Kanisa lakusanya mamilioni kutoka kwa waumini ili ziombewe

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,791
2,078
Elius Msuya
KANISA moja huko Mlandizi, wilayani Bagamoyo, Pwani, limeingia katika kashfa ya kuwatapeli mamilioni ya fedha waumini wake kwa kisingizio cha kuziombea fedha ili kuondoa mikosi kwa kuzifanyia ibada ya utakaso. Uchunguzi wa gazeti hili umeonyesha kuwa ibada katika kanisa hilo, inafanyika ili kuwaombea watu wenye matatizo ya fedha na magonjwa.


Kwa mujibu wa uchunguzi huo, fedha zinazoletwa kwa ajili ya kuombewa, zinawekwa kwenye sanduku maalumu linaojulikana kuwa ni sanduku la agano na baadaye kuombewa kwa muda kabla kuzirejesha kwa muumini.

Mmoja wa waumini waliodai kuibiwa fedha zao, kwa njia hiyo na ambaye hakutaka jina ake litajwe gazetini, alidai kuwa analidai kanisa Sh20 milioni, alizozitoa kwa nyakati tofauti ili ziombewe.


“Nilimpa mtumishi fedha ili aziombee na kuzifanyia utakaso kwa sababu alisema mara nyingi fedha tunazotumia zina mashetani,” alisema muumini huyo ambaye ni mwanamke.



“Unajua kuna wakati mtu unafanya biashara lakini, haitoki, hupati faida, sasa watumishi wa Mungu wanasema kunakuwa na mikosi kama vile chuma ulete. Ndiyo maana nilimkabidhi aziombee,” alisema.


“Mara ya kwanza nilipojiunga nilitoa Sh 600,000 ambazo aliziombea na baada ya miezi minne alinirudishia. Mara ya pili nilikuwa nasafirisha mzigo wa thamani ya Sh 7.5 milioni kwenda Zimbabwe. Siku hiyo walikuja dukani kwangu Kariakoo na kuniambia kuwa itabidi nitoe fungu la kumi la mzigo huo yaani Sh750,000 ambazo hata hivyo, walisema watanirudishia,” alisema.



“Kwa kuwa sikuwa na fedha hizo nililazimika kukopa nikijua kuwa watazirudisha kabla sijasafiri. Kesho yake nilipozifuatilia Mlandizi nikakuta wamesafiri kwenda Moshi, ila wameniachia Sh 75,000 wakisema hilo ndiyo fungu la 10 langu.”


Alisema kiongozi huyo wa kanisa na wenzake walimpa masharti ya kutoa ‘chenji’ fedha atakazopata faida isipokuwa nauli, pesa ya kulipa hoteli na ya chakula tu. Alidai kuwa alipotoka Zimbabwe, watumishi hao walimpigia simu wakimtaka akutane nao Makambako, mkoani Iringa kwa madai kuwa Roho Mtakatibu amewaagiza wakafanyie ibada katika mji huo.



Alisema ingawa ya hakuwa na fedha za Kitanzania lakini kwa faida ya Dola 4,800 alizopata kwenye biashara zake, aliwatii na kushukia Makambako.


“Pale Makambako ndiyo nyumbani kwa wazazi wa huyo mtumishi, tulifanya ibada kuanzia saa saba usiku. Wakaniambia nitoe fedha zote nilizonazo ili waziombee. Nikamwambia itabidi azirudishe mapema kwa sababu nilikuwa na order ya kupeleka mzigo nchini Zambia. Akasema atazirudisha mapema,” alidai muumini huyo.



Alidai kuwa walikaa Iringa kwa muda wa siku tatu na kwamba waliporudi Dar es Salaam, mtumishi alianza kumzungusha licha ya kukumbushwa kila mara. “Badala ya kurudisha fedha kama tulivyokubaliana, alinipigia simu akisema twende kwenye maombi Mlandizi saa saba usiku. Huko tena akasema zile fedha itabidi ziombewe kwa siku saba zaidi. Siku saba zilipokwisha bado alisema ameambiwa na Roho Mtakatibu kuwa fedha zikae kwenye Sanduku la Agano kwa siku 21 zaidi,” alidai.



Alidai kuwa wakati wakiendelea kusubiri siku hizo, mtumishi alimshauri asiendelee tena kufanya biashara.
Kwa mujibu wa mtu huyo, pamoja na kuzungushwa lakini bado aliendelea kumwamini mtumishi kiasi cha kumpa fedha nyingine alizotaka.



Alisema kijana mmoja wa Kitanzania anayeishi naye alitaka kufanyiwa maombi ili mambo yake ya mwendee vizuri na kwamba yeye alimshawishi aje kufanyiwa maombi kwenye kanisa hilo.


“Yule kijana akaja kutoka Zimbabwe kwa ajili ya maombi hayo Siku hiyo mtumishi alikuja nyumbani Kinondoni. nikamtambulisha mgeni wangu kwake. Baada ya kusalimiana, alimwita kisha akamuuliza, una fedha hapo mfukoni. kijana akasita kwanza halafu akaja nje kuniuliza, ‘huyo mama anauliza kama nina fedha mfukoni lakini nimeshindwa kumjibu’. Mimi nikamwambia ampe tu” alisema.


