Kanisa kumuombea JK dhidi ya mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa kumuombea JK dhidi ya mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MaxShimba, Dec 9, 2008.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160

  Kanisa kumuombea JK dhidi ya mafisadi

  Na Peter Mwenda

  WAUMINI wa Kanisa Katoliki nchini, leo watakuwa na ibada maalum ya kuombea taifa liendelee kuwa na amani, utulivu na kuitakia mafanikio mema Serikali ya awamu ya nne katika vita dhidi ya ufisadi.

  Hayo yapo katika salamu za Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kadinali Policarp Pengo zilizosambazwa katika makanisa yote nchini.

  Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Ukonga, Padre Joseph Kanduta, akitoa ujumbe wa Askofu Pengo kwa waumini wa kigango cha Kitunda alisema Wakatoliki wote watakuwa na ibada leo itakayokuwa maalum kwa ajili ya kuombea amani.

  "Askofu Pengo amewataka waumini kuiombea serikali ya Rais Kikwete isikate tamaa kupambana na ufisadi kwa kuwa ni kazi ngumu ambayo inahitaji baraka za mungu kufanikiwa, tufike kwa wingi kuombea utulivu katika kipindi hiki kinachohitaji ujasiri," alisema Padre Kanduta.

  Ibada hiyo pia imeapewa kipaumbele na Wanawake Wakatoliki Nchini (WAWATA) Jimbo la Dar es Salaam ambao wameandaa ibada ya kuombea amani kwa kuwaunganisha wanawake wote wa jimbo hilo kusali pamoja katika eneo ambalo huenda kuhiji lililopo karibu na shule ya Sekondari ya Pugu.

  Habari kutoka kwa wanawake hao zinasema akina mama hao wataanza ibada hiyo kwa maandamano kutoka Shule ya Sekondari Pugu kuingia kwenye eneo maalum la hija ambapo wanatarajia Askofu Pengo ataongoza ibada hiyo.

  Comment in this Story Nakala inayochapika

   
 2. j

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 16,227
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Muse A Muse...Kwanza karibu sana ukumbini.
  Je habari hii umeipata wapi? Whats the source?
  Kwasababu heading inadai kanisa kumwombea JK dhidi ya mafisadi na ukweli ni kuwa ni kuliombea Taifa kama inavyoonyesha kwenye highlight.
  Kauli inayokaribiana na kichwa cha habari hata hivyo ni hiyo ya Pengo kuwa sirkali ya JK isikate tamaa kupambana na ufisadi....Sasa wapi hapo penye JK dhidi ya mafisadi kwenye habari hii?
   
 3. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160

  Peter Mwenda ni mwandishi wa IPP, kwahiyo, nafikiri hii habari ameipata IPP Media
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,167
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Na hilo Jimbo la Ukonga (para 3) liko wapi? Tuache kulegea legea hivi jamani!
   
 5. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,190
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Teh teh, Jimbo? sio kosa lake labda atakuwa amekosea au hajui kama sio Jimbo ila ni Parokia. ni ufafanuzi tu unaohitajika.
   
 6. N

  NTIRU Member

  #6
  Dec 10, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachoombewa hapa si JK dhidi ya mafisadi bali nchi ambayo tayari imekosa mwelekeo. Nchi iliyokosa viongozi wenye dira sahihi akiwemo JK mwenyewe. Nchi yenye viongozi waroho na wabinafsi na walio tayari kuiuza nchi yao kwa wageni ilimradi wajikusanyie mabilioni. "Wananchi kuleni majani, ni lazima 10% ipatikane kwenye biashara ya ndege ya Rais na Rada .....". Kanisa limeamua kumwomba Mungu ainusuru nchi na madhila hayo ili aiongoze kupata viongozi waadilifu na wenye kumwogopa (Mungu)
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ntiru umeileza vyema, ila mwandishi na kichwa cha habari kimepinda kidogo kwani kinaelekeza kumuombea JK aka Chaguo la Mungu!!!

  Well, hapa ni kuiombea nchi yetu Mungu ainusuru katika makucha ya mafisadi!
   
 8. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  To me this is crazy.God does not work like this.For God to help, Kikwete first needs to realize that there is a problem,and then have a genuine desire to solve it.He then needs to take action.Only then can God help in solving the problem.
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Ilikua katika majira ya jana na si IPP Media

  pia ilitoka katika Dar Leo ya wiki iliyopita kwa njia tofauti kabisa

  DarLeo-Gazeti lako la kila siku jioni
  Mkapa,Mramba wagusa Kanisa Katolika. •

  na

  ktk Raia Mwema ya leo nalo kwa njia tofauti pia
   
Loading...