Kanisa kuu la MT. Patriki Morogoro ondoeni haya mapungufu

kzba

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,356
789
Kwako Paroko,

Mimi ni muumini wa kanisa tajwa hapo juu, na huwa nahudhuria misa takatifu kila jumapili , kuna baadhi ya mambo sioni kama yako sawa juu ya uendeshaji wa misa katika parokia hii.

Kwanza, mwanzo wa misa kunakuwa na mlolongo wa matangazo ambayo hayana hata tija kwa maana ya kwamba wahusika wa matangazo hayo wangeweza kusoma hata ubao wa matangazo.

Pili, nyimbo za kusifu na kuabudu ni za kizamani mno kiasi kwamba wengi wetu tumeshazisahau kuimba ingawa ni wa seminary.

Tatu, sala na majitoleo mbalimbali, kumekuwa na mlomlongo wa Sara za kubuni na matoleo ambayo hayana tija, mfano Sara ya kuombea korona na kumpata askofu ni ndefu sana na wengi wa waumini hawajazikalili Sara hizo,

Nne, wanakwaya na waimbaji, wamepooza kiasi kwamba hata kutamka vizuri nyimbo wanashindwa.

Tano, mazingatio ya muda hili kila muumini anafahamu, hapa kanisani hawazingatii muda katika kuendesha utaratibu mzima wa misa.

Ushauri,
Badilisheni muda wa kuanza misa takatifu hasa za juma pili kwa maana ya kwamba , misa ya kwanza ianze saa 12 kamili asubuhi mpaka saa moja kamili, ya pili ianze saa moja na dk 20 mpaka saa mbili na nusu, ya tatu saa 3 kamili mpaka saa nne.
Ondoeni mlomlongo wa matangazo.

Nendeni mkajifunze katika kanisa la kiwanja cha ndege dodoma mkutane na faza jarome atawapa somo zuri na pia mkajifunze kanisa la mtakatifu immaculate kurasini dar es salaam hasa mapadre(paroko), na wanakwaya. Mtabadilika.
Nb;
nitachangia laki tatu katika ziara hizo na mafunzo.

20210411_081923.jpg
 
Mkuu ibada uitakayo kaongee na uongozi Natumai watakuelewa.. Wakizingua Tanzania is a free independence country jichange fungua kanisa lako.

Nasema uwongo Ndugu zangu..
 
Kuna makanisa watu huwa wanaenda kufarijiana na kutimiza wajibu tu ila sio kwenda kusali.Kwangu maana ya ibada ni kubwa na sio km haya niyaonayo kwenye makanisa siku hizi.
 
Humu hupati msaada wowote!
Nakushauri kwamba uache woga!
Peleka tatizo lako kuanzia Jumuiyani kwako.
 
hivi hio sala ya kuombea askofu apatikane kwani mapadre wa kuchaguliwa kua askofu hawapo? au ni urasimu , au ni ugumu wa kufikisha jina vatikani?
tokea 2019 mpaka leo hawana askofu, na ilijilikana kabisa askofu mkude 2020 anastaafu sasa mbona hawakufanya maandalizi?
 
hivi hio sala ya kuombea askofu apatikane kwani mapadre wa kuchaguliwa kua askofu hawapo? au ni urasimu , au ni ugumu wa kufikisha jina vatikani?
tokea 2019 mpaka leo hawana askofu, na ilijilikana kabisa askofu mkude 2020 anastaafu sasa mbona hawakufanya maandalizi?
Mmh
 
...Sara (sala) ...hawajazikalili Sara (hawajazikariri sala)...

unapokosoa ukumbuke nawe sio mkamilifu
 
Back
Top Bottom