Kanisa Katoliki Tanzania hizi ‘ Kero ‘ tunazokutana nazo katika ‘ Jumuiya ‘ litafutieni ufumbuzi wa haraka

Naona umedai reference kuhusu Mambo hayo ya jumuiya....Ukiendelea kudadavua na kudai reference nyingi utakuta Ni mipango ya watu nasi Mungu (Kitabu)...Huenda kwa hilo ukapata kujua uliposimama Ni wapi.Epukana na NDIYO isiyo kuwa na marejeo ya Bible.
 
Kama ukiwa hai haukutaka kushirikiana na kanisa unategemea ukifa kanisa ndo lishiriki? Utakua umejitenga mwenyewe.
Toa michango ili kusaidia kueneza injili mbona ofa za bia unatoa ila michango midogomidogo ya jumuiya na kanisa unaona ni kero kumbuka kazi iliyokuleta duniani haujaimaliza
 
Uo utaratibu hauko kwa katolik tu hata lutheran upo,tunaamin jumuiya ndo msingi wa kanisa mambo yote yanaanzia kwenye Jumuiya nahis lengo la kuweka jumuiya halikuwa baya na hayo yanayojitokeza n changamoto ambazo hazihusian na kanisa n suala la wanajumuiya lenyewe
Uwepo wa jumuiya unarahisisha kazi ya kanisa mfano watu wanaohitaj huduma mbali mbali za kiroho na hata kimwili wanapeleka taarifa kanisan kupitia viongoz wao jambo ambalo inakuwa n rahis kuliko angekuja muumin.mmoja Mmoja
Pili kuna maswala mengine n madogo yawe ya kijamii,na hata kiuchum yanaweza kutafutiwa ufumbuzi kupitia jumuiya hii inapunguz mzigo kwa kanisa
pia,Jumuiya inawaleta watu pamoja mnapokuwa na utaratbu wa kukutana kijumuiya inaleta ukaribu fulan unajua fulan ndo nakaa naye mtaa fulan na mnaweza kusaidiana hvo mfano jana niliona harus mtu amemaliza kufunga ndoa jumuiya kama jumuiya imemfanyia bonge la part wakat yeye hkuwa na uwezo
Mwisho jumuiya n muhmu sana hasa kwa watu wanaoishi mjini bora hata vijijn watu wapo karibu sna
 
Hzo mnazoona wanafanya kama sheria kwamba kama so mwan jumuiya hupat huduma za kanisa wanataka kuweka msisitizo ili uende jumuiya otherwise lengo so baya wakat mwingine utii bila shurut inakua ngumu
 
Kinachofurahisha ni kwamba waumini wengi wa RC na KKKT wanalalamika sana kuhusu michango kanisani na kwenye jumuiya lakini hao hao ndio watoaji wazuri wa sadaka na michango kwenye hayo makanisa ya kiroho wanayohudhuria baada ya kutoka misa za kwanza kwenye makanisa yao, wengine wanafikia mpaka hatua ya kukopa hela ya sadaka, lakini wakikumbushwa michango midogo ya jumuiya wanalalamika.
Nakule nasikia wanatoa kwa shuruti na classes zipo kam zote
 
Tangu 2009 !!? Huwezi kujiita wewe Ni mkatoliki ila ulikuwa muumini wa katoliki, kweli sheten halali usingiz , mtu ulishaacha kwenda kanisani halafu bado unalalamika? Mimi ninachojua Anglican, Roman Catholic ,KKKT wana taratibu zao ambazo lazima uzifuate Kama zinakuchosha unahama tu kanisa
Umenena vyema alafu sis hatutafti waumin n msukumo ndani yako tu na sadaka hulazimishwi kutoa n ww mwenyewe na roho yako
 
I know you are a very good Catholic, mkuu jaribu kutengeneza urafiki na Padri yeyote hata kama sio paroko wako, ujadiliane nae juu ya hili, ni dogo litakwisha
 
