Kanisa Katoliki Tanzania hizi ‘ Kero ‘ tunazokutana nazo katika ‘ Jumuiya ‘ litafutieni ufumbuzi wa haraka

Nalipenda sana na mno Kanisa langu Kuu la Katoliki na nawashukuru kwa Mafunzo yenu mliyonipa tokea nilipokuwa Mdogo na Kujijua Mimi ni Mkatoliki na hadi kupata Kwangu Ubatizo na Komunio ya Kwanza japo bado hadi Uzee huu unaonianza nadaiwa Kipaimara ila nashukuru kusikia kwamba mmelegeza Masharti kwamba naweza Kuipata hata wakati nafunga Ndoa yangu kama nitabahatika Kumpata huyo Mwanamke wa Kumuoa.

Ila kama kwa miaka hii 15 iliyopita kuna Kitu ambacho ‘ Kinanikwaza ‘ sana Mimi ‘ Muumini ‘ wenu GENTAMYCINE ni suala zima la ‘ Jumuiya ‘ na mambo ambayo huwa nakutana nayo na niliwahi kukutana nayo ambayo yamesababisha sasa niwe Kando Kidogo ya ‘ Ukatoliki ‘ japo najua siwezi Kuukwepa huu ‘ Ukatoliki ‘ wangu.

Kanisa Katoliki Tanzania leo naomba mniambie Mimi ‘ Muumini ‘ wenu haya ‘ Mamlaka ‘ kuwa kama hushiriki na hauhudhurii ‘ Jumuiya ‘ au huna ‘ Jumuiya ‘ ukifa / ukifariki Kanisa Katoliki halikuziki na hutofanyiwa ‘ Maombi ‘ mlipewa lini na wapi na Mwenyezi Mungu Baba Muumba Wetu?
Hivi ‘ Kumfokea ‘ Mkatoliki kuwa ahudhurie ‘ Jumuiya ‘ ndiyo Kulikuza Kanisa na Kupata Baraka za Mwenyezi Mungu? Na mnavyotutisha kuwa kama hatuhudhurii ‘ Jumuiya ‘ zenu basi tukifa kama siyo kufariki hatuendi Mbinguni mlikaa Kikao chenu hiki na Mwenyezi Mungu lini kisha mkaja na haya ‘ Maazimio ‘ ya Kutishana na Kukomoana hivi?

Hivi Kanisa Katoliki Tanzania mmeshawahi Kufanya Utafiti Wenu wa Kina ili Kugundua ni kwanini akina GENTAMYCINE na Wenzake Siku hizi hawana habari kabisa na ‘ Jumuiya ‘ zenu? Mmeshajiuliza ni kwanini Wakatoliki wengi leo hii ‘ wanahamia ‘ rasmi Makanisa ya Kiroho japo na kwenyewe huko kuna baadhi kuna ‘ Matatizo ‘ haya yaliyopo huku ‘ Ukatolikini ‘ Kwetu yana afadhali?

Najua kila Mtu anaweza akawa na Sababu zake za Kuchukia au Kutohudhuria ‘ Jumuiya ‘ zenu za Kikatoliki ila Mimi GENTAMYCINE sababu zangu Kuu ni kama zifuatazo: 1.Michango ya nenda rudi huku mingine ikiwa haina Kichwa wala Miguu, 2. Majungu Kuzidi ndani ya ‘ Jumuiya ‘ zenu Kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu, 3. Viongozi wengi wa hizi ‘ Jumuiya ‘ zenu kuwa na ‘ Makandokando ‘ mengi kinyume na kile ambacho wanatuhubiria mara kwa mara, 4. Lugha ya Ukali na Vitisho kwa Sisi ‘ Waumini ‘ wenu ambayo ni tofauti kabisa na Lugha ya Kiupendo aliyokuwa nayo Mkombozi Wetu Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai, 5. Waumini wengi wa ‘ Jumuiya ‘ zetu kutumia muda Wao mwingi ‘ Kuchunguzana ‘ kuliko Kusikiliza na Kujifunza zaidi neno la Mungu, 6. Unafiki mwingi na usiojificha ndani ya hizi ‘ Jumuiya ‘ zetu ambayo nasikitika Injili ya Mungu bado haijaweza hadi leo Kulimaliza hili tatizo na 7. Ubaguzi na Upendeleo baina ya Waumini na Waumini wa katika ‘ Jumuiya ‘ husika hali ambayo imekuwa ni ‘ Kwazo ‘ kwa wengieneo.

