Kanisa Katoliki Tanzania linapaswa kusitisha misa

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
237
250
Habari wanajamii,

Katika kipindi hiki cha wasiwasi na sintofahamu juu ya coronavirus ndani ya taifa letu viongozi wa taasisi mbalimbali yapaswa kuonyesha umahiri na umadhubuti kukabiliana na janga hili.

Nitaongelea taasisi za kidini kwani kwa macho yangu naona zimevurugwa zaidi

Mpaka sasa taasisi za kidini Tanzania hazijaonyesha kukabiliana na coronavirus, kwa ufupi viongozi wa kidini wamevurugwa na hili janga hii ni kutokana na ukweli usiopingika kuwa mikusanyiko ni sawa na maambukizo, hivyo hakuna misa hakuna sadaka,

Viongozi wa kidini wamekuwa Paralyzed na political agenda za rais. Rais ameongea kisiasa kwamba ibada ziendelee ili asionekane amezuia ibada, viongozi wa makanisa wana nguvu ya kuzuia ibada ili kuokoa waumini wa makanisa yao. Vitabu vyenyewe vimeongea kuna stori ya talanta, na mifano mingi juu ya mchungaji na kondoo sasa sitegemei mchungaji kupeleka kondoo kwa mbwa mwitu.

Nimechagua Katoliki kutokana na kuwa taasisi kubwa ya kidini Tanzania hivyo kuwa mfano endapo katoliki watasitisha misa wengine watafwata au watapinga. Katika majanga ndio chance kuonyesha uongozi askofu yoyote katika jimbo lolote hapa Tanzania anapaswa kusitisha misa na kuwaongoza maaskofu wenzake katika kufanya maamuzi juu ya corona. Nani anayejua huenda huko mbeleni askofu huyu anaweza kuwa mtakatifu wa korona kwa kuweza kuongoza taifa katika kipindi hichi kuzuia vifo vingi visivyokuwa vya maana.

Mapadri na maaskofu wa katoliki wamekuwa wakiheshimika kuwa elimu ya juu kabisa hivyo haitegemewi wafanye maamuzi kama hawana elimu hiyo. Hivyo wana wajibu wa kulinda heshima hiyo.

Basi endapo wakatoliki watashindwa basi hii ni fursa wa wachungaji wengine kuonyesha umahiri na hivyo kupata heshima kutoka kwa jamii.
 
The Most Winner

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
736
1,000
Sokoni kuna mikisanyiko,Njiani kuna mikisanyiko,kwenye magari vile vile yani upande wa mambo ya mambo ya Kidunia ni fresh tu ila upanfe wa Mambo ya Mungu eti wasitishe hapa ndo unagundua kuwa Shetani anavyofanya kazi kwa kutumia watu kama wewe,Anazuai watu wasisaii ili tushindwe kumshinda Nguvu ila mambo mengine yakiendelea

Na mtu bila kujitambua anakuja na hoja weak kama hizi,!mbona hujashauri Mikusanyiko sokoni au njiani,au migahawani au kwenye vijiwe vya kahawa isitishwe? Kibaya zaidi anaweka hofu huyo shetani.

Nguvu ya pekee kumshinda huyu shetani ni sara a maombi, Watu wapate dawa au chanzo halisi kupitia wasayansi au madoctor Mungu aliowaweka.

Ndugu jitambue
 
bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
237
250
The Most Winner

Mbona ipo wazi kabisa, na sio siri kwamba watu wanaweza ishi pasipo sala lakini hawawezi ishi pasipo chakula.

Hapa ni kufanya maamuz yenye ujinga kidogo kuliko kuchagua ujinga mkubwa
 
Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,171
2,000
Baadhi ya makanisa yameweka utaratibu unaowezesha watu kutokaribiana bila hata ya mwongozo toka TEC.
Hii inasaidia hata muumini anasali kwa amani.
 
Kertel

JF-Expert Member
May 11, 2012
4,021
2,000
Sokoni kuna mikisanyiko,Njiani kuna mikisanyiko,kwenye magari vile vile yani upande wa mambo ya mambo ya Kidunia ni fresh tu ila upanfe wa Mambo ya Mungu eti wasitishe hapa ndo unagundua kuwa Shetani anavyofanya kazi kwa kutumia watu kama wewe,Anazuai watu wasisaii ili tushindwe kumshinda Nguvu ila mambo mengine yakiendelea

Na mtu bila kujitambua anakuja na hoja weak kama hizi,!mbona hujashauri Mikusanyiko sokoni au njiani,au migahawani au kwenye vijiwe vya kahawa isitishwe? Kibaya zaidi anaweka hofu huyo shetani.

Nguvu ya pekee kumshinda huyu shetani ni sara a maombi, Watu wapate dawa au chanzo halisi kupitia wasayansi au madoctor Mungu aliowaweka.

Ndugu jitambue
kwamba tumtangulize sara shetani atajiziuka kushangaa uzuri wa sara?au mimi nimechanganyikiwa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom