Kanisa Kulipa $ 166 milllions kwa waliopatikana na maovu ya mapadre | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa Kulipa $ 166 milllions kwa waliopatikana na maovu ya mapadre

Discussion in 'International Forum' started by Percival, Mar 27, 2011.

 1. P

  Percival JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Kanisa katoliki litalipa dola za kimarekani zipatazo millioni 166 kwa watu walio ingiliwa na mapadre wakati wakiwa watoto wadogo na wakiishi katika himaya za kanisa. Wengi wa watu hawa ni wananchi wa marekani wajulikanao kama wahindi wekundu ambao kanisa lilikua likisema linawasaidia kwa mashule na malezi. Habari hizi za kusikitisha zilizosababishwa na mapadre waliopotoka zinaendelea kujitokeza na kuharibu jina zuri la kanisa katoliki.

  Cha kushangaza ni kua hii fidia ya mamilioni ya dola inatoka kwenye mfuko wa sadaka na zaka ambao waumini wa kanisa hilo hutoa kwa moyo wa kidini.

  http://www.boston.com/news/nation/articles/2011/03/26/jesuit_order_to_pay_abuse_victims_166m/?p1=Well_MostPop_Emailed4

  Swali kubwa la kujiuliza ni Je inawezekana mambo haya yametokea hapa Tanzania ? Uwezekano kua mambo haya pia yametokea hapa ni mkubwa sana ukichukulia kuwa watoto wadogo wengi walikua wakipewa mafundisho na upendo katika seminari mbali mbali hapa nchini. Ni muhimu kuwahimiza watu wajitokeze ili jambo hili pia lijadiliwe hapa na lizikwe. sababu utakuta watu hao walio chezewa wakiwa wadogo hawana raha au amani katika mioyo yao mpaka watakapo ona mambo yamejadiliwa. pia inawezekana bado yanaendelea katika hizo seminari.
   
 2. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ninachowapendea watu wa western na mifumo yao ni uwazi na kuwajibishana... Nenda nchi za kiarabu uone madhila wanayofanyiwa watumishi wa ndani toka far-east na Africa, kubakwa, kuteswa kwa vipigo nk. ikiwa public maskin wa Mungu anarudishwa kwao na kesi imeisha!
   
 3. P

  Percival JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Serikali ingefaa ianzishe uchunguzi wa jambo hili na kuwaambia watu waliopata majamga haya wakati wakiwa wadogo wajitokeze ili mambo yaangaliwe kwa kina.

  Ni lazima kuna mapadre ( wazungu ) walifanya mambo machafu kwa watoto hapa nchini kwa miaka ya nyuma sababu siku zote utawakuta wako na watoto na watachagua na kuwachukuwa mmoja au wawili kwnye pikipiki au gari na kutoka nao au watasema wana kazi au masuala ya maombi nyumbani kwa padre.

  Haiwezekani hawa wakafanya haya machafu huko Ulaya na Amerika pekee lazima yametokea huku pia.
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kwenye red....mmmhhhh
  kwenye blue, ikiwa wanatoa sadaka na zaka kwa dini na si Mungu, wacha zitumike kufidia uchafu walioufanya wenye dini.
   
Loading...