Kanisa lamshitaki Mwakipesile kwa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa lamshitaki Mwakipesile kwa JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kidudu Mtu, Jan 28, 2010.

 1. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #1
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MKUU wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), Advocate Nyombi na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya (DC) Leonidas Gama, wameshitakiwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Kanisa la Pentecostal Evangelistic.
  Kanisa hilo limechukua hatua hiyo kwa madai kuwa viongozi hao hawakuhudhuria sherehe za kumshukuru Mungu kwa ajili ya uhusiano mwema wa miaka 15 kati ya Tanzania na Israel zilizofanyika Januari 14-16 mwaka huu mkoani Mbeya.
  Kanisa hilo limewashitaki viongozi hao waandamizi wa serikali kwa kumwandikia barua Rais Kikwete ili awaeleze viongozi hao umuhimu wa kushirikiana na viongozi wa dini katika masuala mbalimbali.
  Barua hiyo ambayo Tanzania Daima imeona nakala yake imeandikwa Januari 19 mwaka huu na kupewa kumbukumbu namba PEC/653/7688 VOL. 1/IS-TZ/010.
  Kichwa cha habari cha barua hiyo kimeandikwa: ‘Kilio cha huzuni kuhusu utendaji kazi wa viongozi wa serikali mkoani Mbeya’ na kwamba viongozi hao walialikwa katika sherehe hizo kwa kupelekewa barua kwa ‘dispatch’ Novemba 14, 2009.
  Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa barua hizo zenye kumbukumbu namba PEC/6537688/VOL.1/IS-TZ/09 walipelekewa viongozi wa mkoa huo na Jiji la Mbeya, akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, Mkuu wa Uhamiaji wa Mkoa wa Mbeya na Mkurugenzi wa jiji hilo, wote hawakuhudhuria wala kutoa sababu zozote.
  “Mheshimwa Rais, tumeona litakuwa jambo la busara kuleta kilio hiki kwako, kama kiongozi wetu wa taifa la Watanzania kwa ufafanuzi wako mzuri utakaotusaidia kushirikiana na viongozi wetu wa serikali, badala ya kunug’unika chini chini.”
  “Mheshimiwa Rais tumeshindwa kuwaelewa viongozi wetu tuwaweke wapi katika ngazi hizi; kiburi, dharau, urasimu, uelewa au uzembe?” imeeleza barua hiyo ambayo imesainiwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Zebadiah Mwanyelele Mwakatage.
  Aidha, barua hiyo imewashutumu viongozi hao wa serikali ya Mkoa wa Mbeya kwa kueleza kuwa sherehe hizo licha ya kuwa na lengo la kumshukuru Mungu kwa ajili ya uhusiano mwema kati ya Tanzania na Israel pia zilikuwa na lengo la kuiombea Tanzania kuendelea kuwa nchi yenye neema na Amani.
  “Licha ya viongozi kupuuza wito wa neema kuu, sijui kama kuna kiongozi yeyote, awe wa serikali au wa dini ambaye hataki amani na utulivu! Ni shetani pekee asiyetutakia amani, tutafurahi sana kama viongozi wetu wataonyesha mabadiliko na kuwa karibu na viongozi wa dini pale wanapohitajiwa kwa ajili ya faida ya taifa na wananchi wake,” imeeleza moja ya haya ya barua hiyo.
  Tanzania Daima ilimtafuta Askofu Mwakatage ambaye alikiri kuandika barua hiyo kwenda kwa Rais Kikwete juu ya kuonyesha huzuni yao kwa viongozi wa serikali ya Mkoa wa Mbeya wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo John Mwakipesile kutohudhuria shehehe hizo.
  “Ni kweli hiyo barua tumeandika sisi maana tumehuzunishwa sana na uongozi wa mkoa huu kutoweza kuhudhuria sherehe hizo ambazo zilifanyika eneo la Simike, mkoani hapa licha ya kuwapa taarifa mapema, na kibaya zaidi hawakufika na hawakutoa taarifa zozote za kutofika kwao,” alisema Askofu Zebadiah Mwakatage.
  Licha ya barua hiyo kuonyesha viongozi hao kupewa nakala ya barua aliyoandikiwa Rais Jakaya Kikwete, uchunguzi umebaini kuwa viongozi hao wanaoshutumiwa hawajapata nakala ya barua hiyo.


  http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=12550
   
 2. B

  Bull JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanapaswa watafautishe Nchi na Kanisa, Tanzania ya sasa siyo ile ya Nyerere, things have changed. Hawa walijisahau sana, wanaendelea kufikiri kuwa Tanzania kama nchi haina tafauti na kanisa. Kweli wanahitaji elimu ya Uraia
   
 3. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Mbeya yetu kituko sana kwa kweli. Kwanza hata hapa mjini watu hawautaki uongozi wa mkoa. Ukiona mpaka independent orfanisations kama DINI zimeanza kulalamika, ujue kuna shida sasa. Maana mmesema sana kuwa ni siasa au ugomvi wa Mwakipesile na Mwakyembe. Lakini kwenye dini kuna nini? Nadhani RC ni kituko cha mwaka. Mfupa mkali
   
 4. c

  charles mususa JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 208
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Ebo hii inachekesha kidogo, kumbe ukialikwa usipohudhuria unashtaikwa! kulikuwa roll call kwa waliohudhuri? hivi kama ni maombi na shukrani mtu akihudhuria lazima akae kwa waheshimiwa? haya makanisa vipi jamani?
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Umasikini wa akili ni mbaya sana kuliko umasikini wa mali.
   
 6. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hiyo haikuwa ibada, bali ni sherehe. Mungu wangu, ninayemfahamu, hahitaji uwepo wa Mwakipesile ili apokee shukrani.

  Ila kama walitaka kujionyesha kwa Mungu na umma, napo inaibua maswali kama kushiriki au kutokushiriki ni kwa lazima. Isitoshe, hao waheshimiwa wanaratiba zao ambazo bila shaka huenda ziliwabana kuhudhuria kongamano/ tafrija hiyo.
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  inaonesha hata wewe umekumbwa na umasakini wa akili kulingana na mchango wa mawazo yako
   
Loading...