‘ Jumuiya ‘ za Kikatoliki zikianza kuwa Rafiki na hayo ‘ Makwazo ‘ yangu Saba ( 7 ) tajwa hapo yakitatuliwa na yakiwa hayapo Mimi GENTAMYCINE hata Kesho nitaanza rasmi kuwa ‘Active Mkatoliki ‘ na nitalifurahia Kanisa kama ambavyo nilikuwa nikilifurahia Kipindi cha Miaka ya mwishoni ya 80 wakati nikiwa napata ‘ baraka ‘ za mara kwa mara mida ya mchana kutoka kwa Hayati Kadinali Laurean Rugambwa pale Oysterbay Kanisani na katika ile Shule yao ya ‘ Chekechea ‘ ya St. Peters.

Kama kuna mahala popote nitakuwa ama nimewakosea au nimewakwaza nawaombeni radhi / msamaha.

Nawasilisha.
Kila kitu kina utaratibu wake kama unaona haifai tafuta au anzisha kanisa lako. Hata hapa JF au Klabu ya Pombe kuna utaratibu
 
Dini ni utumwa, dini sio Mungu, tusichanganye, kumuomba Mungu sio lazima uwe dini fulani, na tuukatae utumwa wa kupelekeshwa na hizi dini, hizi dini zililetwa na wazungu na waarabu, mbona mnasahau historia ya miaka 100 hadi 200 tu iliyopita..!!
MUNGU AKUSAMEHE SANA NA UKUONGOZE ....DINI SIO UTUMWA ILA DINI NI NJIA YA KUFIKIA MALENGO YALIYOEKWA NA ALIYEKUUMBA WEWE , AMBAYE AMEKUPA AKILI, NA UMBO ZURI SANA LA KUPENDEZA ...MUNGU AMEWEKA MASHARTI YAKE KWAMBA LAZIMA ABUUDIWE HILI SILO OMBI BALI NI LAZIMA ....MUNGU (ALLAH ) ANAKUBALI KBXA KUWA DUNIA INA DINI NYINGI SANA TENA SANA ILA DINI PEKEE ALOICHANGUA NA AKAPENDEZWA NAYO NI UISLAM...NA KWA UPANDE WANGU SIJAONA DINI YA AJABU NA NZURI KAM UISLAM , NA KAMA MTU ANAHITAJI KWEL KUFNYA UTAFITI BILA USHABIKI ACHUNGUZE HILO, THEN ATANIAMBIA .. MUNGU AWAAJALIE MUWE WAISLAM ..AMIN
 
Huu ni ukweli na wamezidi majungu.
Wengine tunapigwa majungu tangia tukiwa watoto, na huu utu uzima wangu nitapenda kwenda kweli?
Na wana matabaka hiyo ni kweli. Kuna watu wanaonekana bora kuliko wengine na sababu kuu ni pesa.
Na kanisa lisifikiri kwamba litasimama kwa kutishia watu kutowazika kila kukicha badala ya kutatua haya matatizo.
Itafikia muda watu hawatatishika na ndo itakuwa mwanzo wa kuharibika kwa kanisa.
Mimi ninaamini Kanisa halijui haya mambo.
Na haya malalamiko ninaami yatafanyiwa kazi humu hawakosekani baadhi ya viongozi.
Kwa kweli wanakatisha sana Waumini tamaa ya kumwabudu Mungu
 
Taratibu hazina mantiki mpaka sisi wenyewe kwa wenyewe tunalalamika kina shida
Taratibu zinawekwa na kanisa ikiwemo jumuia hivyo kama kuna shida ni vizuri kupeleka malalamiko kunakohusika. Pia kumbuka wengi wape kama wengi wamekubaliana na utaratibu huo huwezi kuubadirisha wewe pekee yako. Jaribu kuwashawishi la sivyo badilisha au anzisha kanisa lako kama wakina Kakobe dada!
 
MUNGU AKUSAMEHE SANA NA UKUONGOZE ....DINI SIO UTUMWA ILA DINI NI NJIA YA KUFIKIA MALENGO YALIYOEKWA NA ALIYEKUUMBA WEWE , AMBAYE AMEKUPA AKILI, NA UMBO ZURI SANA LA KUPENDEZA ...MUNGU AMEWEKA MASHARTI YAKE KWAMBA LAZIMA ABUUDIWE HILI SILO OMBI BALI NI LAZIMA ....MUNGU (ALLAH ) ANAKUBALI KBXA KUWA DUNIA INA DINI NYINGI SANA TENA SANA ILA DINI PEKEE ALOICHANGUA NA AKAPENDEZWA NAYO NI UISLAM...NA KWA UPANDE WANGU SIJAONA DINI YA AJABU NA NZURI KAM UISLAM , NA KAMA MTU ANAHITAJI KWEL KUFNYA UTAFITI BILA USHABIKI ACHUNGUZE HILO, THEN ATANIAMBIA .. MUNGU AWAAJALIE MUWE WAISLAM ..AMIN


Ulaaniwe ww mtumwa usiyejua lolote, mentally crippled
 
Uo utaratibu hauko kwa katolik tu hata lutheran upo,tunaamin jumuiya ndo msingi wa kanisa mambo yote yanaanzia kwenye Jumuiya nahis lengo la kuweka jumuiya halikuwa baya na hayo yanayojitokeza n changamoto ambazo hazihusian na kanisa n suala la wanajumuiya lenyewe
Uwepo wa jumuiya unarahisisha kazi ya kanisa mfano watu wanaohitaj huduma mbali mbali za kiroho na hata kimwili wanapeleka taarifa kanisan kupitia viongoz wao jambo ambalo inakuwa n rahis kuliko angekuja muumin.mmoja Mmoja
Pili kuna maswala mengine n madogo yawe ya kijamii,na hata kiuchum yanaweza kutafutiwa ufumbuzi kupitia jumuiya hii inapunguz mzigo kwa kanisa
pia,Jumuiya inawaleta watu pamoja mnapokuwa na utaratbu wa kukutana kijumuiya inaleta ukaribu fulan unajua fulan ndo nakaa naye mtaa fulan na mnaweza kusaidiana hvo mfano jana niliona harus mtu amemaliza kufunga ndoa jumuiya kama jumuiya imemfanyia bonge la part wakat yeye hkuwa na uwezo
Mwisho jumuiya n muhmu sana hasa kwa watu wanaoishi mjini bora hata vijijn watu wapo karibu sna

Sasa kama Mkeo uliyemuoa anajua kabisa kuwa hukuwa na Uwezo wa Kugharamia Harusi yako na Yeye ila ni kwa Msaada tu wa wana ' Jumuiya ' hivi Siku ikitokea Kiongozi wa hiyo ' Jumuiya ' anamtaka Kimapenzi unadhani huyo Mwanamke / Mkeo atachomoa Kwake? Vitu vingine ni Kujidhalilisha tu kwani kama huna Uwezo wa Kuoa ni lazima Uoe? Ni Wapi katika Katiba ya nchi au Vitabu vya Dini vimeandikwa kuwa Mwanadamu ni lazima aoe?
 
POLE SANA NDUGU YANGU...KARIBU SANA KATIKA DINI ISIYO NA SHAKA HATA KIDOGO , NDIO DINI PEKEE AMBAYO MUNGU (ALLAH) AMEICHAGUA KUWA NDIO YA HAKI , DINI ISIYO KUWA NA UBABAISHAJI WALA KASORO .WALLAH NDUGU ZANGU HUWENDA BAADAE MTU AKAJA KULALAMIKA KUWA HAKUWAHI KUAMBIWA KUHUS UKWEL WA DINI YA UISLAM , MIMI NAWAFIKISHIA NA NAWAPENDA DFIO MAAN NAWAMBIA UKWEL KWAMBA UISLAM NDIO DINI PEKEE MUNGU AMBAYO AMERIDHIKA NAYO ..MUISLAM KOKOTE DUNIANI ANAWEZA KUINGIA MSIKITI WOWOTE DUNIAN PALE NA AKAMUELEWA KIONGOZI WA HUO MSIKITI NA AKA SALI HUMO BILA TATIZO LOLOTE LILE.​

Kazi ipo!
 
Hivi unajua misukosuko iliyopitia kanisa katoliki na jinsi lilivyopambana mpk wewe mtoto wa miaka ya tisini ukalikuta?
Hivi waasis wa kanisa katoliki wakiwemo mitume wa Yesu wangengekimbia kanisa kwa changamoto kutoka kwa Warumi Leo hili kanisa ungelikuta?

Hivi unaelewa maana ya kanisa katoliki takatifu la mitume na mamlaka yake? Unafikiri hizo tozo na amri ya kutozikwa imeanzia na kuishia hapo kurasini tu.

Nabora umezaliwa enzi hizi wakati kanisa limeshasimama, wewe ungezaliwa enzi za mashahidi wa Uganda ungemkana Yesu wewe. Acha kulia Lia hiyo ndio kazi ya utume.
Kanisa lipo jana,leo na hata kesho. Leo hii tunavyoona kanisa linapitia skendo za aina yake kwa baadhi yetu wala hatushangai. Maana tulitimia nguvu nyingi kuficha matatizo yetu.
Adui wa kanisa hayuko nje ya kanisa kama tunavyopenda kufikiria. Yuko ndani na analiharibu kweli kweli. Kulinda uovu, kupeana madaraka kwa kupendeleana na sio kwa uwezo. Kuzima kwa nguvu wale wote wanaolalama kutaka mambo yaende sawa. Ndio maana leo hii mpaka senior cardinals ndani ya Vatican wamepata misukosiko na scandals....mmoja alikuwa Marekani....na Australia pia tena alikuwa mtu wa karibu sana na Pope.
Misukosuko ya nje itazalisha mashahidi...kama wale wa Uganda. Uozo wa ndani ya kanisa unazalisha nini hebu tuambiane?
 