Kwa mujibu wa muumini huyo, kijana huyo alikuwa na a Dola 5,900 na Randi 1,000 ambazo zote aliamriwa kumkabidhi mtumishi kwa maelezo kwamba zinakwenda kuombewa na baadaye kurejeshwa.
Taratibu za ibada Habari zimeeleza kuwa ibada katika kanisa hilo inategemea uongozi wa Roho Mtakatifu na hakuna ratiba maalumu.


Mmoja wa wawatumishi wa kanisa hilo (jina tunalo), alisema hakuna ratiba maalumu hadi pale roho wa bwana atakavyowaambia.


“Hii ni huduma ya maombezi ambayo ukija hapa, tunakuuliza mahitaji yako, kisha tunakufanyia maombi. Unajua sisi hatuombi kama makanisa mengine. Tunafuatilia mzizi wa tatizo la mtu tangu kizazi cha kwanza. Kama wewe hukufanya matambiko na maagano, inawezekana wazazi wako au hata babu zako. Hayo yote tunayavunja kwa jina la Yesu. Muda wa maombi utategemea uzito wa tatizo,” alisema Kuhani huyo.


Baadhi ya watu walioko karibu na kanisa hilo, walisema misururu ya magari imekuwa ikufurika ikiwa na watu wanaofanya ibada katika kanisa hilo hasa nyakati za usiku.


“Hapa kila siku wanakuja matajiri na magari yao ili kuombewa na mara nyingi ibada zinafanyika usiku,” alisema mwana kijiji ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini. Siku ya maombi Akisimulia jinsi ibada ya kumwombea kijana huyo ilivyofanyika, mwanamke huyo alisema waliandaa mbuzi, maziwa, pombe ya mbege, mvinyo, vitambaa vya rangi mbalimbali, mtama na ulezi.


“Alisema vitu vyote hivyo ni kwa ajili ya kutengua laana alizowekewa na mababu zake. Ibada ilifanyika usiku wa manane huku yule kijana akiogeshwa kwa mvinyo, uliochanganywa na damu ya mbuzi na sarafu za amani huku akiombewa. Baadaye vile vitu vilichanganywa na biblia mpya na kufukiwa kwenye shimo. Yule kijana alioga na kwenda kupumzika. Hata hivyo, ibada iliendelea kwa siku tatu.” Alisema baadaye kijana aliambiwa asubiri kwa muda wa siku 21 ndipo akachukue fedha zake huku akitakiwa kujitakasa ndani ya siku hizo, lakini hadi sasa hajapata fedah hizo.


Sanduku la agano Kwa mujibu wa mwanamke huyo, baada ya kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Oysterbay na Polisi Mlandizi, alipewa ushirikiano iliowezesha kumkamata huyo mtumishi huku wakifuatilia kilichomo ndani ya Sanduku la Agano. “Siku hiyo tulikwenda na polisi kwenye kanisa hilo usiku, wakalitafuta bila mafanikio. Ikabidi waondoke. Ila wakati tunaondoka nilitumiwa ujumbe mfupi na mmoja wa waumini kuwa limefukiwa karibu na madhabahu.


Alisema siku iliyofuata polisi walilifukua na kulipata na kwamba walipolifungua walikuta bahasha nyingi, msalaba, Biblia, kitabu cha Tenzi za rohoni na fimbo.


Muumini mwingine wa kiume, ambaye pia ni mfanyabiashara naye alidai kutapeliwa Sh1.2 milioni alizoambiwa kuwa ni kwa ajili ya ‘Baraka za Ibrahim’ yaani makabila 12 ya Israel.
Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Wajinga ndio waliwao
 
Ndugu,

Walimwengu wanabuni namna ya kuishi, na sisi kwa kuwa ni binadamu inabidi tutafute namna ya kuishi nao. Pole ila inabidi tuwe makini kuhusu suala la IMANI
 
Huu ni ushetani 100%; duh yaani unaliwa mshiko wako then unaachiwa fungu la 10 kutoka ktk pesa yako. Kwa hakika Mungu wa hawa watu si mungu wangu.
 
Kuna watu wadini fulanifulani wanapenda kuwabagua wenzao kwa mavazi, matamshi na majina. Kwanini?
 
Wajinga wanaliwa kila siku! Halafu hii dhani ya utakaso ameitumia yule "nabii zaidi" kumchana mke wa mtu kwa kisingizio cha utakaso! Siku ya mwisho kutakuwa na kazi! naomba JF members wote tuwe pamoja siku hiyo tuchekane! tehe tehe tehe tehe...................
 
faiza fox..kwa nini marehemu alioa kabinti ka miaka sita?

Mnamkumbuka FaizaFoxy.

Ya nini kumuuliza marehemu? tuwaulize waliopo hai, soma hapa halafu ujibu wewe muumini wao: Notorious paedophile priest left laptop with 280,000 child-porn images on plane - Courts, National News - Independent.ie

Na hapa: Paedophile priests remain part of church | World news | The Guardian

Kama bado, sema ntakuwekea na wengine walio hai uwaulize, au unataka nikuletee kutoka jikoni? Vatikan?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom