Kanisa la Efatha la Mch. Mwingira limejengwa sehemu ambayo nina mashaka nayo

Tulijua lazima hayo yatokee baada ya juzi clip kumuonyesha akimsifia mungu kwa maajabu aliyoyaonyesha kwa mhe.Lissu ...risasi 16 na bado yu hai?? Huyu mtu Ni mshindi ..alisikika pastor Mwingira ..povu povu ccm povuuuuuuuuuuu
 
Mimi siyo shabiki wala mfuasi wa Mwingira ila kabla ya October 28 Mch Mwingira ajiandae kwa yafuatayo:
1. Kuulizwa uraia wake
2. Kuulizwa mapato ya kanisa
3. Kuulizwa records zake za ulipaji kodi
4. Usajili wa kanisa lake
5. Kuulizwa bodi ya wadhamini wa kanisa lake
6. Mahusiano yake na waumini wanawake
7. Silaha anayomiliki
8. Uhusuano wake na chadema
9. Kujenga eneo lisilotakiwa

Huu ndio Uhuru anaoupigania Lissu.

Sasa vyombo vikikurupuka na kumshugulikia Lissu anapata credit na waumini wake wengi watamuunga mkono Lissu.

Sasa ni wakati wa wasiopenda kusemwa wazoee kuishi ukweli
 
Watu bwana! hayo yote hamkuyaona kumhusu mpaka alipoonyesha kumuunga mkono Tundu Lissu.
Ni vizuri kiwa na uvumilivu wa kisiasa hamwezi kutaka watu wawazungumze wapinzani vile mnavyotaka. Kama ambavyo hao mnawazungumza wapinzani kwa ubaya kwa sababu mmeona mnayoyaita mabaya msiwazuie wengine wawazungumze kwa mazuri yao waliyo yaona.

Naona pia hujui madhara ya kutekelezwa kwa mapendekezo yako maana hiyo inaweka wazi zaidi mdhaifu ya serikali ya ccm na wizara zake kuanzia uhamiaji, ardhi usafirishaji na ulinzi na serikali ya aina hiyo haipaswi kuwa madarakani tena.

KWA UFUPI JIANDAENI KUACHIA NCHI NA MUANDAE MAPEMA WATU WA KUWAWEKEA DHAMANA MAHAKAMANI.
 
Hapana hapakuwa na upotevu wa hela mkuu. Zile ni propaganda. Ila nadhani kuna umuhimu wa kuachana na siasa za uongo, na ninadhani serikali inaangalia namna ya kuzuia uongo na uzushi, maana mtu kama wewe hicho kitu cha uongo unaweza kuta moyoni mwako unaamini ni ukweli
So CAG alidanganya?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Ka-tortoise alinyooshwa kweri kweri, akanyooka mpaka akapitiliza, sasa ndiye anasifu kuliko aliowakuta kwenye praise team.
Mwingira kasema ukweli ambao unaweza kumgharimu, amejiandaa vipi yeye ndiye anajua na Mungu wake.
eti "ka-tortoise"🤣🤣🤣
 
Nmepita leo kuangalia lile Kanisa lilipojengwa nimepata mashaka kiasi. Nina wasiwasi linaweza kuwa limejengwa kwenye hifadhi ya barabara au limejengwa sehemu ambayo kulipaswa kujengwa bandari kavu.

Lakini pia ile sehemu inawezekana kabisa ikawa ni eneo la Jeshi. Maana kuna kambi ya Lugalo maeneo hayo. Haya mambo sidhani kama Mch. Mwingira ameyafikiria.

Lakini pia nadhani ana mashamba/viwanja vingi vyenye mgogoro huu ndo wakati wake wa kutatuliwa migogoro hiyo kwa kurudishwa maeneo husika hivyo viwanja na mashamba.

Sijajua kama Mwingira analipa kodi ipasavyo. Hili nalo naweka tu kama angalizo maana kumekuwa na tabia ya watu mbalimbali kutolipa kodi mpaka Serikali inasahau. Ila wakija kuimbusha wenyewe baadaye wakidaiwa wanalalamika tena. Mwingira ameanza ikumbusha serikali mambo haya.

Haya nmeyaongea kwa kuangalia tu mwenendo wake na mambo kadhaa. Tusubirini tu siku si nyingi sana.
Ajiandae kwenda KISUTU
 
Back
Top Bottom