Mku kwenye kuhama sikushauri kwani hakuna jipya zaidi nakushauri usimame na Imani yako ya Kikatoliki ambayo umekuzwa nayo.
Mku kuna faida kubwa sana Mimi nilijkuwa na tabia ambayo nikipata tatizo lolote au nikijihisi siko vizuri kanisa lolote la kilokole nilikuwa naenda kwa ajili ya kuombewa mwisho nililokutana nalo huko Mku ni Mungu aliyeninusuru ndo anajua.
Kanisa katoliki linatakiwa hawa viongozi wa Jumuiya watafutwe wenye hofu ya Mungu na hawa wapo wengi tu.
Katika zile Dekania kuna wale Waumini waliosoma makuzi na malezi ya Kiroho na waliosoma Imani Katoliki kwani hawa ni hazina ya Wakatoliki ndio maana haya makanisa wanayomiliki Watu binafsi wakijua kuwa umeyapata haya malezi sio kazi kukabidhiwa Kanisa kwani wako vizuri kiroho (Karesmatiki)
Na Katoliki ikiwapata hawa watu na kuwapa uongozi hakuna Mkatoliki atayehama katika kanisa katoliki kwani hawa ni sawa na Walimu na Wainjilisti.
Mku kama umekwazika uzuria ktk Ibada ya pale Ubungo Emaunsi nyuma ya Stand kuu kwani kila jumapili kuna misa huwa inaanzaga saa saba na hapo kuna hayo madarasa ya kukulia Imani ya Kiroho kila siku kwani Mimi nilisomaga hapo.
Mimi Kuhama Kanisa ndiyo Suluhisho Mkuu? Kwahiyo kama Muumini Mkatoliki sina Haki yangu ya Kimsingi ya Kulalamika? Nijenge Kiimani ila usinitishe kisha nikazidi Kulichukia Kanisa wakati ndiyo limenilea Kiimani tokea nazaliwa.
 
Hivi unajua misukosuko iliyopitia kanisa katoliki na jinsi lilivyopambana mpk wewe mtoto wa miaka ya tisini ukalikuta?
Hivi waasis wa kanisa katoliki wakiwemo mitume wa Yesu wangengekimbia kanisa kwa changamoto kutoka kwa Warumi Leo hili kanisa ungelikuta?

Hivi unaelewa maana ya kanisa katoliki takatifu la mitume na mamlaka yake? Unafikiri hizo tozo na amri ya kutozikwa imeanzia na kuishia hapo kurasini tu.

Nabora umezaliwa enzi hizi wakati kanisa limeshasimama, wewe ungezaliwa enzi za mashahidi wa Uganda ungemkana Yesu wewe. Acha kulia Lia hiyo ndio kazi ya utume.
 
Ajira gani ambayo unaizungumzia hapa ambayo Mimi sina? Kumbe Kuwa Mfugaji, Mvuvi na Mkulima kama ambavyo nilivyo hiyo siyo Ajira bali Ajira rasmi ni Kuajiriwa Maofisini katika Viyoyozi? Pumbavu.
Gentamycine watu mpaka sasa hivi hawajang'amua kuwa ajira ni utumwa na kulima na kufuga ndo hakuna PAYE, sijui NSSF, sijui ripoti ya mwezi, n.k

Hili la jumuia lipo ila nikwambie ni bora Katoriki kuliko makanisa madogo. Katoliki ukichoshwa na umbea au michango unatulia halafu baada ya muda unarudi unapokelewa. Haya makanisa ya kuja wanakuchunguza kipato chako ole wako usitoe fungu la kumi halafu sadaka ni mali ya mchungaji na familia yake. Lusekelo anasema kuwa maskini ni ufala tu.
 
Kuna ' Kajihisia ' fulani kananiijia nibadili tu Dini niwe Muislamu ila bado natafakari. Waislamu hawana ' Mbwembwe ' na ' Unafiki ' katika baadhi ya ' Religious Doctrines ' zao kama huku Kwetu Ukristoni Mkuu.
[/QUOTE
Okoka, mpe Yesu maisha yako
 
Huu ni ukweli na wamezidi majungu.
Wengine tunapigwa majungu tangia tukiwa watoto, na huu utu uzima wangu nitapenda kwenda kweli?
Na wana matabaka hiyo ni kweli. Kuna watu wanaonekana bora kuliko wengine na sababu kuu ni pesa.
Na kanisa lisifikiri kwamba litasimama kwa kutishia watu kutowazika kila kukicha badala ya kutatua haya matatizo.
Itafikia muda watu hawatatishika na ndo itakuwa mwanzo wa kuharibika kwa kanisa.
 
Kwanza nikupongeze mleta mada
Pili labda nikushirikishe Jumuiya ni azimio la makanisa ya Imani Katoliki la 1973 lililoanza kutekelezwa 1974. Kwa hiyo ni kweli ni geni hasa upande mmoja unapolichulia ni chanzo kimojawapo cha mapato ya kanisa.
Tatu kubali usikibali kwenye jumuiya kuna fursa za huduma nyingi za kimwili na kiroho kuliko changamoto. Kuna mchangiaji ameshauri ujadiri hilo jambo na padre yo yote. Nakubaliana naye kwa msingi kuwa unaweza kukuta hata makanisani hawana uelewa mzuri wa madhumuni ya jumuiya na wanashiriki kuyapotosha.
Nne ninavyokufahamu nashindwa kukuelewa wewe kukimbia uwanja wa mapambano. Nina ushahidi wa Jumuiya za Imani Katoliki zilizovuka changamoto hizo.
a Walijifunza kwa kina historia ya Jumuiya na kuielewa.
b. Walitafuta mambo gani ya kijumuiya yanayopaswa kutekelezwa kama ni michango shirikishi ya kulijenga kanisa.
c. Walibainisha fursa za kimwili na kiroho walizonazo wanajumuiya kwa eneo walipo.
d. Hoja zote na majadiriano yaliongozwa na biblia na maagizo ya kikanuni ya kanisa yenye makubaliano bayana.
e. Walishirikiana mwongozo wenye makubaliano na Baraka za pande zote.

