Kanisa lachomwa moto Ngara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa lachomwa moto Ngara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 3, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  Kanisa lachomwa moto Ngara


  Na Theonestina Juma, Ngara

  KANISA la Pentekoste ambalo waumini wake walikimbia nyumba zao na kuishi porini baada ya kukataa kunyunyiziwa dawa ya kuua mbu limechomwa moto na mwananchi mmoja mwenye hasira kwa madai kuwa serikali imeshindwa kumchukulia hatua mchangaji wa
  kanisa hilo.

  Waumini wa kanisa hilo, walikimbia nyumba zao na kupiga kambi katika pori la Nyakafandi, Kata ya Mugaza wilayani hapa kwa madai kuwa kukubali nyumba zao kunyunyiziwa dawa hiyo ni kinyume, kwa kuwa mlinzi wao ni Mungu pekee.

  Mwandishi wa habari hizi alishuhudia waumini hao wakiwa na watoto wao katika pori hilo.Mchungaji Annamaria Mulengera, alisema Kanisa lao ambalo lilijengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi lilichomwa moto Novemba 7, mwaka huu saa 1:00 jioni.

  Alimtaja mwanamume aliyechoma kanisa lao, ambaye mke wake ni miongoni mwa waumini wa kanisa hilo kwa madai kuwa mchungaji amevunja ndoa yake.Alisema mwanamume huyo alikuwa akiwatembelea mara kwa mara lakini baadaye wamebaini kuwa alikuwa akiwachunguza jinsi wanavyoishi ili kutimiza lengo lake la kuchoima kanisa.

  Hata hivyo, mchungaji huyo alisema hawakuripoti tukio hilo popote kwa kuwa wanamwamini Mungu kwa kila jambo na kwamba aliyefanya tukio hilo anatumiwa na shetani.Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bulinda Kijiji cha Mukubu, Bw. Thobias Nkenke, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kukiri kuwa mwanamume aliyetajwa ndiye aliyefanya kitendo hicho.

  Alisema kuwa mwanamume huyo alifikia maamuzi hayo ya kuchoma moto kanisa hilo baada ya mkewe kumkimbia na kuhamia katika pori hilo pamoja na mwanawe mwenye umri wa miaka mitano.

  Alisema mtuhumiwa huyo alidai kuwa mkewe alikataa kurejea nyumbani na mwanaye kwa madai kuwa wametokewa na sauti ya Mungu kuwa anakaribia kushuka.Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Bw. Salum Nyakoji alikana kuwa na taarifa za kanisa hilo kuchomwa moto.Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kagera, Vitus Mlolere, aliahidi kufuatilia kwa karibu suala hilo.
   
 2. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2010
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Zanzibar makanisa yanachomwa moto kila uchao, lakini serikali iko kimyaaaaaaaaaa tu
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Dec 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Yalio tokea uko Ngara, hutaki kuyaongelea!?
   
 4. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hili la ngara naona halina matatizo sana kama uchomaji wa zanzibar-maana huyo aliechoma inawezekana ni frustration za kuchukuliwa mke wake ndo zilizomfanya afanaye hivyo-ila kwa wale wanaochoma zanzibar0huwa wana political & religuious motives
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana
   
 6. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Kumbe mambo ya 2010?Nilidhani issue mpya!!
   
 7. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Bila shaka waumini wa Kanisa hilo wameachana na ujinga na kurudi majumbani mwao na dawa ya kuua mazalia ya mbu imepulizwa!
   
Loading...