Kweli dini ni utumwa! Ningekuwa mimi wala siwazi zaidi ya mara mbili, najitoa kwenye hizo jumuiya zao very instantly!

Kwa taarifa tu ni kwamba nina zaidi ya miaka kumi sijakanyaga kanisani! Upumbafu ni mwingi!

Nilidhani nipo peke yangu kumbe tupo wengi tusiopenda huu Utaratibu? Ewe Mwenyezi Mungu tusaidie na tupiganie Sisi ambao tunatishiwa na Viongozi wa ' Jumuiya ' za Kikatoliki kuwa kama hatuwi ' active ' huko basi tukifa / tukifariki ' tujizike ' tu wenyewe ila Kanisa lako Katoliki halitakuwa na muda huo.
 
Kanisa katoliki halina mijadala mitandaoni utaongea weee ila kanisa ni moja, takatifu, katoliki la mitume, wewe hujumuiki na wenzako we ni nan, kasome matendo ya mitume ndipo chimbuko la jumuiya ndogo ndogo, ata ukiama iman yako sio suluisho kanisa ni moja, takatifu, katoliki la mitume. Wengi wameama lakin kanisa litasimama.
Tumsifu yesu kristo
 
Sasa kama Mkeo uliyemuoa anajua kabisa kuwa hukuwa na Uwezo wa Kugharamia Harusi yako na Yeye ila ni kwa Msaada tu wa wana ' Jumuiya ' hivi Siku ikitokea Kiongozi wa hiyo ' Jumuiya ' anamtaka Kimapenzi unadhani huyo Mwanamke / Mkeo atachomoa Kwake? Vitu vingine ni Kujidhalilisha tu kwani kama huna Uwezo wa Kuoa ni lazima Uoe? Ni Wapi katika Katiba ya nchi au Vitabu vya Dini vimeandikwa kuwa Mwanadamu ni lazima aoe?
Nadhan mkuu ungejikita zaid kwenye point yangu kuliko kuchukua mfano ambao nmeelezea kuhusu jumuiya kwa mfano hyu mtu so kwamba ilikuwa lazma afanye harus isipokuwa n upendo tu wa wanajumuiya wenzao nasisitiza kwenye point zangu hazikuwa zikielezea suala la ndoa naomba rudia kusoma
 
Watu wanamtaka Mungu bila ushirika wowote, ni kama mnajiumbia mungu wenu ambaye mnaweza kumuabudu mnavyotaka au kujisikia nyinyi. Moja ya hatari kubwa kiroho ni pale unapoisikiliza sana akili yako na kuiamini! Hapo wewe mwenyewe unaelekea kuwa mungu wa maisha yako bila kujua!

Ndio maana wengine wanahangaika na makanisa wakichoka wanaanza kusali majumbani mwao! Kama wewe ni Mkatoliki na hauishi Kikatoliki fahamu kuwa moto wa milele unanukia kwako labda uokolewe kwa neema tu maana huruma ya Mungu haina mipaka lakini ni hatari! Hivyo hivyo makanisa mengine, popote unaposali lazima uwe mshirika kamilifu ili uchote baraka za madhabahu hiyo.

Jumuiya ndio sehemu ambayo nyinyi wenyewe mnaamua nani awe kiongozi, na pia ndio unaweza kutoa maoni yoyote kama kuna vitu havikupendezi, sasa unataka jumuiya ya watakatifu tu? Haipo duniani maana hata Yesu alisema hakuja kwaajili ya watakatifu tu! Wewe unapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko kwenye jumuiya badala ya kulalamika.

Kwa mfano toa hapa orodha ya hizo sadaka tuone ubaya wake! Unafikiri Kanisa linatoa wapi fedha ya kuendesha huduma zake? Nenda kwenye mbao za matangazo uone mapato na matumizi ili uone kazi iliyopo! Kanisa ni mimi na wewe, mipango yote tunapanga wenyewe na jinsi ya kutekeleza hivyo kama wewe hutaki kushiriki kwenye issues za kanisa utapangiwa kila jambo na kuishia kulalamika mitandaoni.
 
Back
Top Bottom