Kanisa la Anglikana: Ndoa ni kati ya MUME na MKE

Status
Not open for further replies.

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Kanisa la Kianglikana duniani limesisitiza kwamba ndoa ni kati ya mwanamume na mwanamke na likasimamisha ushirika wa jimbo la Marekani lililotambua ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Jimbo hilo la Marekani, ambalo kwa Kiingereza hujiita Episcopal Church, sasa halitaruhusiwa kushiriki kikamilifu katika masuala ya kanisa hilo.

Viongozi wa kanisa la Kianglikana duniani, waliokutana Canterbury, wamesema kanisa hilo lilikiuka Imani inayofuata na waumini wengi wa kanisa la Kianglikana kuhusu ndoa.

Marufuku hiyo ya muda ambayo imepewa jimbo hilo a Marekani inalenga kuzuia kugawanyika kabisa kwa kanisa hilo kutokana na tofauti kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.

Ndoa hizo zimekuwa zikipingwa sana na majimbo ya kanisa hilo barani Afrika.

Uamuzi wa kusimamisha uanachama wa jimbo hilo la Marekani ulifanywa katika mkutano ambao umeeleza kuwa "mkali sana".

Askofu wa sasa wa jimbo hilo la Marekani Michael Curry amesema uamuzi huo "utasababisha uchungu mwingi". Mzozo kuhusu ndoa za jinsia moja ulianza kutokota baada ya kutawazwa kwa Kasisi Gene Robinson, aliyekuwa ametangaza hadharani kuwa mpenzi wa jinsia moja, kuwa askofu wa dayosisi ya New Hampshire ya jimbo hilo la Marekani mwaka 2003. Hatua hiyo ilizua mgawanyiko mkubwa miongoni mwa viongozi na waumini wa kanisa hilo duniani.


Chanzo: BBC
 
Kuna vitu viwili ambavyo ni aibu ya dunia kwa sasa. Cha kwanza ni USHOGA na cha pili ni UGAIDI. Ila kwa Tanzania tuna kingine MAUWAJI YA BINADAMU KWA IMANI ZA KISHIRIKINA. Ni aibu kwamba tunaishi katika kizazi ambacho mambo haya yanatendeka tena waziwazi.
 
Nilipenda msimamo wa Askofu wa Uganda kwenye Mkutano huo ambaye naskia kuna wakati alitoka nje kuonyesha msimamo thabiti na kwamba hakukua na cha kujitetea wala nini, ilikua ni msimamo tu kwamba Canterbury lazima waondolewe. Sijui Askofu wa TANZANIA alisemaje..... mana JK akiwa kama Rais enzi zile alipoulizwa kuhusu ushoga alisema kuwa ni suala la muda tu, watuache kwanza!!!
 
kila jambo linapitia Marekani,..kuenea duniani,..ibilisi anatumia sana marekani kwasababu ni taifa lenye nguvu,...sodoma na gomola iliteketezwa kwa machukizo kma haya,..leo ibilisi anaitumia marekani kupitisha na kuhalalisha huu uchafu,..napata picha ibilisi anaitumia sana USA Kuiharibu dunia,.....through utandawazi,...watu tunatakiwa tuwe makini na hili,..
 
Hii Daniel alitabiri katika kitabu chake, sura 9 mstari wa 26 na 27. Ni wazi alimaanisha watakuja watawala ambao hawataheshimu tena mahala patakatifu, badala yake watapabadili na kuwa mahala pa kufanyia kufuru na kwenda kinyume na matakwa ya mungu.
Eti maaskofu wanajadili ushoga.... ni ajabu. wasije siku moja wakaanza kujadili kubadili maandiko matakatifu
 
Ndoa ya jinsia moja ni uasi dhidi ya Mungu kwani utaratibu huo haukuwa mpango wa Mungu tangu awali.
Kwani sababu ya Mungu kuanzisha ndoa ni nini? Kama siyo ya kwanza basi ni ya pili kwamba watu waweze kupata watoto na kuongezeka. Je ndoa ya jinsia moja kusudi lake au matokeo yake ni nini? Binadamu ni muasi kwa asili na kwa jinsi hiyo humfuata muasi mkuu mkuu wa kwanza shetani. Hivyo basi hao wanafuata mfumo huo ni wa shetani.
 
Ila pesa zao mnazipokea

Ndo nashangaa...
Mie nafikiri ushirikina nayo ni laana tosha pia. Mbona africa tunaongoza kwa ushirikina na tanzania ndo tuko mstari wa mbele kuuwana kutokana na imani za kishikina? Kwani hiyo ni dhambi ndogo machomani kwa Mungu kulinganisha na ushoga? wamarekani nao basi mbona hawaigi huu ushirikina wetu tukawaaona nao wanaaanza kuuwa albino? hivi kweli tumeshikiwa kisu kuiga tabia ambazo ni kinyume na maadili yetu? hata kama tumeshikiliwa kisu kwanini basi tukubali kuwa wanyonge? hiyo nayo si laana nyingine tu? Kwa hiyo kweli tunataka kusema sisi ni watu righteous sana na kwamba wamerekani ndio wanatuchafua?

I am not condoning ushoga... lakini lets take a step back kabla hatujawatupia wamerekani lawama... tujiulize sisi tunafanya nini ili kuhakikisha maadili yanazingatiwa na dunia inakuwa mahali salama...
 
Matatizo ya kuleta sasa kanisani. Huo mkutano haukuwa na ulazima. Biblia iko wazi kuwa ulawiti/ufiraji/usagaji/ushoga ni dhambi na machukizo mbele za Mungu. Ni upumbavu wanadamu kuweka kikao kujadili jambo ambalo Mungu wanayedai ni Mkuu wao ameshalotolea uamuzi kuwa ni dhambi.
.sishangai lakini maaana Biblia imrwataja watu kama hawa. They just prove God right
 
Mara nyingi binadamu huuona uovu wa mtu mwingine ni mbaya kuliko wa kwake.

Ushoga ni dhambi, hakuna mjadala. Maana neno la Bwana linasema, 'hakika waasherati, wafilaji, waabudu sanamu, walevi, wauaji, kamwe hawataurithi ufalme wa Mungu'. Miongoni mwetu yawezekana hakuna wanandoa wa jinsia moja (wafilaji), Je wazinzi/waasherati hawapo? Walevi hawapo? Wauaji hawapo (wauaji wa albino/vikongwe)? Waabudu Miungu (wapiga ramli) hawapo?

Tunawaona Wamarekani ni wadhambi sana kwa sababu ya ndoa za jinsia moja lakini neno la Bwana halitofautishi uzito wa dhambi katika hizo nilizozitaja hapo juu. Tumwombe sana Mungu Baba yetu wa mbinguni ili atujalie neema ya kuuona uovu wetu kwanza kabla ya ule wa mtu mwingine.

Kuachilimbari ushabiki na mambo ya kuiga Mkuu hilo si la kijinga,Hta Mungu apendezwi na hilo swala na limepigiwa kelele karibu vitabu vyote vitakatifu ...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom