Kanisa laionya NEC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa laionya NEC

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Oct 28, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  BARAZA la Makanisa ya Pentekoste (PCT) limeeleza kuwa hakuna mgombea ambaye anapewa kipaumbele na baraza hilo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili.

  Akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari jana, mwenyekiti wa PCT, Askofu David Batenzi alisema, PCT inaitaka Tume ya Uchaguzi (Nec) kusimamia kwa haki uchaguzi mkuu na kutoa haki bila kupindisha, likisema kuwa jaribio lolote la kuupindisha ukweli ni hatari kwa amani ya Taifa.

  "PCT inatoa tamko kwa umma wa Watanzania kwamba haina chama au mgombea anayepewa kipaumbele au kupigiwa kampeni ndani ya umoja wake katika uchaguzi mkuu wa 2010, lakini ni vizuri Tume ya Uchaguzi isimamie kwa haki uchaguzi huo na itoe matokeo kwa haki kwa kadiri yatakavyokuwa kwa kuwa kupindisha matokeo ni hatari kwa amani ya taifa", alisema Askofu Batenzi.

  Mytake: Ni maneno ya hekima hayana udini wowote lakini wasiopendezwa nayo watayapindisha. Jaji Lewis Makame, Rajabu Kiravu including John Tendwa are the victims of this message.
   
 2. T

  The King JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana!
   
 3. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mungu aibariki Tanzania, Damu ya Yesu inafunika kila kitu kipindi cha uchaguzi na kila hila itagoma na kuwa wazi. Amina
   
 4. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tendwa, makame, kiravu, na njama zenu zinatizamwa sana na kila mtanzania. kama mkidhani mtafanya uvurugaji utokee, ICC, Mahakama ya kimataifa itawabeba wote ninyi. hakuna la kuficha ktk hili. liepukeni.
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Mungu ni mwema anafikisha ujumbe kupitia vinywa vyetu siku zote.
   
 6. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mkuu Luteni,

  Sio busara kabisa kwa kanisa au kundi lingine lolote la kidini kuja na statements kama hizi. Ni sawa na ambavyo haikuwa sahihi kwa jeshi kutoa ile statement yao.

  Kama wana ushahidi wowote basi waikabe NEC kwa makosa inayofanya na sio kutoa statements vague kama hii ambayo inaweza kuwa na matokeo mabaya kwani inawaandaa wananchi kwamba kuna kitu cha ajabu NEC inapanga.

  Kama huamini au huna ushahidi kwamba NEC itapindisha mambo kwanini utoe tamko?

  Haya mambo ya dini yanaenda pabaya Tanzania. Kuna vyombo vingi vya kuhakikisha uchaguzi unaenda kwa haki na kama sio wa haki vitasema. Hatuhitaji kuhubiriwa na makanisa au misikiti kila siku wakati wameshindwa hata kuwapa somo hao waumini wao wakawa raia wema.
   
 7. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siri imefichuka.Pamoja na kujificha nyuma ya pazia. Kikwete ni Rais Tu. Padre Slaa Mmhhhhhhh
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa kura yako wewe sawa.Kwa kura za Watanzania itajulikana baada ya tarehe 31/10/2010.
   
 9. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Your completely off point. Soma kama unasoma sio kuperuzi
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mungu Ibariki Tanzania
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni statement gani unayoiona mbaya kwako waliposema 'kupindisha matokeo ni hatari kwa amani' ulitaka wasemeje, je wanaosema tuchagueni sisi mdumishe amani wana wasiwasi gani wengine wakichaguliwa au wanaushahidi gani amani itatoweka, soma angalizo langu.
   
 12. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Kwa kawaida viongozi na watawala ktk Africa huwa hawataki kujifunza kutokana na kiburi. Pamoja na hayo napenda kutoa ushauri kwa NEC/ZEC kujifunza kutoka kwa tume ya Uchaguzi kenya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwisho.
   
 13. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Kama umeshindwa kuelewa nilichoandika basi kazi ipo! I am not off point! I stand by every word in my comment!

  So far NEC has done a very good and transparent job in preparing this election! Kanisa wanatoa tamko ili iweje?
   
 14. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Nina wasi wasi Lewis Makame,Rajab Kiravu na John TENDWA,watakua wateja wa Moreno Ocampo mda si mrefu.
   
 15. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Naona kama vile jembe la leo ulizidiwa na jua. Kapumzike kivulini
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Ni tamko zuri sana kwa mustakabali wa taifa letu.......

  swali," kwa nini masheikh na mamufti walianza kwanza kwa kuwaambia waumini wao wasimchague dr.slaa alafu baadaye ndiyo wa kwanza kuhubiri kuwa tusichanganye siasa na dini na huku wakionesha wakristo wakorofi wakati wao ndiyo wa kwanza kuonesha kwa vitendo?
   
 17. G

  GAMA LUGENDO Senior Member

  #17
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hakika bwana amesikia kilio, masononeko, kupuuzwa na kunyanyaswa kwa watu wake.Mungu ni mwema na siku zote husimamia wale wenye haki.Sauti za walio wengi ni sauti ya Mungu.Wizi hautafanyika na jaribio lolote litazuiliwa na mwenye enzi Mungu na wale watakao husika tunamuomba Mora awape adhabu kama zile alizopewa Farao na watu wake wakati wa Musa.
   
 18. P

  PAMBANA Member

  #18
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana askofu lakini tuendelee kuliombea taifa letu kila mtu kwa dini yake.


  CHAGUA CHADEMA CHAGUA DR.SLAA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU
   
Loading...