bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,129
- 2,003
Habari wanajamii,
Katika kipindi hiki cha wasiwasi na sintofahamu juu ya coronavirus ndani ya taifa letu viongozi wa taasisi mbalimbali yapaswa kuonyesha umahiri na umadhubuti kukabiliana na janga hili.
Nitaongelea taasisi za kidini kwani kwa macho yangu naona zimevurugwa zaidi
Mpaka sasa taasisi za kidini Tanzania hazijaonyesha kukabiliana na coronavirus, kwa ufupi viongozi wa kidini wamevurugwa na hili janga hii ni kutokana na ukweli usiopingika kuwa mikusanyiko ni sawa na maambukizo, hivyo hakuna misa hakuna sadaka,
Viongozi wa kidini wamekuwa Paralyzed na political agenda za rais. Rais ameongea kisiasa kwamba ibada ziendelee ili asionekane amezuia ibada, viongozi wa makanisa wana nguvu ya kuzuia ibada ili kuokoa waumini wa makanisa yao. Vitabu vyenyewe vimeongea kuna stori ya talanta, na mifano mingi juu ya mchungaji na kondoo sasa sitegemei mchungaji kupeleka kondoo kwa mbwa mwitu.
Nimechagua Katoliki kutokana na kuwa taasisi kubwa ya kidini Tanzania hivyo kuwa mfano endapo katoliki watasitisha misa wengine watafwata au watapinga. Katika majanga ndio chance kuonyesha uongozi askofu yoyote katika jimbo lolote hapa Tanzania anapaswa kusitisha misa na kuwaongoza maaskofu wenzake katika kufanya maamuzi juu ya corona. Nani anayejua huenda huko mbeleni askofu huyu anaweza kuwa mtakatifu wa korona kwa kuweza kuongoza taifa katika kipindi hichi kuzuia vifo vingi visivyokuwa vya maana.
Mapadri na maaskofu wa katoliki wamekuwa wakiheshimika kuwa elimu ya juu kabisa hivyo haitegemewi wafanye maamuzi kama hawana elimu hiyo. Hivyo wana wajibu wa kulinda heshima hiyo.
Basi endapo wakatoliki watashindwa basi hii ni fursa wa wachungaji wengine kuonyesha umahiri na hivyo kupata heshima kutoka kwa jamii.