Nahitimisha kwa neno moja zito ninaloliamini
DHUMUNI KUBWA LA JUMUIYA NI KUKABILIANA NA UPOTOSHWAJI WA KIIMANI KUANZIA MITAANI. LINAFANIKIWA KWA KUWASHIRIKISHA WAUMINI KWENYE MAENEO YAO KUWA NA FURSA ZA KUJIFUNZA N.A. KUITUNZA IMANI YAO.
Jichunguze kama hutaki KUJIFUNZA na KUITUNZA Imani yako.
 
Kuna ' Kajihisia ' fulani kananiijia nibadili tu Dini niwe Muislamu ila bado natafakari. Waislamu hawana ' Mbwembwe ' na ' Unafiki ' katika baadhi ya ' Religious Doctrines ' zao kama huku Kwetu Ukristoni Mkuu.
POLE SANA NDUGU YANGU...KARIBU SANA KATIKA DINI ISIYO NA SHAKA HATA KIDOGO , NDIO DINI PEKEE AMBAYO MUNGU (ALLAH) AMEICHAGUA KUWA NDIO YA HAKI , DINI ISIYO KUWA NA UBABAISHAJI WALA KASORO .WALLAH NDUGU ZANGU HUWENDA BAADAE MTU AKAJA KULALAMIKA KUWA HAKUWAHI KUAMBIWA KUHUS UKWEL WA DINI YA UISLAM , MIMI NAWAFIKISHIA NA NAWAPENDA DFIO MAAN NAWAMBIA UKWEL KWAMBA UISLAM NDIO DINI PEKEE MUNGU AMBAYO AMERIDHIKA NAYO ..MUISLAM KOKOTE DUNIANI ANAWEZA KUINGIA MSIKITI WOWOTE DUNIAN PALE NA AKAMUELEWA KIONGOZI WA HUO MSIKITI NA AKA SALI HUMO BILA TATIZO LOLOTE LILE.​
 
Mkuu umenifurahisha sana nilifikiri ni mimi tuu nachoshwa, kutoa zaka mpaka ukajoandikishe na jumuiya, nyumba za kupanga kila siku tunahama mjina hapa kila siku kutafuta jumuia na ugeni wa mazingira na hiyo adhabu ya kutofanua ibada baada ya kufariki nikwanini wanahukumu? Mungu pekee anaestahili kuhukumuu, nataka kupeleka zaka lkn nawaza naanzia wapiii
 
POLE SANA NDUGU YANGU...KARIBU SANA KATIKA DINI ISIYO NA SHAKA HATA KIDOGO , NDIO DINI PEKEE AMBAYO MUNGU (ALLAH) AMEICHAGUA KUWA NDIO YA HAKI , DINI ISIYO KUWA NA UBABAISHAJI WALA KASORO .WALLAH NDUGU ZANGU HUWENDA BAADAE MTU AKAJA KULALAMIKA KUWA HAKUWAHI KUAMBIWA KUHUS UKWEL WA DINI YA UISLAM , MIMI NAWAFIKISHIA NA NAWAPENDA DFIO MAAN NAWAMBIA UKWEL KWAMBA UISLAM NDIO DINI PEKEE MUNGU AMBAYO AMERIDHIKA NAYO ..MUISLAM KOKOTE DUNIANI ANAWEZA KUINGIA MSIKITI WOWOTE DUNIAN PALE NA AKAMUELEWA KIONGOZI WA HUO MSIKITI NA AKA SALI HUMO BILA TATIZO LOLOTE LILE.​
Eeeh, asante
 
Kweli dini ni utumwa! Ningekuwa mimi wala siwazi zaidi ya mara mbili, najitoa kwenye hizo jumuiya zao very instantly!

Kwa taarifa tu ni kwamba nina zaidi ya miaka kumi sijakanyaga kanisani! Upumbafu ni mwingi!
 
Dini ni utumwa, dini sio Mungu, tusichanganye, kumuomba Mungu sio lazima uwe dini fulani, na tuukatae utumwa wa kupelekeshwa na hizi dini, hizi dini zililetwa na wazungu na waarabu, mbona mnasahau historia ya miaka 100 hadi 200 tu iliyopita..!!

 
Back
Top Bottom