Kanisa Katoliki yaanzisha kampeni kupima ukimwi waumini wake Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanisa Katoliki yaanzisha kampeni kupima ukimwi waumini wake Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaFalsafa1, Jun 21, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Na Mwandishi Wetu
  KANISA Katoliki nchini limeanzisha kampeni ya kupima virusi vya ukimwi kwa waumini wake ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini alisema, kanisa limeamua kuanzisha mpango huo kwa malengo makuu matatu, kutokomeza ukimwi, kuondoa unyanyapaa na kuhamasisha upimaji afya kabla ya ndoa.

  ``Tunataka kutokomeza ukimwi miongoni mwa waumini wetu, pamoja na unyanyapaa na kuhamasisha hali ya upimaji wa afya kabla ya ndoa ili vijana wetu wasiingie kwenye hatari wanapofunga ndoa,” alisema Kilaini.

  Alisema mpango huo wa kanisa umesambazwa katika majimbo yote ya Kanisa Katoliki na kwamba kila jimbo limeweka utaratibu wake wa kutekeleza maelekezo ya Baraza la Maaskofu kuhusu kutokomeza ukimwi.

  ``Hatutatumia mapadri na makatekista kupima virusi vya ukimwi, ila tutatumia wataalamu wetu chini ya mpango wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS in Dar es Salaam Archdiocese (Pasada), katika kupima na kutoa ushauri nasaha kwa waumini na wasio waumini kabla ya kupima,” alisema.

  Askofu huyo alisema kuwa jimbo lake tayari kazi hiyo imeanza katika parokia tatu za Manzese, Sinza na Tandale pamoja na vituo vingine vya afya vinavyomilikiwa na kanisa.

  Akifafanua jinsi kanisa hilo litakavyoendesha kampeni yake kwa mafanikio, Askofu Kilaini alisema, wataalamu kutoka Pasada wamekuwa wakipewa fursa katika makanisa baada ya misa/ibada kutumia muda huo kuwaelimisha waumini kuhusu umuhimu wa kupima afya zao.

  ``Hakuna muumini atakayelazimishwa kupima virusi vya ukimwi, ila tutatumia wataalamu ambao wataweza kuwashawishi waumini kupima afya zao na kujitambua; na kujua waishi maisha gani baada ya kupima na kufahamu kuhusu afya zao,” alisema Kilaini.

  Aidha, askofu Kilaini alisema kuwa watakaokuwa wanawapima sio watu wanaowafahamu kwa maisha yao ya kila siku, na suala la kupima watakwenda siku ambayo wamejisikia kufanya hivyo.

  ”Tukitoka kanisani hatusemi haya sasa waumini nendeni mkapime, hapo sasa kinakuwa ni kitu binafsi, maana wanaopima sio mapadri,” alisema Kilaini.

  Alisema mpango huo uliridihiwa na Baraza la Maaskofu kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Jimbo la Bukoba, ambalo limeufanya Mkoa wa Kagera kurudi nyuma katika takwimu za maambukizo ya ukimwi ukilinganisha na mikoa mingine, kwa kuwa wanaotaka kuoana wanalazimika kupima virusi vya ukimwi.

  Askofu Kilaini alisema, mpango wa Jimbo la Dar es Salaam kuamua kuwatumia mapadre kulizungumzia suala la kupima VVU baada ya misa litasaidia maana waumini wanaamini kile wanachoambiwa na viongozi wao wa kiroho.

  Kanisa Katoliki hapa nchini litakuwa ndio taasisi pekee ya dini ambayo imeamua kuingilia kinagaubaga suala la kupima virusi vya ukimwi miongoni mwa waumini wake, ukiondoa mpango wa serikali wa kupima wananchi wote uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kupima yeye na mkewe Salma.
  Mwananchi
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Safi! Bado kuhamasisha mipira mambo yaende vizuri zaidi.
   
 3. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
   
Loading...