Kanisa La Waadventista Wasabato na mabadiliko

Eliya Dawa

JF-Expert Member
May 12, 2014
270
164
Habarini Wakuu

Katika kukaa kwangu na kutafakari katika muonekano na katika biblia tunasoma siku ya sabato yapaswa kufuatwa sawa lkn nina mtazamo chanya ambao wasabato wanaupuuzia siku hizi na tunasema kuwa tunaifuata biblia

1 Suala la wanawake kuhudumu ni makosa ktk biblia limekataliwa na mtume paulo naambatanisha hapa
1 Timothy 2:8 Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.

2: Suala la mavazi ni tatizo ikiwa tunaenda kwa kufuata biblia then wanawake ni lazima watii kwa kila namna
1 Timothy 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

3: Maaskofu na Mashemasi ni lazima wawe wanaume na sio wanawake ktk kanisa letu tumekuwa tukiwapa wanawake kile kinachoitwa haki sawa ikiwa tunafuta Biblia basi hakutakiwi kuwa na usawa tena biblia imekataa kabisa mwanamke kusimama kanisani

Kisha kuna suala la Ellen G White ikiwa tunaamini Biblia kama. Kiongozi wetu mkuu basi Ellen G White sio nabii kwa kuwa biblia imesema mwanamke Alitenda Dhambi na akapotoka kabisa Mungu hawezi kusema leo hivi afu kesho hivi Biblia ni shahidi No1 ~ 1 Timothy 2:12
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

Kuna mafungu pia kama 1Wakoritho 11: 3 na kuendelea
[14] Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.

Sasa kwa muktadha huu ikiwa tunifuata Biblia then Ellen G White sio Nabii Ndg Zangu wasabato naomba mje mnipe maelekezo huwenda mm sielewi mambo yanavyotakiwa kwenda

Lakini waislam wako sahihi kwenye maswala ya kuhudumu na mavazi.
 
Dunia inabadilika, Mungu alipotuma manabii enzi hizo kulikuwa na mazingira yanayoruhusu. Kwa mfano kama wanaume hawako serious ndo tuiache injili isisonge mbele? Acha kina mama wapige injili ulimwengu kama uliingia dhambi kupitia mwanamke likewise unaweza kuokolewa kupitia mwanamke
 
Bublia haiko hivyo ,eti wanaume hawako serias 😀😀😀😀
 
Bible imesema YESU hakuja kutangua torati Bali kutimiliza, torati sheria ilisema jino kwa jino ,ila YESU asema samehe maana hata ww una dhambi hatuokolewi kwa Matendo na Sheria bali kwa Neema ya MUNGU aamineye na kubatizwa ataokolewa YESU alikuja kuweka usawa ktk wokovu kukamilisha wokovu maana ni mpango wa ulioasisiwa kwa nyakati na wakati
 
Hao mashemasi mmm palipo na wanaume 10 wanawake 50 hao wanaume wanajigawa vipi hapo!
 
Usisome Biblia kwa kuruka ruka,, Siyo kila kitu walivhofanya mitume, wafalme na manabii kina apply katika tamaduni zote,, Fuatilia Paulo alikuwa anawandikia akina nani muda huo, mazingira yao na utamaduni wao ulikuaje..

Haya Wana wa Israel waliongozwa na manabii wanawake kama, Debora, Naomi, Ruth, Ester, Miriam. N.k hao wote walikuwa wanawake unasemaje mwanamke asinene mbele ya wanaume na Akae kimya??

Kama sisi wenye Dini yetu tumekubali wanawake wahudumu katika ibada zote kama uimbaji na kuongoza idara wewe ni nani?? Zingatia jambo lolote lililoanzishwa kwa mapenzi ya mwanadamu Mungu hawezi kuruhusu likadumu Ataliondoa tu,, Hivyo usipate taabu kama Wanawake kuhubiri na kuongoza ni Mpango wa Mungu basi hata watokee wapingaji Litadumu.. na kama siyo mapenzi ya Mungu basi Litaondoka lenyewe.. Mungu hapiganiwi anajipigania mwenyewe.
 
Habarini Wakuu

Katika kukaa kwangu na kutafakari katika muonekano na katika biblia tunasoma siku ya sabato yapaswa kufuatwa sawa lkn nina mtazamo chanya ambao wasabato wanaupuuzia siku hizi na tunasema kuwa tunaifuata biblia

1 Suala la wanawake kuhudumu ni makosa ktk biblia limekataliwa na mtume paulo naambatanisha hapa
1 Timothy 2:8 Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.

2: Suala la mavazi ni tatizo ikiwa tunaenda kwa kufuata biblia then wanawake ni lazima watii kwa kila namna
1 Timothy 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

3: Maaskofu na Mashemasi ni lazima wawe wanaume na sio wanawake ktk kanisa letu tumekuwa tukiwapa wanawake kile kinachoitwa haki sawa ikiwa tunafuta Biblia basi hakutakiwi kuwa na usawa tena biblia imekataa kabisa mwanamke kusimama kanisani

Kisha kuna suala la Ellen G White ikiwa tunaamini Biblia kama. Kiongozi wetu mkuu basi Ellen G White sio nabii kwa kuwa biblia imesema mwanamke Alitenda Dhambi na akapotoka kabisa Mungu hawezi kusema leo hivi afu kesho hivi Biblia ni shahidi No1 ~ 1 Timothy 2:12
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

Kuna mafungu pia kama 1Wakoritho 11: 3 na kuendelea
[14] Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.

Sasa kwa muktadha huu ikiwa tunifuata Biblia then Ellen G White sio Nabii Ndg Zangu wasabato naomba mje mnipe maelekezo huwenda mm sielewi mambo yanavyotakiwa kwenda

Lakini waislam wako sahihi kwenye maswala ya kuhudumu na mavazi.
Naona sasa mnamalizana wenyewe kwa wenyewe.
 
Bible imesema YESU hakuja kutangua torati Bali kutimiliza, torati sheria ilisema jino kwa jino ,ila YESU asema samehe maana hata ww una dhambi hatuokolewi kwa Matendo na Sheria bali kwa Neema ya MUNGU aamineye na kubatizwa ataokolewa YESU alikuja kuweka usawa ktk wokovu kukamilisha wokovu maana ni mpango wa ulioasisiwa kwa nyakati na wakati
Lkn mkuu umesahau kuwa nimetoa mafungu katka Agano jipya tena baada ya Yesu na ufunuo huo alipewa paulo na yesu mwenyewe hapa kunahitajika deep scanning 😂😂😂
 
hakuna kanisa hapo kwa sasa maana wanaume hadi ndani ya familia tunaendeshwa,hadi sasa mm nategemea kuasi hilo kanisa
 
Back
Top Bottom