamini ushauri huu na kuufnyia kazi bila kinyongo ama kwa awamu au kwa ahadi
Mungu ni mkuu sana.
Kanisa ni wanafiki sana,jiwe alifanya kila uonevu ila kanisa lilijikalia kimya kama halipo vile ila akija rais Muislam ndipo huo upuuzi wa makanisa kuanza kutoa waraka huanza.

Nb:Mimi ni mkristo.
 
Back
Top Bottom