kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
KATIKA kile kinachoonekana kuithibitishia jamii kuwa nyumba za ibada si mahala pa siasa, Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga limewafukuza na kuwazuia kushiriki shughuli za kanisa zaidi ya waumini wake 400 wanaotuhumiwa kuisaliti imani ya kanisa hilo kwa kukishabikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni.
Miongoni mwa waumini wanaotajwa kuwa wamesimamishwa na kanisa hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hipolitus Matete na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sumbawanga, Charles Kabanga.
Habari za uhakika ambazo HABARILEO Jumapili imezipata zinasema kwamba, uamuzi huo wa kanisa umelenga kujisafisha na 'kashfa ya kuegemea upande fulani wakati wa kampeni na baadaye uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Chanzo chetu cha habari kimepasha kwamba, wanaCCM hao wanaotuhumiwa na kanisa hilo wanahusika kufanya mikutano ya ndani, kuvaa sare za chama hicho na kumshabikia waziwazi aliyekuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika Jimbo la Sumbawanga Mjini,
Aeshi Hilaly.
Kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu huo mgombea ubunge wa CCM, Aeshi aliibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi dhidi ya mgombea wa Chadema, Norbet Yamsebo ambaye kwa sasa amekata rufaa Mahakama Kuu mjini hapa kupinga matokeo hayo.
Inaelezwa kwamba, mgogoro wa kiimani baina ya Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga Mjini na waumini wake ambao ni wanaCCM, umetokana na waumini hao kupuuzia agizo la kanisa la kutomshabikia Aeshi kwa madai kwamba, alikufuru imani ya kanisa hilo kwa kujifananisha na Mwana wa Mungu, Yesu Kristu.
Baadhi ya viongozi wa kanisa jimboni humo wamekuwa wakimtuhumu mgombea huyo wa CCM pale alipodai katika moja ya mikutano yake ya kampeni kwa kufananisha mafiga matatu na Utatu Mtakatifu ambao mgombea huyo anadai kuwa alikufuru imani hiyo kwa kumfananisha mgombea Urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kama Mungu Baba, mgombea ubunge kama Yesu Kristu mwana wa Mungu na wagombea Udiwani sawa na
Roho Mtakatifu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Rukwa, Kapteni Fratern Kiwango amethibitisha kutengwa kwa wanachama wa chama hicho ambao ni waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga.
Ni kweli hadi sasa kanisa hilo limewafukuza na kuwazuia wanaCCM zaidi ya 400 kupokea sakramenti zozote kwenye Kanisa Katoliki la hapa, alisema Kapteni Kiwango aliyewataja baadhi ya waliofukuzwa na kusimamishwa kuhudhuria ibada za misa takatifu kuwa ni pamoja na Matete, Kabanga, dereva wa Katibu wa CCM mkoa wa Rukwa aitwaye Vitalis Kalwangwa na mkewe na Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Majengo, Christina Tinde.
Inadaiwa kuwa waumini hao ni kutoka kanisa la Familia Takatifu lililopo Chanji mengine ni Kristu Mfalme , Katandala na Kanisa la Kiaskofu lililopo Mazwi mjini hapa ambapo kanisa lililopo kijiji cha Mlanda limefungwa na waumini wake wote wamezuiwa kupata
huduma yoyote ya kiroho kwenye kanisa hilo.
Inadaiwa kuwa pamoja na kuzuiwa kuingia makanisani na kuhudhuria ibada ya misa takatifu waumini hao wamezuiwa pia kupokea sakramenti zozote katika Kanisa Katoliki.
Pia wamezuiwa kupata huduma za kiroho kanisani zikiwemo kufunga ndoa, kubatizwa au kupata kipaimara na pia kufanyiwa ibada wakati wa maziko hadi hapo suala lao litakapopatiwa ufumbuzi ambapo itategemewa zaidi jitihada zao binafsi na huruma ya Mungu.
Mwandishi wa habari hizi alisoma baadhi ya nakala za barua za kuwasimamisha kupokea sakramenti kwenye kanisa hilo zilizosainiwa na Paroko wa Kanisa la Kristu Mfalme, Padri Pambo Mlongwa.
Sehemu ya barua hiyo inasema; "Kufuatia mwenendo mbovu wakati wa uchaguzi mkuu, huku ukiendekeza vitendo vya rushwa na usaliti wa imani Katoliki.
Kwa heshima ya Mungu wetu na utatu mtakatifu wa kanisa, Mama kanisa Mtakatifu kwa nguvu ya Sheria ya kanisa CIC 13669, CIC1389,CIC 13712 na CIC 1391 naagiza usipokee sakramenti zozote katika Kanisa Katoliki tekeleza amri hii mara umalizapo kuisoma barua hii.
Padri Pambo alipohojiwa kwa njia ya simu ili kupata ufafanuzi zaidi wa suala hilo alisema kwamba, yuko mbali sana ambako hataki mtu yeyoye ajue aliko.
"Sawa mimi ni kiongozi wa kiroho kwa sasa sitaki kabisa mtu yeyote hata wewe ujue wapi nilipo, niko mbali sana kwa sasa nakushauri nenda ofisini ni suala la kiofisi hilo kwa sasa sina majibu yake, alisema kiongozi huyo wa kiroho.
Lakini kabla ya mawasiliano ya siku hiyo, kwa nyakati tofauti Padri Pambo alipokuwa
akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alikiri kuwa mgombea wa CCM, Aeshi alikuwa amekufuru imani na Kanisa Katoliki kwa kujifananisha na Yesu Kristu Mungu Mwana ambapo Kanisa liliwasilisha malalamiko yake kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuja mjini hapa kumnadi mgombea huyo, lakini hawakuweza kufikia mwafaka.
Pia zimekuwa taarifa mjini hapa kwa Padri Pambo amekimbia kanisa lake la Kristu Mfalme kwa kile kinachodaiwa kuwa amekwenda kujificha kusikojulikana ili kukwepa hasira za waumini wa kanisa hilo wanaopinga kufukuzwa kwa wenzao kwa sababu ya itikadi zao za kisiasa.
Naye Paroko wa Kanisa la Kiaskofu mjini Sumbawanga, Padri Deo Simemba hivi karibuni alipohojiwa na gazeti hili alikiri kuwa kanisa limeanza kuwasimamisha baadhi ya waumini wake kwa kile alichodai kuisaliti imani ya Kanisa Katoliki.
Kutokana na tukio hilo, Katibu wa CCM wa Mkoa amelitahadharisha kanisa hilo kwa kujiingiza kwenye malumbano ya kisiasa.
Baadaye, gazeti hili liliwasiliana na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde ili aweze kulizungumzia suala hilo na alipopatikana kwa njia ya simu alisema:
Kwa nafasi yangu, naweza kusema sijui lolote kwa sababu sijapata taarifa rasmi na inawezekana kwa kuwa katika siku za hivi karibuni nilikuwa na vikao vingi pamoja na kuhudhuria mafahali pale Chuo Kikuu cha Madaktari Bugando (Mwanza).